Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

tundu lisus ni zaidi ya magufuli tatizo la magu akizidiwa hoja anaweza chukua maamuzi makali saana maana ana hasira sana huyu baba,wakati ye akikasirika mwenzie atakuwa akicheka,kwani ugumu utakuwa pale azam tv au bbc itakapowaweka pamoja kuwahoji baadhi ya hoja zao na matarajio yao sidhani kama magu atweza stahimili ya huyu tundu,tundu si wa dunia hii ipo siku mtanielewa
Tundu LA choo kumbe Si wadunia hii. Ni wa chooni au??
 
Pascal uliona mbali sana....

Kumbuka hili ni bandiko la 2017, kabla Tundu Lissu hajamiminiwa risasi zaidi ya 30!

Je katika kipindi hiki ambacho yeye Tundu Lissu ana-enjoy kura nyingi za "sympathy"

Tusifanye makosa 2020

#TunduLissuForPresidency2020
#MagufuliMustGo
 
tundu lisus ni zaidi ya magufuli tatizo la magu akizidiwa hoja anaweza chukua maamuzi makali saana maana ana hasira sana huyu baba,wakati ye akikasirika mwenzie atakuwa akicheka,kwani ugumu utakuwa pale azam tv au bbc itakapowaweka pamoja kuwahoji baadhi ya hoja zao na matarajio yao sidhani kama magu atweza stahimili ya huyu tundu,tundu si wa dunia hii ipo siku mtanielewa

So wewe unataka maneno Au kazi. Kikwete kaongea sana. Mwinyi anaweza tena kwa Sauti ya Pwani. Tz shida yenu bado mnafikiri kisecondary. Nani mropokaji tu WA kushindana na uongozi. Huna kigezo kingine chochote. Uapotea sifa za Urais toa sifa ya historia ya Kazi zake. Hata sijui kama Mayalla umemuelewa
 
Ndugu Paskali, mheshimiwa Lisu ni mtu jasiri na mwenye hoja makini lakini kwa kupewa kugombania nafasi ya urais ni bado kwanza, kwani lazima aangalie afya yake mpaka pale itakapoimarika vizuri na hali yake ya kisaikolojia ikawa vyema kwani lile shambulio la kutaka kumuua bado liko kwenye akili yake na waliyotaka kuuondoa uhai wake rasmi hawajulikani hivyo si vyema kuwa mgombea wa urais. Naona Chadema wakitaka kutoa upinzani kwa CCM bora wamsimamishe Profesa Abdallah Safari, ambaye ni mtu asiye na jazba na ni mwenye hekima za kiuongozi.

Lol. Umeandika maskini kwa unyongee. Ndio mnavyoomba huko asisimame Lissu mwakani! Tuko na Lissu 2020. Hata aje akiwa kwenye wheelchair sisi tunamtaka hivyo hivyo.
 
Uwezo gani ?wa kuongea risasi alizopigwa huko BBC, DW?da hata nyie wasomi mnakuwa kama mtu wa darasa la saba,wapiga kura hawako BBC au DW wapo hapa Tanzania,sijui ni Watanzania wangapi wanasikiliza BBC na DW. Zimeshindwa propaganda zinazotolewa hapa FJ ambayo angalau ina wafuasi kwa hapa Tanzania kulinganisha na hao BBC na DW na wamekwama sembuse huko,endeleeni kuota labda awe raisi/mwenyekiti wa Chadema, huko ndiko ungemshauri, Lissu na Lyatonga Mrema wana tofauti gani? mwishowe utakuja andika kuwa kwa ulivyosikia Shangazi nae anafaa kuwa raisi, bure kabisa Paskali
 
Hivi Pasco mayala mnaposema chadema imeshindwa kuwa chama kikuu huku bara mlitaka wafanyaje kwa mazingira Kama haya ya udikteta?

Viongozi wa upinzani mashinani mpk taifani wanauwawa wakiwa vocal sasa mlitaka wafanyaje? Au mlitaka washawishi ugaidi ndio muone chadema ina nguvu?

Kwa Hali ilivyo huwezi kuilaumu chadema unless uwashawishi watumie nguvu kupambana na dola je Hii itakuwa sawa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naunga mkono hoja. Na kama chadema wakimzingua, aingie CUF, Tadea, au kile chama cha Hashim Rungwe (sikumbuki jina), agombee kupitia huko ili achuane na Magu na mamvi.
 
superbug,
Mkuu Super bug, Mazingira ya siasa ya 1995 kwa Zanzibar yalikuwa magumu zaidi chini tya dikiteta hatari zaidi lakini CUF waliweza kuwa chama kikuu cha upinzani kule Zanzibar.

Politics is a game of hide and seek na changing variables, ili ushinde inategemea unavyojipanga na inavyoipanga timu yako, tatizo la Chadema haijawahi kujipanga.

Ni kweli kwa sasa the police atmosphere has changed, tunafuata the law of the jungle, survival is for the fittest, kwa vile Chadema imejikuta imo ndani ya mabadiliko haya ya hii changing political atmosphere, ili I survive for 2020, it has to adapt kwenye Mazingira haya haya vinginevyo inakwenda kuwa wiped completely 2020.

Chadema haita ma strategists makini, humu jf tunao na wamekuwa wakitoa ushauri wa bure .

Ili ushinde vita, silaha Kuu ni kuwa na the right info kuhusu nguvu ya adui yako. Na silaha kuu ya vita vya kisiasa ni psychological warfare.

Mpaka sasa hapa ninapoandika hapa, Chadema bado haijamjua adui yake ni nani.
P
 
Pascal Mayalla, Tatizo la Chadema ukiwakosoa na kuwapa ushauri halisi wanakubeza na kukutukana. Utaitwa ccm, utaitwa gamba, msaliti etc.
Na watamalizia na kusema chadema mpango wa Mungu.

Post ya Super bug inaonyesha kuwa chadema wamekata tamaa (eti sasa kwa mazingira haya wafanyeje). Chadema imebakia kulialia na kusubiri huruma tu.
Chadema wameshindwa hata kupinga zuio la mikutano yao..

Chadema wameshindwa kuonyesha kwenye mahakama ya katiba ubaguzi dhidi yao na ziara za kina Polepole na Bashiru..wanakagua miradi ya ccm na kueneza chama..wao wakifanya wanazuiwa...ni jambo rahisi saaaana kutengua hii amri ya eti mikutano hadi 2020..je ndivyo sheria inasema? Je ndivyo katiba inasema? Je ccm inafanya? Kama inafanya wao kuzuiwa sio ubaguzi wa kisiasa? Chama gani cha upinzani makini duniani kilishashindwa kufanya jambo kama hilo?

Yaani wameshindwa kuitisha mkutano siku ambayo Bashiru anafanya wa kwake?? Kuunda ziara ya kukagua miradi ya chama..siku pole pole anakagua yake?
Chadema inashangaza sana.

Kama chadema haiwezi kufanya yote haya kwa nini inajiita chama cha siasa tena cha upinzani? Nilidhani katika mazingira ya sasa chadema kingekuwa na nguvu zaidi kisiasa..walishindwa kuitumia momentum na influence ya Lowassa baada ya uchaguzi wa 2015, sio kupinga matokeo bali kuunda upinzani imara ambao ungeitoa jasho serikali. Idadi ya wabunge inao wa kutosha tu..ila basi tena.

Chadema wanalalamika rais anatumia pesa nje ya bajeti..sawa..je wanafanya nini? Sheria na utaratibu wa kuchukua hatua dhidi ya jambo hili viko wazi..je wamechukua? Je wanachukua hatua gani kuwajulisha wananchi rais kakosea?.. hakuna kabisa..
Pesa hizo rais ananua ndege na anajenga viwanja vya ndege, anakarabati hospitali, mabarabara etc. Wanachoona wananchi ni haya maendeleo wanafurahi..Muhimbili ya leo sio ya miaka 5 iliyopita. Jana nimeenda uwanja wa ndege kuwaaga simba mida ya saa 3 asbh. Niliona vyuma vinne vya ATC vinang'aa na kula abiria..ruti ya Kigoma-Bujumbura na Kilimanjaro-Entebbe.
Nilitabasam kimya kimya. Je madhara ya kikatiba nani anayasemea?
Chadema inafanya nini kukosoa na kurekebisha hali? Hakuna ndio maana raia wanashangaa na ukweli ni kuwa sapoti ya wananchi inashuka sana.

Sauti ya upinzani ndani ya chadema ni LISSU pekee.
Hii ni aibu kubwa kwa chadema. Tangu uchaguzi wa 2015 ni Lissu tu ndio mpiga kelele. Ni Lissu mpambanaji.
Aibu kubwa, masikitiko na uchungu ni kuwa Lissu haingwi mkono na chama chake katika hizi harakati anazofanya.

Ngoja nirejee nyuma. Mwakumbuka zile press za Lissu dhidi ya JPM na kauli zake zilizofanya akamatwe mara kwa mara na kusafirishwa na polis kutoka Dodoma hadi Dar? Ni sapoti gani alipewa na chadem? Ni viongozi gani wa juu walisimama naye hadharani na kumuunga mkono? Ni nani walishikamana naye mahakama ya Kisutu?? Hakuna cha maana. Hakuna. Lissu was a lone voice.
Lissu alikuwa ametengwa kiaina. Tofauti ilikuja kina Mbowe na wenzie walivyokamatwa na kupelekwa Kisutu. Viongozi karibu wote wa kitaifa wa Chadema walifika kisutu na maandamano ya wanachama yaliandaliwa kushinikiza kuachiwa kwao kwa dhamana. Je mbona Lissu hajapata sapoti hiyo kwenye kesi zake??

Kwa kuwa humu kuna ma great thinker, na internet ni shimo la kumbukumbu, chunguzeni kuna jambo moja kubwa na la kutia uchungu sana. Pale Lissu amepigwa risasi na anapigania maisha yake...kuna baadhi ya viongozi wakubwa chadema hawakutoa kauli ya kulaani wala ya pole. Baada ya wiki kadhaa ndio waliibuka. Hata JPM aliwawahi kwa ile tweet yake. Lissu hapendwi pale level ya juu chadema. Inauma lakini ndivo ilivyo.

Chadema inabidi ibadilike. Ijiendeshe kama chama cha siasa.
Hii lialia ni upuuzi wa hali ya juu.
Chadema ina viongozi wengi sana katika ngazi ya serikali za mitaa. Wenyeviti, madiwani, mameya na wabunge. Hawa hawafanyi kazi ipasavyo katika level ya chini y wananchi. Kujenga siasa bora na kuleta maendeleo. Vitu ambavyo mwananchi anataka ma kuthamini.
Chadema ingewatumia vizuri viongozi hawa hakuna hata katazo lolote la mikutank au vibali vy polisi vingefua dafu.
Madiwani wengi wa chadema hawaonekani kwenye kata zao, wabunge hawaonekani majimboni. Hawafanyi tena kazi na wananchi bega kwa bega.

Chadema imekuwa kama sikio la kufa. Hawabadiliki na mazingira...hawaundi mbinu mpya.
Wameshindwa hata kutumia weakness kubwa ya ccm wakati huu...hata hawaijui. Ni
Viongozi wake kupenda sifa na kutaka kukubalika na wananchi ghafla ghafla.
Afu utasikia mtu wa chadema anauliza hiyo ni advantage gani..ha ha ha hata hawajui kuwa hii weakness ndio sababu kuna viongozi wa ccm wanachukiwa saaana na wananchi. Wameshindwa kuitumia kujijrnga kiasiasa na kuwaletea wananchi wao maendeleo.

Chadema inatakiwa ijifunze siasa na ifanye siasa bora. Isisubiri matukio na mvumo wa upepo.
Sasa hivi wanashangilia umaarufu wa Lissu ambao hawapiganii kuujenga. Chadema ibadilike na ijiongeze.
 
Lol. Umeandika maskini kwa unyongee. Ndio mnavyoomba huko asisimame Lissu mwakani! Tuko na Lissu 2020. Hata aje akiwa kwenye wheelchair sisi tunamtaka hivyo hivyo.
Ni kweli nimeandika kiunyonge kwa kumuonea huruma Lissu kutokana na afya yake kwa kumbebesha mzigo wa kugombea uraisi, kampeni za kugombea uraisi si mchezo, kwa kuwa yeye ni kijana, bora asubiri kwanza na kuangalia afya yake kama si hivyo huweza akatumiwa na wachahche wanaopenda madaraka ya kumfanya kama karai la kubebea zege, likimaliza kazi yake hutupwa.

Huko 2020 hata wewe jimama26 ukiwa na mikakati mizuri ya kuikwamua nchi yetu kiuchumi, kisisasa na kimaendeleo bila ya shaka nitakuwa na wewe.
 
MsemajiUkweli, Chinibya Tume huru, kutakuwa na ongezeko kubwa sana la wabunge wa upinzani 2020.

Lakini kwa maigizo ya uchaguzi yanayofanyika sasa, kunaweza kusuwepo na mbunge hata mmoja wa upinzani.

Ndiyo maana ni muhimu kupinga udikteta kwa nguvu zetu zote. Dictatorship is an old fashion of leadership that can take our lovely Tanzania to the deep grave.
 
Back
Top Bottom