Tundu Lissu: Michango ya Wananchi kwaajili ya kununua Gari langu imefika Tsh. 104,081,139

Tundu Lissu: Michango ya Wananchi kwaajili ya kununua Gari langu imefika Tsh. 104,081,139

Imekamilika ama bado? Na kama bado, bado sh ngapi?
 
Safi Sana wananchi kwa mioyo ya upendo kwa shujaa Lissu
 
1000029771.jpg
 
Tundu Antipas Lissu ni mnyenyekevu hakika .
 
Samia kachangia na hasemi ,nimtumishi wawote asione aibu kusema kachangia
 
Kwani lengo ni kufikia kiasi gani hasa?

Pia inafaa sasa kuonyesha wakati (muda maalum) ambapo lengo tarajiwa linatakiwa kufikiwa

Taarifa hizi zitasaidia kuchochea wachangiaji wengine kufikia lengo hilo haraka.

Ni vizuri pia kila mara taarifa kama hii inapo tolewa, na michango kuendelea, kuweka/kurudia taarifa michango hiyo inapotakiwa kuwasilishwa Account Number(s); kusaidia wale ambao hawakuiona taarifa hiyo mwanzo.
 
..Amina, tena Amina.

..sijui Lissu alimkosea nini Magu mpaka atume watu kumuua kwa namna ile.
Usifanye mchezo na 'megalomaniacs) wakati wowote na mahali popote.

Kwa Magufuli, ambaye alijihisi kuwa karibu zaidi na cheo cha mungu (urais); halafu aitwe "Dikteta Uchwara", tena hadharani mbele ya vyombo vya habari?

Hivi uliwahi kuona video yake pale uwanja wa Nyamagana Mwanza, akienda kununua karanga kwa akina mama pale barabarani alivyo kuwa na jeshi zima na mitutu ya bunduki imemtangulia kama eneo lile kuna vita?

'Mentality' za namna ile ni hatari sana.
 
Badili gear angani tukanunue madawati kuna shule huko watoto wanakaa chini
Subutu yake aache kunywa bia zake baridi ashughulike na madawati, kipimo cha – uzalendo - huwa kidogo sana, hasa huwa ni niya yako ya ndani katika kujali wengine wenye mahitaji muhimu
 
Subutu yake aache kunywa bia zake baridi ashughulike na madawati, kipimo cha – uzalendo - huwa kidogo sana, hasa huwa ni niya yako ya ndani katika kujali wengine wenye mahitaji muhimu
🙏
 
Hii inaleta ukakasi wa siasa safi!!
Hivi lisu alipataje ujasiri wa kuomba michango hii!!

Mbona mi naona aibu !!?
 
Back
Top Bottom