Tundu Lissu: Mkataba wa bandari ni suala nyeti sana

Tundu Lissu: Mkataba wa bandari ni suala nyeti sana

Kwani Magufuli alikuwa nani hadi asipingwe? Ni Yesu tu ndio hapingwi.
Mkuu hawa wafuasi wake umesahau walimpa ukuu mpaka kumlinganisha na KRISTO mfalme wa aman? Hukuona mwingine alisema aliezifanya mbingu na Nchi ndie anapaswa amshukur JPM? Kwa laana ile huez baki salama! Alipaswa akemee hao machawa na kumrudishia MUNGU UTUKUFU wake!!!
 
Akijibu maswali ya wananchi kuhusiana na mkataba huu. Lissu amesema kuwa huu ni mkataba mbaya zaidi tuliowahi kuingia ukilinganisha na mingine yote.

1. Anasema ubaya wa mktaba huu unaenda kubadili sheria za nchi. Akimaanisha kuwa hakuna sheria yeyote nchini ya masuala ya uendeshaji wa bandari itakayotungwa siku na miaka ijayo bila kwanza kuhakikisha haiendi kinyume na mkataba huu wa bandari kati yetu na Dubai. Anasema kwa muktadha huo , uhuru wetu wa kumaneuvre ktk ishu za bandari ndo umeshapigwa PINI na mkataba huu

2. Pili anasema mkataba wenyewe unaenda kinyume cha katiba. Anasema kwa mujibu wa katiba Bandari ni jambo la muungano. Anahoji kdma bandari ni jambo la muungano iweje DP world ihusike na bandari za Tanganyika huku za Zanzibar zikiwa huru nje ya Scope ya mkataba huu. Anauliza utakuwaje na sheria mbili tofauti kwa jambo lilelile la muungano.

3. Pia ameonya kuhusu Kampuni hiyo ya DP kuingilia siasa za Tanzania hasa uchaguzi mkuu, akijibu swali la mwananchi, amesema kuwa uzoefu wake ni makampuni haya ya uwekezaji kufanya michezo hiyo, akatolea mfano kwenye uchaguzi wa nwaka 2005, ambao licha ya CCM kuiba hela za EPA zaidi ya dola milioni 100 ili kuitumia kwenye kampeni za uchaguzi, Makampuni ya Madini yalichangia CCM zaidi ya dola milioni 30. Akaonya kuwa hata hii ksmpuni ya Dubai nayo inaweza kuendelea na mchezo huu maana ili ifanikiwe zaidi katika mkataba huu wa kuuza nchi, lazima CCM iendelee kubaki madarakani, maana serikali yake ndiyo iliyowauzia bandari kiubwete.

Unaweza kumsikiliza kiurefu hapa:


Porojo za Kisiasa baada ya mikutano yenu kubuma.
 
Kwani Kuna mkataba gani ulivyunjwa na vipi kuhusu miga
Inaonyesha hujui inner circle nn kiliendelea... Ni kwan mzee alijirud na kubadili msimamo na kukaa nao? Mwisho wa cku akaona bora tu apokee kishika uchumba ambacho kitalipwa kwa instalment ya miaka? Ile ilikua kutafuta political popularity tu lkn ngoma ilibaki vilevile kilichofanyika ni kubadili majina!! Kuvunja mikataba Mzee haihitaj nguvu bali taratibu za kisheria na c vinginevyo.
 
Evil ni Yule aliyefukiwa chato, NDULI MLA NYAMA za watu.
Chuki za kijinga tu ulitegemea vyeti feki mngeweza kuendesha nchi? Matokeo yake ndiyo haya, mkurugenzi anataka wawekezaji kuongeza ufanisi lkn anataka aendelee kubaki na ukurugenzi wake.
 
Hapa ndipo tunapomkumbuka yule mwamba kutoka Chato;hayati JPM.Sasa mwenye uthubutu kama ule wa kupambania maslahi ya maskini wengi HAYUPO.Nchi inaangamia kwa uratibu wa wakubwa.
 
Chuki za kijinga tu ulitegemea vyeti feki mngeweza kuendesha nchi? Matokeo yake ndiyo haya, mkurugenzi anataka wawekezaji kuongeza ufanisi lkn anataka aendelee kubaki na ukurugenzi wake.
Nafikiri tatizo sio vyeti feki Bali mitaala na ufundishaji Kwenye shule za sheria , wanafunzi wanavishwa mawazo ya kupambana kufauli mtihani kwa namna yoyote ile lakini sio kutekeleza kwa vitendo kwa ubora wa juu fani yenyewe
Haya mambo yalifanywa na magungo wa msovero Leo yanajirudia
 
Asikudanganye mtu, Tundu Lisu ni sehemu ya huu utawala na hakuna asichokijua ni kama Zito Kabwe tu, kwangu mimi Tundu lisu is more evil klk hawa CCM kwa maana anajificha ili kuwahadaa watu kwamba yuko against utawala wa Samia wakati siyo kweli, pure evil!
Mjinga jikite kwenye Maada, au ni kubwa sana kwako? Kama unaona ni sehemu ya huu utawala wewe chukua nafasi zao basi
 
Kwa hiyo masuala ya bandari ni ya Muungano! Lakini katika hali ya kushangaza na kustaajabisha, bandari zinazohusika na huo mkataba wa Waarabu ni zile za upande wa Bara pekee! Yaani bandari za Zanzibar hazihusiki!!

Ukiangalia Rais wa sasa, anayokea Zanzibar! Waziri anayehusika kusaini huo mkataba, naye anatokea Zanzibar! Na mbaya zaidi ni mbunge na waziri wa kuteuliwa tu! Siyo bure, kuna mtu ameturoga Watanganyika. 🤔
 
Back
Top Bottom