Uchaguzi 2020 Tundu Lissu kutinga Chato keshokutwa

Mkuu takwimu zako zina changamoto. Wagombea walioenguliwa maybe 40 maana 30% walirudishwa. Na wagombea hawakuwekwa pemba tu ila unguja waliweka.
Kwa hyo kwenye majimbo 264 hawana wagombea majimbo say 60!! Meaning wanan wagombea 200+ ambayo ni zaidi ya wagombea waliosimamisja 2010 na 2015 (waliachiana majimbo).

Nilitaka kuweka rekodi sawa tu
 
Mgawanyo wa hivyo viti maalum nao unaweza kuleta tafrani kutokana na uchache wa viti watakavyopata.
Watarank wagombea kutokana na kura walizopata majimboni. Pia viongozi wa mabaraza wataingia by default. But all in all kura za viti maalim haziamuliwi na wingi wa majimbp ulioshinda bali jumla ya kura zote za wagombea.

Ndio maana 2015 walikua na viti 36 tu ila viti maluum zaidi ya 40+ . mfano mdee akianguka ila kazoa kura elfu 80 hiyo elfu 80 inaleta kiti maalum hata viwili licha ya kwamba jimbo hajashinda.

Kwa mahesabu hayo walau hawakosi viti maalum 20+ unless maeneo yenye kura nyingi wasiwe hta washindi wa pili
 
Utaratibu mzuri sana, japo sina hakika kama hawawezi kuchepuka na kufanya maamuzi nje ya utaratibu huo. Tulishuhudia 2015 mke wa Lowasa akipewa ubunge, sina hakika kama ile ilikuwa ndani ya utaratibu.
 
Leo Dk Magufuli Yuko saa hii Kinyerezi Segerea akifanya kampeni huyo hapo
 
Chato siyo ngome ya Magufuli kilichomfanya awe mbunge kwa miaka 20 mfululizo ni kupita bila kupingwa tu.

2014 - 2019 Serikali zote za mitaa pale Chato zilikuwa chini ya upinzani.

Uchaguzi wa 2015 Kalemani alishinda kwa margin ya 56% kwa 44 ya mpinzani na hapo baada ya kufanya figisu.

Lowassa alipoenda chato alikuwa na watu wengi kuliko Magufuli licha ya mkutano wa Magufuli kuambatana na mzee Mkapa na ccm yote.

Na malori yalibeba watu wengine kutoka Kibondo mpaka Bukavu na bado alizidiwa watu na Lowassa.

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Mgawanyo wa hivyo viti maalum nao unaweza kuleta tafrani kutokana na uchache wa viti watakavyopata.
Wataanza mahawara na vimada kwanza, halafu wake wa viongozi, mke wa Lissu, mke wa john mrema, kimara wa mbowe etc
 
Utaratibu mzuri sana, japo sina hakika kama hawawezi kuchepuka na kufanya maamuzi nje ya utaratibu huo. Tulishuhudia 2015 mke wa Lowasa akipewa ubunge, sina hakika kama ile ilikuwa ndani ya utaratibu.
Sio mbaya hta akipewa ubunge afterall kma mme akishinda angekua by-default Mjumbe wa kamati kuu na first lady.

Elimu yake inaeleweka pia alafu anaweza kuwa sauti ya Lissu ndani ya bunge hasa kupinga miswada mibovu kipengele Kwa kipengele. Kwahiyo maadam vigezo anavyo sioni shida akipewa shavu
 
Mkuu, hii ipo kwenye katiba?!
 

Lissu asipokwenda Chato kama ratiba ya NEC inavyoonyesha itatafsiriwa kuwa amemuogopa JPM. Atakuwa amepoteza nguvu ya kampeni yake inayosimama kwa yeye kuwa mtu wa pekee mwenye jeuri ya kupambana na JPM nchini. Akionyesha uoga tu, amekwisha.
 
Ni kweli flyovers hazi msaidi lolote kwa mwananchi wa kawaida, labda kwa ajili ya kupigia picha na kufungia harusi labda akiingia yeye na kuleta city trains na maeneo ya wazi alisikika mgombea moja
 
Aje lkn kwa adabu - akikashifu rais wetu hatutakubali - huku ni kwa wastarabu hivyo ajenge hoja kistarabu
 
Huko kote washamaliza kazi. Kinachofanywa ni kwenda sehemu ambazo bado zimelala kuhakikisha Magufuli hapati hata 5% ya kura, so they say.
humo mijini alimozunguka Lisu ndimo apate asilimia nyingi? Asilimia nyingi asilimia 80 ya wapiga kura wako vijijini tena ndani ndani hasa ,Mijini anamozurua Lisu so far anahangaika na asilimia 20 tu ya wakazi wa mijini ambamo CCM ni jogoo mkubwa tena sana

LISU hana jipya labda useme anatafuta 95 percent ya asilimia 20 ya wakazi wa mijini na miji midogo ambayo si rahisi kuipata hata angefanyaje

Kampeni zinaisha siku 13 kuanzia leo hana uwezo wa kuzunguka vijiji vyote Tanzania hata akitaka.Huyu ni mgombea wa kutafuta kura kwenye barabara za lami za Magufuli kwenye miji mikubwa baadhi na midogo

Ukiangalia roadmap ya kampeni anazunguka tu mle Lowasa alipita tu bila kuangalia kuwa mazingira yamebadilika sio yale tena ya Kipindi cha Lowasa na Slaa.Ndio maana alijitia kuzindulia naye kampeni Dar akimwiga LOWASA likamdodea hasa!!!

Ona uzinduzi wa Lowasa DAR jangwani 2015 PICHA zilipigwa na DRONE


Angali uzinduzi wake alipoiga Lowasa Dar ukamdodea ona hii aibu ya Lisu umati wake pamoja na kuweka wasanii


Lisu akajitia kuiga kufanya uzinduzi Dar MBAGALA ona umati wake!!!!
 
Akienda chato atapita zaidi ya majimbo kumi na saba kabla hajafika chato na akitoka chato atapita Rorya Simiyu then Kilimanjaro na Arusha kwa vyovyote vile atapita tena kwenye hiyo mikoa ya kimkakati.

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
wewe LISSU hajiendei tu, kapangiwa na NEC kule.
 
Wewe acha ujinga nafwata ratiba ya NEC
Huyu kibaraka sasa naona hana sera kabisa! Anahangaika kama maharage yakiwa kwenye sufulia ya kipikwa lakini tarehe 28/10/2020 yataiva tu. Anafikiri urais ataupata kupitia Kanda ya Ziwa asahau kabisa anapoteza muda wake tu huyu kibaraka wa mabeberu!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…