Tundu Lissu: Mashtaka dhidi ya Freeman Mbowe ni mepesi kuliko pamba, awaponda Waendesha Mashtaka

Tundu Lissu: Mashtaka dhidi ya Freeman Mbowe ni mepesi kuliko pamba, awaponda Waendesha Mashtaka

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu , amechambua mashitaka yaliyosomwa Mahakamani yanayomkabili Mwenyekiti wake Freeman Mbowe , huku akiyaita duni , mepesi na ya UONGO.

Amedai ana uzoefu wa kutosha kwenye kesi za uzushi na uongo kama hii kutokana na kazi yake ya Uanasheria aliyoifanya kwa miaka mingi , ameahidi kushinda kesi hiyo ya kutunga mapema asubuhi .

Hebu msikilize mwenyewe ufaidi uhondo .
 
Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu , amechambua mashitaka yaliyosomwa Mahakamani yanayomkabili Mwenyekiti wake Freeman Mbowe , huku akiyaita duni , mepesi na ya UONGO.

View attachment 1906115

Amedai ana uzoefu wa kutosha kwenye kesi za uzushi na uongo kama hii kutokana na kazi yake ya Uanasheria aliyoifanya kwa miaka mingi , ameahidi kushinda kesi hiyo ya kutunga mapema asubuhi .

Hebu msikilize mwenyewe ufaidi uhondo .
Lisu asipuuze mashtaka, apambane ashinde kesi kwanza. Hawezi jua kuna version ngapi za hiyo kesi.
 
Ogopa sana kesi hata kama ni kesi ya wizi wa kuku. Hata biblia inatutaka tupanate na washitaki wetu tusisubiri watufikishe mahakamani.
hujui kitu wewe, kwenye judiciary inayofanya kazi vizuri, hii si kesi hata kidogo. Sema kwa vile majaji wanapokea magizo anything can come out... ukiipeleka Kenya wanaifukuza nakwambia.
 
Lisu yeye kakimbia kesi bado anaona zawenzake nyepesi ,lisu ni mwoga Sana

USSR

Huwa nikisikia comments kama hizi mara moja huwa nahitimisha kwamba mtoaji comments ameshikiwa akili na ni mburula. Yaani ni mtu ambaye hana kabisa uwezo wa kutumia akili yake yeye mwenyewe kutafakari na kufanya hitimisho lake kwenye issues mbalimbali. Watu wa namna hii huendeshwa tuu kwa kufuata mkumbo wa kile wanachoelezwa kukiamini.

Why kwa sababu mtu yeyote mwenye akili timilifu, na siyo akili ya kuvumia barabara au kwenda kukojoa , na wala si chuki za kijinga za kiitikadi au upuuzi mwingine, anajua fika nini hasa kilimkuta Tundu Lissu. Pia anajua fika uwezo wa Lissu kwenye eneo lake la sheria na ni kwa jinsi gani washindani wake wanamuogopa sana wanapokuwa naye mahakamani, kiasi kwamba ilifikia mahala wakaona hatakaa wamshinde mahakamani badala yake watafute njia ya mkato ya kushughulika naye.....
 
Back
Top Bottom