Wakati mwingine huwa najiuliza ni kipi kilichomsukuma aliyevujisha ule mkataba akafanya vile?
Kwasababu hawa jamaa wamekuwa wakituchezea kwa mikataba ya hovyo miaka mingi sana, kwanini huu wa bandari ukawa mwisho wa kufichwa?
Nikaona inawezekana mpaka aliyeamua kuvujisha, nikiamini kabisa ni mwenzao, anayewezekana akawa anakula 10% nao.
Lakini alivyoona huu wa bandari hauna ukomo, waarabu watakuja kujitawala ndani ya nchi yetu, na uwepo wao hautakuwa na faida yoyote kiuchumi kwetu, wanakuta mazingira yote wameshatengenezewa, wao ni kuchuma faida na kupeleka kwao milele!, jamaa akaona hapana, kwa hili nawasemea kwa wenye nchi yao.
Ndio akauvujisha mkataba wa hovyo kabisa kuwahi kutokea katika historia ya nchi yetu.