Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

Unaweza kusema mengine yote lakini tukubaliane tu kuwa, Mwl. Nyerere hakuwa mtu wa kawaida. Historia inabainisha hivyo na wala siyo yeye anayebainisha kwenye historia. Think bigger!.

Mkuu umenena vema sana. Pili, kwa muumini yeyote wa dini atakubaliana na mimi kuwa hakuna 'roll modal' wa dini yeyote anayekubalika bila kuhojiwa na upande usiomkubali. Mathalani, wanaomwamini Yesu Kristo kuwa ni Mungu na Mwokozi inapingwa vikali na 'makafiri' (asiyeamini) na pia wanaoamini kuwa mtume Mohamad SAW ni 'roll moda'l wao pia wanapingwa vikali na 'makafiri' na hata ukiwazungumzia wale wanaoamini kuwa 'ngombe' ndio 'roll modal' wao pia hawaeleweki na baadhi ya makundi. Kwa kusema hivyo maana yangu ni kuwa Nyerere yeye ana nini cha zaidi hadi akubaliwe na watu wote kitu ambacho hao the 'great' modals walikuwa nacho zaidi yake? This means simshangai Tundu Lissu kwa hoja zake. Nionavyo mimi, tuko hapa tulipo (kwenye tope) kwa sababu kuu mbili ambazo ni kukosekana kwa uadilifu na uwajibikaji! Kwa kukosekana kwa mambo hayo kumepelekea watu kwa nafasi mbalimbali kufanya wapendavyo huku wengine tukibaki kuangalia tukiwa hatuna cha kuwafanya au la kufanya! Kwenye hii katiba tarajiwa kama haya hayatawekewa tofauti (yaume na kuadabisha) hata zije serikali saba, hakutakuwa na jipya bali ni wigo mpya wa ulaji kwa wale ambao hawakuwa na nafasi kabla! Ushauri wangu kwa kina Tundu Lissu na wabunge wote wa bunge maalum la katiba, sisitizeni viwepo vipengele vigumu sana vya kusimamia uadilifu na uwajibikaji! Else ni kuongezeana ulaji tu kama zamani (business as usual)!
 
Msome Mkristo mwenzio Mwandishi Jan P van Bergen anasemaje kuhusu Nyerere:

Mwandishi Jan P van Bergen katika kitabu chake Development and religion in Tanzania, amefichua taarifa za kikao cha siri Ikulu ya Dar es Salaam mnamo Agosti 3, 1970 kati ya Rais Julius Nyerere, Padri Robert Rweyemamu na muwakilishi wa Papa, Giovanni Cerrano. Kwa mujibu wa van Bergen, katika kikao hicho Nyerere aliwaeleza viongozi wake wa dini kuwa ameunda idara ya elimu ya siasa katika TANU na amemuweka Padri aiongoze kwa sababu ya imani yake madhubuti. Aliwaeleza pia kuwa katika Kamati kuu ya chama ameweka Mapadri lengo likiwa kulipa Kanisa fursa na uwezo mkubwa hapa Tanzania.

Jee, na yeye ni mdini?

mwandishi wa huo upuuzi nani?
 
Nyerere kazowea vya kunyonga. Kwanini kamfungia Aboud Jumbe, Mjimwema?
 
Mimi huwa nadhani wanasheria ni watu wazuri sana katika uwanja wa siasa hasa ukiangalia kwa kutumia darubini katika siasa za nchi za magharibi utakuta kuwa, viongozi wengi wa nchi hizo ni wanasheria na wamefanikiwa/wanafanikiwa katika siasa zao.

Kama hoja yako ni kweli, kwa nini inakuwa tofauti kwa Mh. Tundu Lissu?.

Nyerere alitufundisha woga. Ona jmaa huyo uliyemjibu alivyo mwoga! Definitely atakuwa CCM
 
Godmanhustler, Verry true, Huyu Lisu anatumiwa na watu wenye maelekezo toka nje ya nchi kuisambaratisha TZ, hafai kabisa! Halafu lilivyokua jinga linadhani ni sifa kuuponda na kuusambaratisha muungano, ile dhambi ya ubaguzi itaendelea kuwatafuna cdm.

Alichosema LISU ni UONGO? tuanzie hapo kwanza,,,!!
 
Last edited by a moderator:
Nyerere: niliwashawishi wakenya na waganda tuingie kwenye federation (shirikisho?) la Afrika Mashariki kwamba ndani ya federation kutapunguza ukabila ndani ya nchi zao.
 
Ilikwisha semwa na watukuka. "HUWEZI KUWADANGANYA WATU WOTE SIKU ZOTE" watatokea wenye akili isiyokubali kudanganywa watasema au kuuanika "UONGO HUO." Akina Wasira na Mwigulu nao waje na references zavkukanusha hoja ya Lisu.
 
Mimi huwa nadhani wanasheria ni watu wazuri sana katika uwanja wa siasa hasa ukiangalia kwa kutumia darubini katika siasa za nchi za magharibi utakuta kuwa, viongozi wengi wa nchi hizo ni wanasheria na wamefanikiwa/wanafanikiwa katika siasa zao.

Kama hoja yako ni kweli, kwa nini inakuwa tofauti kwa Mh. Tundu Lissu?.

Inakuwa tofauti kwako kwa sababu anayoyaongea Tundu Lisu ni mwiba kwa wale mliozoea kuishi maisha ya kinafiki nafiki.
 
Msome Mkristo mwenzio Mwandishi Jan P van Bergen anasemaje kuhusu Nyerere:

Mwandishi Jan P van Bergen katika kitabu chake Development and religion in Tanzania, amefichua taarifa za kikao cha siri Ikulu ya Dar es Salaam mnamo Agosti 3, 1970 kati ya Rais Julius Nyerere, Padri Robert Rweyemamu na muwakilishi wa Papa, Giovanni Cerrano. Kwa mujibu wa van Bergen, katika kikao hicho Nyerere aliwaeleza viongozi wake wa dini kuwa ameunda idara ya elimu ya siasa katika TANU na amemuweka Padri aiongoze kwa sababu ya imani yake madhubuti. Aliwaeleza pia kuwa katika Kamati kuu ya chama ameweka Mapadri lengo likiwa kulipa Kanisa fursa na uwezo mkubwa hapa Tanzania.

Jee, na yeye ni mdini?
Naona unatoa darsa murua.
 
mama foxy we we si Nazi wa magamba??
imekuaje Leo unamtusi muasisi wa chama Chetu????

Sikuanza leo kusema ukweli, tatizo tukisema ukweli mnasema matusi, nyie ndio wale mliozowea "kuishi kwa uongo hawawezi kusema kweli".
 
siku zote Tundu Lisu ni mlopokaji na asieweza kudhibiti hisia zake anaposhangiliwa anaondoa kabisa hadhi ya upinzani nchini. Na hili ndio tatiizo la upinzani, hawa jamaa hawana uzalendo, heshma wala miiko.

Alichosema LISU ni Uongo? tuanzie hapo kwanza,,,!
 
Sijui niikuite dada, mama au bibi yangu anyway wote tunakubali kuwa Nyerere anamakosa na mapungufu yake kama mwanadamu. Lakini kwa hii shutuma ya lissu kwenye bmk, wewe na lissu wako mmekosa hekima. Kwa nini nasema hivyo?

Nyerere alitoa angalizo kuwa hatawalazimisha waznz muungano kama wataudai uvunjike wao wenyewe sio kutumiwa na watu kutoka nje. Hapo ndipo hekima na hoja ya Nyerere ilipo jikita.

Sasa wewe na lissu wako mlisha jiuliza na kujiridhisha kuwa je, Jumbe na wenzake wengi hawakuwa wanatumiwa na watu kutoka nje?

Tangu Nyerere auachie urais wameshakuja marais watatu wa jmt na wawili kati ya hao wa dini yetu. Je wamemfanyia nini jumbe pale mji mwema au nao ni waongo kama Nyerere. Acheni hizo bwana lissu kwa hili kakosa hekima.

Jumbe alikuwa si Mzanzibari?

Wolfgang Dourado alikuwa si Mzanzibari?

Tundu Lissu anasema wote hao walipohoji kuhusu muungano Nyerere aliwaweka kizuizini.

Njoo na lingine.
 
Na wewe muongo, mzandiki mfitini na mnafiki mkubwa, Sitta aliomba kuonana na viongozi wa dini Pengo na Mufti Simba

Hujamsikia Pengo anasema anataka Serikali mbili? sasa jiulize hayo ni maoni ya nani wakati yeye Mkuu wa Kanisa Katoliki hapa kwetu. Ukishapata jibu, jiulize, Nyerere alikuwa kanisa lipi? na serikali mbili ni nani aliziasisi na kuiuwa Tanganyika?

Ukipata majibu usijiaibishe, kaa nayo moyoni tu.
 
Unaweza kusema mengine yote lakini tukubaliane tu kuwa, Mwl. Nyerere hakuwa mtu wa kawaida. Historia inabainisha hivyo na wala siyo yeye anayebainisha kwenye historia. Think bigger!.
Kweli mkuu kwani pale Mwitongo alikuwa anachenza na nyoka.........ajabu sanaaa........
 
Afadhali ya Nyerere ambaye alikiri kuwa wao hawakuwa malaika kwani miaka 24 ya uongozi kuna mambo ya kijinga waliyafanya, alienda mbali zaidi kwa kuasa mbona mnaacha yale mazuri na kufuata yale ya kijinga?...Mimi natamani kumuona alisaini ile hati ya Muungano maana inaonekana ni bonge la mtaalam! Je? Hawezi kushtakiwa kwa mujibu wa sharia? Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni! Baada ya JKN sijaona Msomi Mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa kama Tundu Antipasi Maghway Lisu!... Huyu Jamaa ni mwiba Mkali sana kwa walioko Madarakani! Sielewi Kinana et al na uwezo wao wote wanawang'ang'ania watu kama akina Nape, Nchemba na Juliana wanaacha kumshawishi Mtu mwenye mvuto Mkubwa kisiasa pengine kuliko wote Africa kwa sasa... I think Ikulu Should do something for Lisu! anatakiwa arudishwe kundini kwa gharama yoyote ile... I wonder strategist wa CCM wamelala wapi wanashindwa kuona mlinganyo mdogo kama huu ...
 
Back
Top Bottom