Naona kuropoka ropoka ndo kwingi hapa, kwani sifa za mtu kuwa rais kwa nchi kama hii ni zipi, labda tuanzie hapo.
Make kwa uzoefu wangu, sioni kama wapigakura wa nchi hii wana vigezo vyovyote wanavyotumia ktk kumchagua rais ila naona wengi wanafuata mkumbo tu.
Tukiangalia waliotutawala hadi leo, sioni mwenye "Unic Qualities" kando ya Nyerere, ambazo naweza kusema watu walivitumia kama vigezo vya kumchagua, sioni, to be candid.!
Tumeona majuzi kwenye uchaguzi nchini France ambapo mgombea wa chama kisichofahamika Bw. Emmanuel Macron, alishinda urais, bcoz pasipo kujali uchanga wa chama chake lkn bado wapigakura waliweza kumpatia kura nyingi, aidha kwa sababu ya qualities zake au bcoz of what he stood for.
Kwa bahati mbaya hapa kwetu hilo halipo, mtu atachaguliwa tu kisa anatoka labda ccm, hata kama hana ile hulka ya uongozi! Kwa mantiki hiyo, nina-sum up kwa kusema kwamba, kwa Tanzania mtu yeyote anaweza kugombea urais na akapata kwani hakuna cha kuzingatia vigezo. Hata huyo Tundu Lisu, anaweza tena vizuri tu, (Since he is not worse and neither the incumbent nor his predecessors are any better).