Akijibu maswali ya wananchi kuhusiana na mkataba huu. Lissu amesema kuwa huu ni mkataba mbaya zaidi tuliowahi kuingia ukilinganisha na mingine yote.
1. Anasema ubaya wa mktaba huu unaenda kubadili sheria za nchi. Akimaanisha kuwa hakuna sheria yeyote nchini ya masuala ya uendeshaji wa bandari itakayotungwa siku na miaka ijayo bila kwanza kuhakikisha haiendi kinyume na mkataba huu wa bandari kati yetu na Dubai. Anasema kwa muktadha huo , uhuru wetu wa kumaneuvre ktk ishu za bandari ndo umeshapigwa PINI na mkataba huu
2. Pili anasema mkataba wenyewe unaenda kinyume cha katiba. Anasema kwa mujibu wa katiba Bandari ni jambo la muungano. Anahoji kdma bandari ni jambo la muungano iweje DP world ihusike na bandari za Tanganyika huku za Zanzibar zikiwa huru nje ya Scope ya mkataba huu. Anauliza utakuwaje na sheria mbili tofauti kwa jambo lilelile la muungano.
3. Pia ameonya kuhusu Kampuni hiyo ya DP kuingilia siasa za Tanzania hasa uchaguzi mkuu, akijibu swali la mwananchi, amesema kuwa uzoefu wake ni makampuni haya ya uwekezaji kufanya michezo hiyo, akatolea mfano kwenye uchaguzi wa nwaka 2005, ambao licha ya CCM kuiba hela za EPA zaidi ya dola milioni 100 ili kuitumia kwenye kampeni za uchaguzi, Makampuni ya Madini yalichangia CCM zaidi ya dola milioni 30. Akaonya kuwa hata hii ksmpuni ya Dubai nayo inaweza kuendelea na mchezo huu maana ili ifanikiwe zaidi katika mkataba huu wa kuuza nchi, lazima CCM iendelee kubaki madarakani, maana serikali yake ndiyo iliyowauzia bandari kiubwete.
Unaweza kumsikiliza kiurefu hapa: