Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

Unataka atupeleke chaka kama alivyowapeleka chaka Chadema wakaishia kudai serikali tatu na kura ya wazi/kura ya siri wakasahau kwamba ili kuiondoa serikali ya CCM lazima kuwepo tume huru ya uchaguzi. haya mengine yangefuata baadaye.

RAIS keshateua wakurugenzi wake tayari kwa uchaguzi wa 2020. Sijui huyo ambaye anaonekana bora atapenyea wapi. hata kama Rais huyu angekuwa dhaifu angeshinda tuu kwa katiba tuliyonayo.

After all binafsi I believe in Magufuli maana kwa sisi tuliopitia jeshini, ukitaka jambo liende kwa Tanzania ilipokuwa imefikia lazima nchi ipelekwe kijeshi, hakuna siasa ni KAZI TU.

Siasa tutafanya huko mbeleni tukishapata maendeleo.
 
Kwa vile wewe unaongea kisukuma basi kabla ya hoja hii mwambie Magufuli aruhusu siasa halafu ndio uje na haya.

Mmewafunga watu midomo halafu mnakuja na propaganda za kichovu , wakati magufuli anaongea anavyotaka , huyu lissu unayemuandika kila akiongea mnatuma polisi wenu kumkamata !

Wekeni kwanza uwanja sawa , huyo ndugu yako kama anafanya vizuri hofu yake kwa hawa wapinzani wachovu ni nini ?

Uwanja sawa waliupoteza wenyewe kwenye awamu ya nne. wacha sasa tuijenge nchi. hizi siasa za kijinga tumefanya miaka zaidi ya ishirini tumefanya kipi cha maana.

Halafu kukosoa gani kwa kejeli na dharau. I wish mimi ndo ningekuwa president, waropokaji wote wasio na staa ambao wanataka kuturudisha nyuma ningewaweka ndani mpaka 2020 halafu wakitoka ndo wakafanye siasa, uzuri wake katiba ya sasa inamruhusu Rais kufanya hivyo.

Tukitaka maendeleo lazima tuende sote, na kama kuna tatizo tujadiliane kwa staha. Kwa asilimia kubwa Rais anafanya yale yale ambayo hawa hawa waropokaji walikuwa wakidai awamu zilizopita leo wanapinga.

Rais piga KAZI tusonge mbele, hizi the so called demokrasi wakati mwingine zinachelewesha maendeleo.
 
Ila una mapenzi MAHABBA! na kile chama fulani japo kimoyomoyo lkn ni MAHABBA MUBASHARA!
HONGERA KWA UWAZI ULIOJIFICHA.😵
 
Swala la ubinyaji wa democrasia na Uhuru wa raia kujieleza ni uchochezi wa fujo wenye kikomo cha uvumilivu.

Uchochezi wa namna hiyo unaweza sababisha tusifike 2020
hili nalo ndio tatizo kuu la SIZONJE
 
Ha haaaaaa... Weee Paskali, yaani ndio tuseme upinzani kama wa Messi na Ronaldo unautaka 2020 in our National Election, haaaaaaa..

Haaaaaa
 
Kaka Paskali,
Nafikiri umetumia Tashtiti kwa kusema Lissu ni zaidi ya JPM! Kiukweli Lissu na mtu yeyote wa UKAWA kwenda Ikulu kwa ubabaishaji uliopo ni ndoto na huenda 2055 tukapata Rais wa Upinzani. Kwa sasa Lissu anaendesha Siasa za kitoto za kutafuta umaarufu na huruma kwa Umma! Inaonekana hana maturity pale anapoonesha dharau kwa Viongozi wa Serikali kwa kujidai anajua Sheria! Hafai, hafai, hafai kugombea URAIS wa Nchi labda uanaharakati ndio penyewe!!
 
naona mayalla umechoka kuishi mtaani nawe unataka ukajumuike na lissu huko haliko wewe endeleza hilo bandiko hapo juu kama ujatuambia hapa haya
 
Back
Top Bottom