Tundu Lissu: Mkataba wa bandari ni suala nyeti sana

Tundu Lissu: Mkataba wa bandari ni suala nyeti sana

Mikataba ilibadilishwa haikubadilishwa
Ilibadikishwa according kwa previous agreement, fungua akili yako kijana. Huez kurupuka vunja mkataba na kuubadili kama mkataba husika umezuia. Ww jiulize kwann ndege zetu zimekamatwa san huko nje? Au CDM ndio wamesababisha!!
 
Zimekamatwa na miga
 
Tundu Lissu ameeleza kuwa mkataba huo unaenda kukinzana na Sheria zetu za maliasili zilizopitishwa na Magufuli zinazolazimisha migogoro yote ya rasimali zetu baina ya serikali na wawekezaji iamriwe nchini na kwa sheria zetu, lakini mkataba wa bandari unataka migogoro yote iamriwe Johannesburg Afrika kusini kwa kutumia sheria za Uingereza
 
SA Kalokola: .....Baada ya kusema hayo, hoja yangu ni kwamba IGA ni Mkataba wa kimataifa uliopitia mchakato wa 63[3]e ya KATIBA

Jaji: kwani issue ilikuaje?

SA Kalokola: issue ilikuwa whether IGA is contract

Jaji: wewe umejibu vipi?

SA Kalokola: IGA is international agreement

Wadau: Miguno kidogo.
 
Tatizo la nchi yetu ni sisi wananchi wenyewe. Tuna ujinga wa kipekee sana na ninadhani huu ni mtaji mkubwa sana wa kisiasa. Wanasiasa( Upinzani na Chama Tawala) hawa wanatuelezea masuala tofauti wakilinda mikabala na mitazamo yao mfano mwanasiasa wa Upinzani atakosoa tu au atatafuta makosa wakati yule wa Chama Tawala atasifia.
Wananchi jukumu letu ni kusikiliza "mikabala yote "na kupima kuangalia maslahi mapana ya umma. Tatizo letu na sisi tunaingia kwenye ushabiki wa kizamani kuaminishwa kabla ya kupima. Tuna uelewa mdogo sana wa mambo.
 
Makamu mwenyekiti wa Chadema Tundu Antipas Lissu amesema mkataba wa kuwakabidhi bandari baina ya Tanzania na Dubai ni swala nyeti (very seriously) ndiyo maana limepelekwa bungeni.

Akiongea club house amesema kitendo cha mkataba huo kupelekwa bungeni kinaashiria unyeti wake na athari ya mkataba husika katika sheria za nchi. Mikataba ya kimataifa yenye athari ya kubadilisha sheria lazima ipite bungeni.

Kwa mujibu wa sheria Za kimataifa kwa mfumo wa Tanzania mikataba ya kimataifa (international treaties) haiwi na nguvu dhidi ya Tanzania mpaka ipitie bungeni na kutungiwa sheria ya bunge. Hatua hii ndiyo inayoitwa domestication /ratification, yaani bunge linapitia Masharti ya mkataba wa kimataifa na kuyapitisha upya kama sheria ya bunge na baada ya hapo mkataba husika unakuwa na nguvu nchini maana unakuwa ni sheria.

Kwa kawaida mikataba ya kibiashara (bilateral commercial agreements) huwa haipiti bungeni, ukiona umepita bungeni basi mkataba husika una athari kubwa Sana kwa sheria za nchi hivyo unahitaji kupita bungeni ili kubadilisha baadhi ya sheria za nchi kuendana na mkataba husika. Hivyo kwa mujibu wa Tundu Lissu mkataba huo ukiridhiwa na bunge unakuwa sheria na unakwenda kubadilisha sheria zetu.

Tundu Lissu ameeleza kuwa mkataba huo unaenda kukinzana na Sheria zetu za maliasili zilizopitishwa na Magufuli zinazolazimisha migogoro yote ya rasimali zetu baina ya serikali na wawekezaji iamriwe nchini na kwa sheria zetu, lakini mkataba wa bandari unataka migogoro yote iamriwe Johannesburg Afrika kusini kwa kutumia sheria za Uingereza

Kuhusu vipengele vya ukomo Tundu Lissu amesema mkataba huu hauna ukomo kwani unasema utakoma pale ambapo shughuli husika zilizomo kwenye mkataba zitakoma, shughuli za kuendeleza na kusimamia bandari hazina ukomo.

---

Wamejitahidi kuleta Mechi za Simba na Yanga mara Azamu mwisho zimegoma.
 
SA Kalokola: .....Baada ya kusema hayo, hoja yangu ni kwamba IGA ni Mkataba wa kimataifa uliopitia mchakato wa 63[3]e ya KATIBA

Jaji: kwani issue ilikuaje?

SA Kalokola: issue ilikuwa whether IGA is contract

Jaji: wewe umejibu vipi?

SA Kalokola: IGA is international agreement

Wadau: Miguno kidogo.
😅😅😅
 
Back
Top Bottom