Unaweza kusema mengine yote lakini tukubaliane tu kuwa, Mwl. Nyerere hakuwa mtu wa kawaida. Historia inabainisha hivyo na wala siyo yeye anayebainisha kwenye historia. Think bigger!.
Mkuu umenena vema sana. Pili, kwa muumini yeyote wa dini atakubaliana na mimi kuwa hakuna 'roll modal' wa dini yeyote anayekubalika bila kuhojiwa na upande usiomkubali. Mathalani, wanaomwamini Yesu Kristo kuwa ni Mungu na Mwokozi inapingwa vikali na 'makafiri' (asiyeamini) na pia wanaoamini kuwa mtume Mohamad SAW ni 'roll moda'l wao pia wanapingwa vikali na 'makafiri' na hata ukiwazungumzia wale wanaoamini kuwa 'ngombe' ndio 'roll modal' wao pia hawaeleweki na baadhi ya makundi. Kwa kusema hivyo maana yangu ni kuwa Nyerere yeye ana nini cha zaidi hadi akubaliwe na watu wote kitu ambacho hao the 'great' modals walikuwa nacho zaidi yake? This means simshangai Tundu Lissu kwa hoja zake. Nionavyo mimi, tuko hapa tulipo (kwenye tope) kwa sababu kuu mbili ambazo ni kukosekana kwa uadilifu na uwajibikaji! Kwa kukosekana kwa mambo hayo kumepelekea watu kwa nafasi mbalimbali kufanya wapendavyo huku wengine tukibaki kuangalia tukiwa hatuna cha kuwafanya au la kufanya! Kwenye hii katiba tarajiwa kama haya hayatawekewa tofauti (yaume na kuadabisha) hata zije serikali saba, hakutakuwa na jipya bali ni wigo mpya wa ulaji kwa wale ambao hawakuwa na nafasi kabla! Ushauri wangu kwa kina Tundu Lissu na wabunge wote wa bunge maalum la katiba, sisitizeni viwepo vipengele vigumu sana vya kusimamia uadilifu na uwajibikaji! Else ni kuongezeana ulaji tu kama zamani (business as usual)!