Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Narudi kama Mwananchi huru tarehe 27 Julai 2020, Serikali inipe Ulinzi. Kesi zangu 6 zina dhamana, sitakamatwa

Serekali ipi itoe ulinzi ua ni ile uliokuwa huna imani na polisi wake
 

Hata udhikiri uchi hapo uwanja wa Taifa, ila ukweli unabaki kuwa jiwe ndio muhusika.
 
Hivi unaweza kuomba adui akupe Ulinzi?
 
Alisema hana imani na vyombo vyetu vya usalama. Iweje awaombe ?

Hawaombi bali anawataka maana ni jukumu lao kisheria, maana wanalipwa mshahara kwa kazi hiyo. Sisi wengi acha huyo Lisu, hatuna imani na jeshi la polisi, lakini kutokuwa na imani nao hakuondoi wajibu wao kisheria.
 
Lissu ndiyo rais wako baada ya October
 
Hivi unaweza kuomba adui akupe Ulinzi?

Neno kuomba unalitoa wapi, hawaombi bali anawakumbusha wajibu wao wa kisheria. Huenda unadhani kulindwa na jeshi ni hisani, ndio maana unachomeka maneno ya kipuuzi sijui kumuomba adui yako ulinzi. Tundu Lissu hahitaji urafiki wowote wa kujipendekeza kwa polisi, bali anahitaji polisi watekeleze wajibu wao kisheria fullstop.
 
Mawazo ya kipuuzi hayo kama ya TL
 

Acha segerea, mkiona hata hapo segerea hapatoshi mpelekeni Guantanamo, ila tunajua fika kuwa jiwe hataki kuingia kwenye uchaguzi wa 2020 na Lissu. Hivyo itabidi atumie hila zote, na vyombo vyote vya dola kuhakikisha hapambani na mwanaume wa kweli kwenye uchaguzi. Hivyo vitisho vya Segerea havikuanza juzi, ni toka awamu hii iingie madarakani. Kama mlitaka kumuua ikashindikana, ndio mtashindwa kumuweka segerea?
 
Karibu nyumbani kamanda mungu yupo pamoja na ww atakulinda
 
Haachi kulialia!
 
Ataongea na Watanzania kwa kulihutubia Taifa akiwa kama nani? Anataka ulinzi wa vipi na yeye kama nani? Kwani mbona kila Mtanzania analindwa, yeye anataka ulinzi upi na kwa lipi alilonalo?
 
Mungu akubariki mh Lissu walitaka kukuua Mungu akakataa wanasita hata kujibu barua ya ombi la ulinzi wako ambalo ni haki yako kikatiba anyway huu utawala sio wa kawaida shetani Ana makazi yake kwenye nafsi zao usijali wakati si milele viongozi wetu wa dini wapo kimya wanasubiri sadaka zetu jumapili na inawezekana hata tukio la kuwasili kwako likafifishwa na tukio la kupangwa litakalo divert attention usihofu uwe na moyo mkuu Mungu wetu ni mwenye haki.

Karibu Sana nyumbani mtetezi wa kweli wa wanyonge wa Tanzania.
 
Sura
Ataongea na Watanzania kwa kulihutubia Taifa akiwa kama nani? Anataka ulinzi wa vipi na yeye kama nani? Kwani mbona kila Mtanzania analindwa, yeye anataka ulinzi upi na kwa lipi alilonalo?
Roho halisi ya shetani ndio hii Yani huyu ndio shetani mwenyewe kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…