Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

Kura zikihesabiwa kwa haki Amini nakwambia tundu lissu anao uwezo wa kupata kula zaidi ya milioni 6 lakini kwa kua mwaka huu kuna kila dalili kua watu hawataenda kupiga kura na wataojitokeza hawatazidi milioni kumi basi ikiwa kura zitahesabiwa kwa haki LISSU anaweza kupata zaidi ya million kumi kwa sababu wapo wanaccm wanahasira sana Mfano Njombe kuna watu wanahasira baada ya ndugu yao kuwekwa mahabusu zaidi za mwaka mmoja japo hawasemi hadharani kwa kuogopa,pili kuna watu wanahasira za maisha ya miaka mitano.Sababu nyingine zitakua ni hasira za wapambe wa CCM ambao watakua hawajakubaliana na teuzi za wagombea kama ilivyotoea Njombe mjini 2015 wako wanaccm wa kweli kabisa walipigia kura upinzani baada ya diwani wao kuenguliwa na kutopitishwa jamaa mmoja hivi aliyekua chaguo la makinda.
 
Mkuu Paskali, hata Tundu mwenyewe anajua kuwa ni mzuri sana kwenye nafasi ya kuongea hovyo na kukosoa lakini si utekelezaji. TLS sasa imeshamshinda,hakuna linalofanyika kwa manufaa ya wanasheria.
Usisahau TLS alikiaa miezi sio ziadi ya sita lakini Jengo jipya la wanasheria ndiye aliyelianzisha baada ya kwa kukwama kwa zaidi ya miaka ishirini,pia amewasaidia wanasheria waliokua wakiibiwa fedha kupitia chama cha wanasheria wa Afrika mashariki ili hali wao hawfanyi kazi huko na sasa mchango huo umekua wa hiari
 
Pascal kwa hili mie nakuunga mkono, ila CHADEMA inabidi wa swallow pride yao wakubali kujadiliana na ACT maana nikimuangalia kiongozi wa ACT Zitto yeye ashasema hana shida Lissu kusimama ila issue naona itakuwa jinsi ya kuachiana majimbo na wahafidhina wa CHADEMA wanaokataa kuona ukweli kuwa Zitto alisha move on and he is a force to reckon na njia bora nikuenda na Zitto na chama chake maana bila hawa wawili ukiongeza na usajili wa majeruhi wa mdau mpya NCCR hata kama kuna tume huru bado CCM atatoka kidedea.

Kwa muono wangu ACT waachiwe wa consoilidate nguvu ya ZNZ, Pwani yote, kanda ya magharib CHADEMA wasalie na kanda ya kaskazini na kusini hapa tutakuwa na mtifuano si wakitoto.

Pia kama Membe anaweza jump ship apewe kugombea maana hii ita wavuruga sana CCM kwani kwao pia kuna mpasuko wachini chini na bahati nzuri kwasasa tofauti na 2015 sasa hivi kuanzia serikalini watu wengi tu wanatamani CCM ipotee kwasababu ya jamaa.
 
Tatizo la Mhe. Tundu A. Lissu ni moja tu akitia miguu katika ardhi ya Tanzania anakamatwa kwa amri ya Mahakama na Kosa lenyewe ni la kukiuka masharti ya Dhamana. Ikumbukwe kwamba Waliomdhamini waliiandikia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujivua udhamini wao baada ya jitihada za kumshawishi Lissu kurudi nchini.

Walienda mbali zaidi na waliiandikia Mwenyekiti wake Mhe. Aikael F. Mbowe kumshawishi arudi najitihada hazikuzaa matunda.

Ikiwa ni mwezi wa 6 leo kasoro masaa machache tu. Atatiwa ndani hadi Mwezi wa 9 baada ya mawakili kupambana sana na kutakua na takribani miezi miwili tu kabla ya uchaguzi.
 
Kipenga cha urais kimepulizwa Chadema, kumekucha!
Screen-Shot-2019-01-17-at-10.42.26-AM-620x308.png

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema
Tundu Lisu: Nitagombea urais
TUNDU Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maaendeleo (Chadema)-Bara, amesema atagombea urais kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Amesema, ataandika barua ya kuomba ridhaa ya chama chake kugombea kiti cha urais kwenye uchaguzi huo na kwamba, wakiona inafaa na kumpitisha, yupo tayari kupeperusha bendera ya chama hicho
Akizungumza na Mwanahalisi Online leo Jumatano tarehe 3 Juni 2020, lililotaka kujua kama anao mpango wa kugombea urais ndani ya chama chake.

“Nilikuwa nasubiri baraza za chama, nitaandika barua ya kuomba ridhaa ya chama changu nigombee urais,” amesema Lissu
Mapema leo Jumatano, Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika ametangaza kufunguliwa kwa milango kwa wanachama wa chama hicho, wanaotaka kuwania urais kuandika barua kwa katibu mkuu.

Mnyika amesema, milango hiyo imefunguliwa kuanzia leo hadi tarehe 15 Juni 2020 kisha baada ya hapo, watakaokuwa wamejitokeza watapelekwa kamati kuu ya chama hicho kwa hatua zaidi za ndani.

Baada ya tangazo hilo la Mnyika, MwanaHALISI ONLINE limezungumza na Lissu kwa simu akiwa nchini Ubelgiji ambaye amesema, “kama mwanachama mtiifu wa Chadema, nilikuwa nasubiri uongozi wa chama unaohusika, utoe baraka zake kwa wanachama kuanza mchakato wa uchaguzi.”

Mbunge huyo wa zamani wa Singida Mashariki amesema, “kwa vile hizo baraka zimekwisha kutolewa na kwa vile nimekuwa natajwa tajwa na najitaja taja, basi nitafanya kitu ambacho nimekuwa nakisemasema.”

Lissu ambaye amewahi kuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) amesema, “nitamwandikia barua rasmi katibu mkuu wa chama ili kutoa tangazo rasmi kwake.”

“Na vilevile, nitazungumza na umma wa Watanzania na wengine wanaotutakia mema baada ya kuwa nimetangaza nia rasmi na kwa uchache, maswala muhimu ninayoyaona katika uchaguzi huu kwenda mbele,” amesema.

Katika kusisitiza hilo, Lissu amesema, “Nafikiri nitafanya hivyo ndani ya muda huu ambao umetolewa na chama wa kufanya hivyo na kwa vyovyote vile sitawachelewesha.”

Akijibu swali aliloulizwa na MwanaHALISI ONLINE anarejea lini nchini, Lissu amesema, “suala la kurejea nchi linashughurikiwa na wakati mwafaka utakapofika wananchi watapata taarifa.”

Amesema, sheria za Tanzania hazijazungumzia mtu akiwa nje ya nchi hiyo kwa kipindi fulani hatoweza kugombea hivyo hana wasiwasi na hilo.

“Kama nitakuwa mgombea urais kwa niaba ya chama lazima nitakuja Tanzania,” amesema
Lissu amekuwa nje ya Tanzania tangu tarehe 7 Septemba 2017, aliposafirishwa kwenda Hospitali ya Nairobi, Kenya kwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 nje ya makazi yake Area D jijini Dodoma.

Mwanasiasa huyo alifikwa na mkasa huo, akitoka kuhudhuria vikao vya Bunge lililokuwa likiendelea jijini humo.

Alipata matibabu Nairobi hadi tarehe 6 Januari 2018 alipohamishiwa Ubelgiji aliko mpaka sasa kwa matibabu zaidi.

Hata hivyo, Lissu amekwisha kusema, amepona na anachosubiri ni kuhakikishiwa mazingira salama ya maisha yake ili yasije kujitokeza kama yaliyomkuta awali.

Source: Mwanahalisi online.
P.ĺ
 
tundu lissu ana uwezo upi? wa kupayuka kama mgonjwa wa malaria? au unaongelea uwezo upi pot?
Mkuu Poti Maige S Chagu, mtu kabla hujachangia uzi wowote si unapaswa kuusoma kwanza?. Ukiisha soma ukikutana na maelekezo, fuata maelekezo!.
Wanabodi,

NB. Sijasema Lissu ni zaidi ya Magufuli kwenye nini, na nawaomba sana msiniulize!.

Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali
P
 
Heshima kwenu wanajamvi.

Ningekuwa na mamlaka ndani ya CHADEMA Mh Lissu angepitishwa mapema asubuhi bila kupoteza muda.Nafikiri ni muda muafaka haswa ndani ya CHADEMA kuacha kupoteza muda Mh Lissu anauzika kirahis zaidi ukilinganisha na wagombea wengine hasa katika majira haya yanayo hitaji mtu wa kushindana na Mh Magufuli ambaye katika kipindi cha miaka mitano amehakikisha upinzani haupati nafasi ya kusikika huku yeye binafsi akitumia vyombo vya habari sana.
Mkuu Ngongo, kwanza naunga mkono hoja ya presidential candidature ya Tundu Lissu kwasababu ni presidential material, hata mimi nilishauri
Elections 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha Uwezo Zaidi ya Magufuli!

Ila baada ya kuanza kufunguka funguka huko Ughaibuni, niliingia mashaka kama atarejea home
Kwa mliomsikia Tundu Lissu kwenye Hard Talk, unadhani atarejea nchini? Mimi sina hakika na akirejea, atakuwa ni shujaa kuliko hata Nelson Mandela!

Tundu Lissu akatoa conditions to be met kabla ya kurejea, na mimi nikashauri
Kamanda Lissu, Usisubiri Jibu la IGP Kuhusu Usalama Wako, Aliyekulinda na Shambulio Lile Yupo, Yeye Aweza, na Ataendelea Kukulinda, Welcome Back Home!

Na alipoamua kugombea kutokea Ughaibuni nika comment
Elections 2020 - Je, kuna uwezekano kutangaza nia kugombea Urais kupitia CHADEMA kwa baadhi, kunatumika kama kichaka cha kujifichia aibu ya kushindwa ubunge?.

Na mwisho nikawatajia mgombea urais wa Chadema, sio Lissu!.

Elections 2020 - Jicho la Tatu: Mgombea Urais CHADEMA ni Freeman Mbowe! Tundu Lissu Pacemaker! Nyalandu ni Serious Contender, Msigwa anatania, Dkt. Mayrose Majinge...

P
 
Pascal Mayalla "Kwa maoni yangu, kwenye kambi nzima ya upinzani Tanzania, tuna watu wawili tu ndio wenye uwezo, wa ability na capabilities za kumkabili JPM na aka feel the heat ya uchaguzi. Hawa ni Zitto Zuberi Kabwe na Tundu Lissu." Mwisho wa kunukuu.

Ni juu yao kufanyia kazi, maana ndio ukweli wenyewe.
 
Back
Top Bottom