Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

Ha ha ha ha.. Lissu ni mzuri sana, ana akili sana, ni mpambanaji sana, na anaijua sheria sana.. Kwa kifupi yuko vizuri sana..
Ila kwa uraisi kwa maoni yangu hapana..
Mkuu Kama magufuli kwa vile alivyo ameweza kuwa rais... lissu anashindwa nini
Duh! Ama kweli akutukanaye hakuchagulii tusi!

Eti Tundu Lissu ni zaidi ya Rais Magufuli! Kwa wanaojua maana tumeelewa una maanisha ni zaidi kwenye 'kuropoka ropoka'.

Kama wanazo pesa za kumrudishia Lowassa then Mtu yoyote anaweza kuwa mgombea kwa tiketi ya CHADEMA achilia mbali Tundu Lissu.

Kwa trends zinavyokwenda kuna uwezekano mkubwa hata wabunge wa kambi ya upinzani watapungua baada ya uchaguzi 2020.

Taja ni kipi Ambacho magufuli anamzidi lissu.. labda anamzidi kwa Sababu ameshiriki ufisadi Wa kuuza nyumba za serikali na kivuko kibovu.. ilihali lisu hajawahi kuiba hata sindano
 
Hivi kwanini mnajitoa akili? Hizo nyumba za selikali aliuza chini ya boss wake Sumaye, na mnae huko chadema, mfukuzeni huko ili tujue kweli hicho chama chenu hakilei mafisadi.

......

Sumaye si aliyetoa idhini aliyetoa idhini ni boss wake na Sumaye,bada angeonyesha Uzalendo kwa kutojigawia lakini issue alijigawia nyumba yeye,nduguze na mahawara period.Usimtetee,ni mwizi tu kama wenzake hana tofauti
 
Paskali, si vema kumlinganisha mtu ambaye ana matatizo ya akili na Dkt Magufuli. Lisu ana matatizo yake binafsi kiakili. ACCACIA wamemkomalia anatafuta kiki pahala pa kutokea
 
Upinzani miaka yote huwa unashindwa kuandaa mtu wa kuwania nafasi ya urais.

Labda Mbowe ndio anaonekana anaweza kupambana kwenye hiyo nafasi kinyume na hapo wakampigie magoti Dr.Slaa.
 
Haina Ubishi Lissu The Great. Ni Mtu Wa Kipekee Mno Kwa Nchi Hii. Ni Wasomi Pamoja Na Vijana Ndio Huwa Wanamuelewa. Plato Aliwahi Sema " If You Hate Politics You Will Be Ruled By Mediocre" Nashukuru Tumempata Lissu.
 
Oh Yeah, This is marvelous! Naomba nisikuwekee maneno hapo ulipoacha kusema Lissu kamzidi nini Magufuli, na iwe hivyo ulivyowaza tunabaki tunajaribu ku-connect mawazo yako na yetu wasomaji wako, mawazo yaki-match huurah...!
 
Pascal Mayalla,

Tundu LISU kumpima uwezo wake mpime kwanza kama mbunge. Je jimboni kwake kafanya nini la maana Tangible linaloonekana? Nawasifu wachaga wana msemo kuwa mtu akikuambia ana akili akuonyeshe vitu vinavyoonekana kama vile biashara aliyonayo, nyumba ya kuishi aliyonayo na pesa alizonazo na mali mbali mbali vinginevyo ni mjinga tu sababu akili kwa mchaga haipimwi kwa uwezo wa kubwabwaja maneno kama Lisu afanyavyo.

Ni baadhi tu ya makabila mengine yanayoamini kuwa mtu kuwa na akili ni uwezo wa kubwabwaja maneno ndio waunga mkono Lisu. Mimi binafsi Tundu LISU haja-ni -convince kuwa ni legal or political material. Ni bahati mbaya kuwa hata proffesion kama za wasomi wanasheria ambao fani yao si ya makelele wameingiza na kuruhusu makelele kwenye ofisi za TLS.Hii TLS ya sasa ni too noisy.Serikali iunde tu bodi ya wanasheria this noisy TLS should go to hell. Yaani mtu hata ukiwa ofisi za TLS huwezi tulia kimya u kaconcenrate kuandika defence case ya mteja wako kisa mikelele ya LISU ofisini isiyoisha.
 
LISU NI MHAINI AWEKWE KIZUIZINI

Na Thadei Ole Mushi.

Mwalimu wangu alishawahi kunifundisha kwenye history kuwa siku zote unapopanga kufanya MAPINDUZI hakikisha unakubaliana na matokeo haya mawili

1.Ukifanikiwa katika mapinduzi yako watakuita SHUJAA ,MWANAMAPINDUZI, NA KILA JINA LA KISHUJAA.

[HASHTAG]#ILA[/HASHTAG]

2. Ukishindwa kwenye mapinduzi hayo watakuita jina moja tu "MHAINI".

Kinachomtokea TUNDU kwa sasa ni hili jibu la pili huyu anatakiwa awekwe KIZUIZINI kama watanzania wengine waliokwisha kujaribu kusaliti nchi yao na kuwekwa kizuizini.

[HASHTAG]#Anachotakiwa[/HASHTAG] kukithibitisha Lisu ni Udikteta wa Raisi magufuli. Kama kuteua msukuma kuwa kiongozi mahali ndio Udikteta basi atuthibitishie.

[HASHTAG]#Najua[/HASHTAG] wote wanaochaguliwa au Kuteuliwa na Mh Raisi wanapendekezwa na mamlaka za Uteuzi baada ya kufanyiwa vetting. Je Lisu yupo kwenye mamlaka za uteuzi ili aseme mapendekezo ya mamlaka hizo yamepuuzwa na Raisi?

#Je Mh Raisi ndio anayetoa vibali vya wakatoliki kufanya kazi nchini na si Uhamiaji? Kama ni uhamiaji je wakatoliki hawaruhusiwi kufanya kazi hapa nchini? Je hao wamisionari wa kilutheri walioambiwa wakapange foleni kule Uhamiaji walitaka nani awape kibali cha kufanya kazi nchini? Je uhamiaji waliwanyima kibali kwa kuwa ni walutheri?

[HASHTAG]#Nimemsikiliza[/HASHTAG] Fatma Karume wakili wa Lisu akitoa tafsiri ya kosa la Uchochezi kuwa ni kumchochea mtu kufanya uhalifu na yeye haoni kama lisu alimchochea mtu.

[HASHTAG]#Huyu[/HASHTAG] naye akili hazipo sawa haoni aliyechochewa kabisa ila anasahau kuwa Lisu anawaaminisha watanzania kuwa Raisi Magufuli anapendelea kabila lake pamoja na Dini yake. Haoni kuwa anawachochea makabila mengine na dini nyingine?

[HASHTAG]#Mataifa[/HASHTAG] mengi yanaingia matatizoni kwa kauli za kichochezi kama hizi. Je wasukuma na wakatoliki wanaofanya kazi maeneo mengine wabaguliwe? Lisu anataka haya makabila na dini nyingine zifanye nini? Nyumbu hawaoni uchochezi huu wanasahau vita haina macho...

[HASHTAG]#Nitashangaa[/HASHTAG] kama upande wa Jamhuri watamuachia huru kwa kauli hizi. Kama mkimuachia basi mtakuwa kawashinda kuwa kweli analiyoyasema yanafanywa kweli na Raisi.

Ole mushi
 
Back
Top Bottom