Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

Hivyo kwa vile Watanzania huwa hawachagui sera wala hawachagui vyama bali huchagua watu
umenifurahisha kwenye hio sentensi na hapa ndipo utahira wa watanzania unapoonekana-ulichokisema ni kweli kabisa kama watanzania wangekuwa wanachagua sera basi hamna mwenye akili anaweza kuchagua seraza CCM ambazo zimeshindwa kuzaa matunda kwa miaka 50
 
Paskali, sio kwamba umewaza sahihi bali ulichokiandika ndicho kitakachotokea, miaka yote CHADEMA wako hivyo na hawana utamaduni wa mtu kugombea urais mara mbili! Lakini je? Lissu hanunuliki? Hivi wakamwambia kabisa wewe umeshinda lakini nchi hatukupi, ukileta fujo tunakudunga sindano ya kutuliza mzuka, unadhani atafanyaje zaidi ya kusema mi sitaki damu za watanzania zimwagike.....!!! Anatakiwa aje mpinzani wa kweli mwenye ukichaa anayetokea jikoni walipo wapishi....!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nawakumbuka wale wa ulipo tupo, naona kila dalili za mzee kukatwa tena!
Unamaanisha Mamvi watamkata mara ya pili? Ukomo wa uvumilivu utamfikia mwisho. Siyo jambo dogo hilo! Mtu amehama na wafuasi kibao toka CCM, amewalipa hela kibao na amekuza jina la chadema na kuiongezea ruzuku kibao kufuatia uwepo wake. Halafu 2020 wamkate kwa mara nyingine, mbona patachimbika.....!
 
Subiri uone CDM 2020 watamsimamisha nani utashangaa, wale jamaa kuna muda unaona wana akili alafu kuna muda unajiuliza zimeenda wapi, walifanya hivyo kwa Lowassa, subiri 2020 uone watakavyotuabisha, wanaweza mrudisha Lowasa tena, Lissu anaweza kuleta serious competition ila ajiangalie sana kuna baadhi ya kauli anatoa sasa hivi wabongo walivyo utaanza kusikia lissu ni kibaraka wa wazungu, na wote tunajua wabongo wanavyochukia wazungu.
 
Paskali, Mungu ibariki Tanzania.

Swali lako ni suri. Sidhani kama ulitaka majibu ya ndiyo au hapana. Umetaja majina ya watu ila huwezi kutenganisha na vyama vyao.

Kulingana na chunguzi mbalimbali zihusuzo maswala (issues) ambayo ni kero kwa watanzania; nikirudi nyuma hadi 2012 ni :

  1. Afya
  2. Maji
  3. Elimu
  4. Umaskini
  5. Rushwa/utawala bora
  6. Ajira
  7. Mawasiliano (infrastructure)
  8. Misukumo ya kisiasa( Political pressures)
  9. Upungufu wa chakula
  10. Kilimo.
Mambo hayajabadilika sana pamoja ya kwamba tunaona unafuu kwenye elimu, afya na rushwa. Haya ndiyo yanashuhulikiwa na serikali ya awamu ya tano.

Tunayoyana karibuni kutoka kwa Tundu Lisu ni:
  1. Ukabila
  2. Udini
  3. Udikteta.
Hayapo kwenye kero za wananchi. Ila pia kuyumba yumba kwa msimamo wa Tundu Lisu kuhusu maswala muhimu ya nchi. Mwanzoni walisema awamu ya tano inatekeleza sera ya chama chao, agenda ya ufisadi ikaondoka, utetezi wa raslimali za nchi ukaondoka, nia yake ya kuona nchi inaadhibiwa na mataifa ya nje, na nia yake ya kuona nchi inapoteza amani. kwa hiyo mambo haya ni ya kuangalia. Kukosekana kwa msimamo wananchi wanaweza kukosa imani.

Kushuka pia kwa approval rating ya chama ambamo yumo ni shida pia. Sina uhakika kama Raisi wa awamu ya tano atagombea. Hajasema popote mbali na wapambe wake. Hata asipogomea Tundu Lisu bado ana kazi ya kuwaeleza na kueneza sera yake ya ukabila, udini na udikteta, rasilimali za nchi, amani-kutaja vichache tu- ili jamii imuelewe.

Hapa zilinganishi Tundu Lisu na Raisi wa awamu ya tano; bali Tundu Lisu kwa wananchi wakati wa uchaguzi
 
Kuna mzuri kwa kuongea na si kiutekelezaji watekelezaji wengi si waongeaji sana. Kwa 2020 ye abaki kama hazina ya baadae. Ila suala la kuongezewa Mda si jema cha msingi kuwepo na maazimio ya kitaifa akiingia yeyote ufuata kutekeleza. Sababu anaweza patikana mzuri zaid ya wa kufanya makubwa zaid, hivo ukomo ni busara zaid.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahaha ngoma itaisha saa mbili asubuhi kura za lisu hazizidi elfu tatu za mawakili plus bavicha na wenye akiri kama zako akisha fanya mikutano kumi tu sauti itakuwa imekwama maana jamaa ana panic wakati wote sauti kama anagombana na mtu hahahaha sasa hivi kisha sahau kama yeye ni Rais wa TLS anashughurika na kubwabwaja sasa akipewa urais wa nchi si itakuwa povu kila mahali jamani hicho chama cha machame hakina mgombea labda huko chini lakini line ya viongozi wenu wakuu wote zero

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tundu lissu naona amekaa kisheria sheria zaidu, nina wasi wasi na uwezo wake wa kusimamia maendeleo ya wananchi, ila all in all sidhani kama ana ushawishi mkubwa kwa wananchi kuliko lowassa , mbowe na zito. Kiufupi hafai na wala hafit hapo
Hapo sikubaliani na wewe mkuu, unakumbuka uchaguzi wa 1995? Che Nkapa alikuwa hajulikani na wala hakuwa na ushawishi wowote. Aliyemuuza Nkapa na kuwaaminisha watz kwamba Nkapa ni mtu safi anayefaa kuwa raisi ni Nyerere.
 
TUJITEGEMEE,

1. Consistent, utakuwa huelewi maanake, he has been at the forefront fighting political and institutional corruptions and the list of shame highlighted individuals who are either corrupt or were part of cartel systems n unfortunately it included JK n many other senior ccm politicians, stop being obsessed with Lowasa n if he is corrupt or was part of systems take him to court instead whining while you're government of the day. To be precise Tundu hajaanza kupiga vita uwizi Tz alipopata nafasi ya uongozi km jamaako juma ponda maharage anayeona Tz kuibiwa leo alipopata uraisi, Lissu hata sasa anapigania corruptions km vile amesema wekeni wazi mikataba ya madini, ununuzi wa ndege na mbaya zaidi matumizi ya fedha za umma km vile ni za binafsi, jiongeze kidogo kujua consistency.

2. Call it whatever you like but Lissu is looking for New Constitution kuondoa uraisi wa ufalme na udikteta Tz, just one example of radical reform, nyie mnapigania kubadili different leadership styles within the same corrupt systems.

3. Sidhani km kupenda just society ni kushinda kesi, it's about what you have been standing for in different circumstances, miaka ya 90 alisema tunaibiwa kwenye madini leo anasema tunaibiwa kwenye madini, bombardier etc etc, wanaodai leo tunaibiwa ndo waliompiga vita Lissu miaka hiyo lakini leo under different circumstances wamejigeuza watetezi wa watz, seriously?

4. Maslahi ya Tz ni pale ambapo mikataba ya madini yanakuwa wazi kwa wenye nchi au vipaumbele ya nchi huamuliwa kwa njia ya public participations, siyo unakaa na shangazi yako kuamua tununue ndege, dunia hii ina civilised and uncivilised countries, kuomba msaada jirani asitoe msaada kwa mwanafamilia kulewa ili asije kuumiza familia nyumbani ni uzalendo wa hali juu kabisa, deni la taifa is close to 50 trillion, ni busara kususiwa pale ambapo nchi inaendeshwa km mali binafsi. So Lissu is very right.

5. Mfano wa alipotumia hovyo hovyo, Lissu anaelewa nafasi ya Tz ktk dunia hii tofauti na yule anayesema Tz ni donor country wakati hata uwezo wa kusitiri MAVI hatuna, pitia mtaani utaelewa namaanisha nini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Urais ni Taasisi na hii Taasisi ili iweze kufanya vizuri Lazima itawale kwa Misingi ya sheria na utawala bora ''Rule of Laws'' Kwa sasa Taifa lina hitaji katiba mpya ambayo itajibu mambo mengi sana
 
Naona watu hamjaielewa vuzuri falsafa ya CHADEMA! Falsafa ya chadema wanataka rais atoke kanda ya kaskazini na siyo kwingineko! Je, TL anatokea Kaskazini? Si anatokea kanda ya kati Singidani? Chadema hawawezi kumpa kiti cha urais la sivyo watakuwa wamepoteza malengo yao ya kuitawala nchi. Ila kama mtu yoyote atajitokeza anatokea kati ya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro au Manyara, huyo atapewa kipaumbele cha kugombea urais. Na kama watampa mtu yeyote anayetoka nje na kanda hii, basi ni rahisi kuwageuka na kuwaacha solemba. Wadanganyeni na wasubutu kufanya hivyo, watajuta kukalibisha mgeni kwenye chama chao. Nina uhakika hawawezi kufanya hivyo!

Chimbuko la Chadema ni Kaskazini, Kanda zingine wanawekwa tu ili kusawazisha mambo na kuwafumba watu wasione malengo yao. Kamuulizeni mzee Mtei atawambia alianzisha chama kwa minajiri gani!
 
Pascal, Tundu akigombea uraisi ni ngumu kupita kwa sasa, hapo agombee tu huo huo ubunge ila tu wapinzani wakazane kupata viti kwa wingi bungeni, akigombea uraisi atakosa na bunge halitaweza kuwa chachu kama lilivyo kwa sasa
Ngumu kwa sababu zipi? Na hiyo chachu ya bunge unaiona wapi au we MP, we subiri tu 2020 itakuja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ofcoz lisu yupo vizuri sana,ila sioni sababu ya msingi ya kupunguza wabunge wa upinzani wa kujenga hoja bungeni..maana Lisu akigombea uraisi means ubunge anaacha.na uhakika wa upinzani kuingia ikulu kwa miaka yetu hii ni 0% hata kama tukishinda hatuwezi kukabidhiwa nchi.so sio kama itakuwa sahihi kupunguza mbunge kwa ushindani ulio dhahili hatuwezi kupewa ubingwa hata kama tumeshinda.
Acha kudanganya watu, Tanganyika siyo Zanzibar, dollar tutachukua kwa ushindi wa sunami, by the way, sasa hv Tz kuna bunge? Stop pretending

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom