Naona unatafuta uungwaji mkono wa JF members ili uhalalishe chuki zako kwa Nyerere. Mpango wenu wa kumchafua kupitia yale magazeti yenu umekwama.....and now unataka kumtumia Tundu Lisu kumchafua! Kwa kifupi ni kwamba mnavyozidi kumchafua Nyerere ndivyo anavyozidi kung'aa...ni sawa na kuchoma DHAHABU kwenye moto....itang'aa mara dufu!
Tambua kuwa isingekuwa misingi imara ya umoja wa kitaifa aliyoiweka Nyerere nchi hii ingekuwa imeshasambaratika siku nyingi sana kwa sababu ya udhaifu wa vviongozi waliofuata baada yake! Hilo liko wazi kabisa!
Aidha, Nyerere aliweka misingi imara ya uchumi wa kujitegemea akitumia falsafa ya USOSHALISTI. Ni kweli kwamba approach aliyotumia ilizongwa na changamoto nyingi kiasi kwamba misingi aliyoasisi ikaonekana haifai. Hao unaotaka tuwaone wa maana kuliko Nyerere wakaja na sera ya UCHUMI HURIA kwa kutumia falsafa ya UBINAFSISHAJI wa viwanda vya UMMA.....serikali ikajitoa kutoka kwenye shughuli za biashara na badala yake sekta binafsi ikatawala!
Kama transition kutoka USOSHALISTI kwenda SOKO HURIA ingetanguliwa na SHERIA BORA YA KUSIMAMIA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA pamoja na SHERIA ZA KUSIMAMIA UBINAFSISHAJI ILI KUWEKA MASLAHI YA TAIFA MBELE huenda leo hii tungeshaanza kuitwa AFRICAN LIONS (KAMA ASIAN TIGERS) kwani ukuaji wa uchumi ungemgusa kila mwananchi wa Tanzania. Leo hii UBINAFSISHAJI unatumika kama kichochoro cha KUIBA MALI ZA UMMA. VIWANDA VYA ZAMA ZA NYERERE VILIVYOBINAFSISHWA leo vimegeuka kuwa godowns za kuhifadhia mali za kutoka ughaibuni.
Nyerere alijenga uchumi wa kumjenga mtanzania...sio yeye binafsi...pamoja na kwamba sera zake zilishindwa. Kumbuka kuwa anguko la sera za Nyerere halikumkumba yeye tu bali nchi zote za Kisoshalisti(Kikomunisti) duniani.
CHINA nayo ilikuwa ni nchi ya KIJAMAA kama TANZANIA. Leo CHINA ni nchi ya pili kwa uchumi mkubwa duniani and is about to overtake USA in the near future. Sera ya Usoshalisti ilifeli CHINA kama ilivyofeli TZ. Swali, Kwanini baada ya kuhamia uchumi huria CHINA imefanikiwa wakati huohuo TZ imeendelea kufeli.? What is wrong?
Deng Xiaoping ndiye raisi wa CHINA aliyeasisi mipango na sera za kuelekea Uchumi wa soko huria. Mipango na sera hizo ziliandaliwa kwa ustadi mkubwa na uzalendo wa hali ya juu zikiambatana na sheria za za hali ya juu zinazosimamia maadili ya viongozi na sera na mipango yenyewe. TZ kwa upande wake ilifanya transition kwa kukurupuka na uzalendo waliuweka kapuni (rejea kuzikwa kwa azimio la Arusha)
Leo hii bila soni wala haya unathubutu kumtukana NYERERE!!!!!! OMG!!!! Hata hiyo tunu moja ya umoja wa kitaifa mumeshaanza kuiharibu kwa kuendekeza UDINI, UKABILA, na UKANDA. Wanasiasa wa leo wanatafuta KURA makanisani na misikitini na ndio hawa unaotaka tuwaone wa maana kuliko Nyrerere!!!
Jambo la mwisho ambalo nataka ulifahamu DADA FAIZA ni kwamba katika SIASA huruhusiwi kutafuta sympathy ya makosa yako kwa kutumia makosa ya viongozi waliokutangalia....badala yake buni sera na mipango mbadala ya kulifanya taifa lisonge mbele kwa kuweka mbele uzalendo.
Deng Xiaoping hakujenga uhalali wake mbele ya WACHINA kwa kumponda
Mao Zedong na sera zake badala yake alipogundua sera ya USOSHALISTI isingeweza kuwavusha kwenda walikotaka kufika alibuni sera na mipango mipya na ndiyo imeifikisha CHINA hapa ilipo leo. Hata siku moja hakuwahi kumdhihaki
Mao Zedong kama wewe na genge lako mnavyofanya kwa
Nyerere.
Hiki kipindi ni cha muda lakini nilikuwa sijakisikiliza, leo nimekisikiliza na kuanzia saa moja na dakika nane ya video hii Tundu Lissu anafunguka na kusema, "kuna mengi sana mabaya aliyoyafanya Nyerere".
Msikilize Tundu akimwaga radhi kuhusu Nyerere kuanzia saa moja na dakika nane:
Swali langu; Tundu Lissu, Nyerere atakuwaje mtakatifu kama hajafanywa "Mungu Mtu"?