Haya tena kile chuma cha pua kwenye ubora wake kitakuwepo ITV kumwaga shule.
Wengine wanakiita Simba.
Wengine hawachoki kukifanyia fitna.
Ama kwa hakika wengine kwetu huyu:
View attachment 3079045
Ndiye yule mwanetu mpendwa tunaye pendezwa naye!
Hadhara hizi zianze kuwa na mpangilio maalum ya kuongelea maswala mazito yanayo ikabili nchi yetu sasa hivi. Hii iwe fursa ya kuanza kuwafahamisha wananchi mwelekeo inakopelekwa nchi hii.
Kwa mfano:
Kama itampendeza Tundu Lissu, binafsi ningeomba azungumzie maana halisi ya maigizo haya ya kubadili mawaziri kila mara anako fanya huyu 'Chura Kiziwi'.
Kwa maoni yangu ni kwamba huyu mwanamke anatumia njia hiyo kuwatia woga mawaziri hao.
Chukulia alivyo fanya kwa kuwapumzisha Kabuti na mwenzake Lukubi; halafu anawarudisha kana kwamba alikuwa amewapeleka kuchukuwa mafunzo mahli!
Hii ni mbinu ya kuwashughulikia hawa viongozi, halafu anapoona ni hao hao atakao wategemea kumrudisha madarakani, anakimbia haraka kuwarudisha. Hali ni hiyo hiyo hata katika ngazi nyingine za uongozi ndani ya chama na serikalini. Akina Makonda ni mfano halisi.
Jambo la pili ambalo ningeomba atafute njia za kulizungumzia ili wananchi walielewe, ni hili la huyo mwanamke kujipa 'u'Chura Kiziwi' eti asisiskie kelele za waTanzania, huku akiendelea kufanya uharibifu mkubwa kwa nchi yetu.
Huku ni kuwadharau watu anao waongoza.
Hili linafaa kuelezwa kwa wananchi walielewe vizuri kabisa. Hii nchi hatuwezi kuswagwa tu kama mifugo.
Mfano hapa ni: Pesa ya kuwahamisha Maasai ilitoka wapi, na uamzi wa kuhamisha raia wa nchi hii mjadala wake ulifanyika wapi na lini.