Tundu Lissu: Magufuli alitufanyia mambo mabaya lakini hakufanya biashara na Rasilimali za Nchi

Absolutely.
Ni kweli kabisa kwamba JPM ana mabaya yake, tena ni mengi tu, lakini kuhusu suala la kuuza nchi kwa raia wa kigeni KAMWE HAHUSIKI.

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
Ndio hapo watu wanapopaswa kumuamini Tundu Lissu kuwa SIO MTU WA KUSEMA UONGO.
Hulka ya Lissu ni kukemea lile baya bila kumchukia mtendaji, ni wazi hakunchukia Magufuli hata kama alitaka afe bali alichukia matendo yake vinginevyo asinge mtetea katika hili.
 
Wakati mwingine huwa najiuliza ni kipi kilichomsukuma aliyevujisha ule mkataba akafanya vile?

Kwasababu hawa jamaa wamekuwa wakituchezea kwa mikataba ya hovyo miaka mingi sana, kwanini huu wa bandari ukawa mwisho wa kufichwa?

Nikaona inawezekana mpaka aliyeamua kuvujisha, nikiamini kabisa ni mwenzao, anayewezekana akawa anakula 10% nao.

Lakini alivyoona huu wa bandari hauna ukomo, waarabu watakuja kujitawala ndani ya nchi yetu, na uwepo wao hautakuwa na faida yoyote kiuchumi kwetu, wanakuta mazingira yote wameshatengenezewa, wao ni kuchuma faida na kupeleka kwao milele!, jamaa akaona hapana, kwa hili nawasemea kwa wenye nchi yao.

Ndio akauvujisha mkataba wa hovyo kabisa kuwahi kutokea katika historia ya nchi yetu.
 
Hebu Kwanza.

Hivi ile nyaraka ya "Makubaliano" (inayohusu IGA), kumbe ilivujishwa?

Mimi nikadhani kuwa labda kwa vile ililazimu kupitishwa Bungeni kama maigizo, ikawalazimu waitoe na ndipo wananchi walipojionea mambo ya ajabu kabisa?

Sasa serikali inasema waziwazi, kwamba "Mkataba" utakaofuata kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali, hiyo itakuwa ni siri; haitatoka nje watu waone kilichomo ndani ya mikataba hiyo.

Kama 'IGA' imekuwa mbovu kiasi hiki, hiyo mikataba itakayokuwa siri tutegemee mambo mazuri kweli kwa taifa letu?

kama kweli jambo hili litapita hivi hivi na kuendelea mbele, nitaishangaa sana nchi yetu hii tulivyo lala kiakili.
 
Ile nyaraka ilivujishwa, wajinga hawakuwa na nia ya kuitoa public, ndio maana licha ya IGA kutaka maoni ya wananchi yachukuliwe, lakini hakuna mwananchi yeyote aliyeweza kuuona ule mkataba/makubaliano mpaka ilipofika siku ya kwenda kutoa maoni yao.

Ilikuwa wanajiendea tu kutoa maoni, kama ni "makubaliano" yanayohusu maoni yenyewe, watapewa huko huko wakifika!.

Na jamaa bila aibu hili zoezi wakalitengea siku moja pekee, yani mtanganyika toka Sumbawanga, Songea, Kilimanjaro, na Lindi, wote wasafiri kama ni kwa ungo au vyovyote wawezavyo, ilimradi kesho yake saa saba mchana wawepo Dodoma kutoa maoni yao kwa kitu wasichokifahamu.

Wakati wangeweza kutumiwa hayo makubaliano wakae nayo hata wiki nzima kabla ya siku husika ili wayachambue vizuri, lakini wahuni walikuwa na nia mbaya kuanzia mwanzo mpaka mwisho.

Hili kama litapita hivi hivi, basi tusubiri kizazi kingine kije kuikomboa Tanganyika, sisi tutakuwa sawa na maiti zinazotembea.
 
Licha ya upumbavu kama huu, bado unakuta watu na akili zao timamu wakisema bila aibu kwamba serikali inayo nia njema!

Sasa ni muhimu sana, wajitokeze watu bayana kabisa, walio tayari kuongoza umma wa waTanzania kukataa upuuzi huu.
W. Slaa, Tundu Lissu na wengineo, inabidi sasa iwepo mikakati ya pamoja ya kuongoza watu watakaohakikisha jambo hili aliendelei mbele zaidi.

Tusibaki kupiga kelele tu wanazozipuuza hawa watu, inalazimu sasa pawepo na taratibu maalum za kukabili uhujumu huu wa taifa letu.
 
“Katika miaka miwili hii ya Samia, Mimi ninaefuatilia mambo ya nchi yetu, ananipa wasiwasi sanaa” Lissu akiwa Kisarawe
 
Why didn't anyone ask or debate when TICTS or Adnani secured tenders or running the port??
 
Huyu anawehuka sasa! Samia kafanya biashara gani?
 
Tukana matusi yooote lkn tambua huna unachoweza kubadili.
 
Yes, wote ni wajinga tu kwa sababu mmeishia kupiga miyowe tu mitandaoni wakati mama yupo kimya.
 
Kelele za chura tu hizo.
 
Mtahangaika sn humu. Mnajibizana na kutiana ujinga wenyewe
 
Mnajazana tu ujinga.
Hivi ni wanaume kweli nyie!?
 
Huyo ni mzushi, mwongo na mnafiki,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…