Pascal Mayalla, Tatizo la Chadema ukiwakosoa na kuwapa ushauri halisi wanakubeza na kukutukana. Utaitwa ccm, utaitwa gamba, msaliti etc.
Na watamalizia na kusema chadema mpango wa Mungu.
Post ya Super bug inaonyesha kuwa chadema wamekata tamaa (eti sasa kwa mazingira haya wafanyeje). Chadema imebakia kulialia na kusubiri huruma tu.
Chadema wameshindwa hata kupinga zuio la mikutano yao..
Chadema wameshindwa kuonyesha kwenye mahakama ya katiba ubaguzi dhidi yao na ziara za kina Polepole na Bashiru..wanakagua miradi ya ccm na kueneza chama..wao wakifanya wanazuiwa...ni jambo rahisi saaaana kutengua hii amri ya eti mikutano hadi 2020..je ndivyo sheria inasema? Je ndivyo katiba inasema? Je ccm inafanya? Kama inafanya wao kuzuiwa sio ubaguzi wa kisiasa? Chama gani cha upinzani makini duniani kilishashindwa kufanya jambo kama hilo?
Yaani wameshindwa kuitisha mkutano siku ambayo Bashiru anafanya wa kwake?? Kuunda ziara ya kukagua miradi ya chama..siku pole pole anakagua yake?
Chadema inashangaza sana.
Kama chadema haiwezi kufanya yote haya kwa nini inajiita chama cha siasa tena cha upinzani? Nilidhani katika mazingira ya sasa chadema kingekuwa na nguvu zaidi kisiasa..walishindwa kuitumia momentum na influence ya Lowassa baada ya uchaguzi wa 2015, sio kupinga matokeo bali kuunda upinzani imara ambao ungeitoa jasho serikali. Idadi ya wabunge inao wa kutosha tu..ila basi tena.
Chadema wanalalamika rais anatumia pesa nje ya bajeti..sawa..je wanafanya nini? Sheria na utaratibu wa kuchukua hatua dhidi ya jambo hili viko wazi..je wamechukua? Je wanachukua hatua gani kuwajulisha wananchi rais kakosea?.. hakuna kabisa..
Pesa hizo rais ananua ndege na anajenga viwanja vya ndege, anakarabati hospitali, mabarabara etc. Wanachoona wananchi ni haya maendeleo wanafurahi..Muhimbili ya leo sio ya miaka 5 iliyopita. Jana nimeenda uwanja wa ndege kuwaaga simba mida ya saa 3 asbh. Niliona vyuma vinne vya ATC vinang'aa na kula abiria..ruti ya Kigoma-Bujumbura na Kilimanjaro-Entebbe.
Nilitabasam kimya kimya. Je madhara ya kikatiba nani anayasemea?
Chadema inafanya nini kukosoa na kurekebisha hali? Hakuna ndio maana raia wanashangaa na ukweli ni kuwa sapoti ya wananchi inashuka sana.
Sauti ya upinzani ndani ya chadema ni LISSU pekee.
Hii ni aibu kubwa kwa chadema. Tangu uchaguzi wa 2015 ni Lissu tu ndio mpiga kelele. Ni Lissu mpambanaji.
Aibu kubwa, masikitiko na uchungu ni kuwa Lissu haingwi mkono na chama chake katika hizi harakati anazofanya.
Ngoja nirejee nyuma. Mwakumbuka zile press za Lissu dhidi ya JPM na kauli zake zilizofanya akamatwe mara kwa mara na kusafirishwa na polis kutoka Dodoma hadi Dar? Ni sapoti gani alipewa na chadem? Ni viongozi gani wa juu walisimama naye hadharani na kumuunga mkono? Ni nani walishikamana naye mahakama ya Kisutu?? Hakuna cha maana. Hakuna. Lissu was a lone voice.
Lissu alikuwa ametengwa kiaina. Tofauti ilikuja kina Mbowe na wenzie walivyokamatwa na kupelekwa Kisutu. Viongozi karibu wote wa kitaifa wa Chadema walifika kisutu na maandamano ya wanachama yaliandaliwa kushinikiza kuachiwa kwao kwa dhamana. Je mbona Lissu hajapata sapoti hiyo kwenye kesi zake??
Kwa kuwa humu kuna ma great thinker, na internet ni shimo la kumbukumbu, chunguzeni kuna jambo moja kubwa na la kutia uchungu sana. Pale Lissu amepigwa risasi na anapigania maisha yake...kuna baadhi ya viongozi wakubwa chadema hawakutoa kauli ya kulaani wala ya pole. Baada ya wiki kadhaa ndio waliibuka. Hata JPM aliwawahi kwa ile tweet yake. Lissu hapendwi pale level ya juu chadema. Inauma lakini ndivo ilivyo.
Chadema inabidi ibadilike. Ijiendeshe kama chama cha siasa.
Hii lialia ni upuuzi wa hali ya juu.
Chadema ina viongozi wengi sana katika ngazi ya serikali za mitaa. Wenyeviti, madiwani, mameya na wabunge. Hawa hawafanyi kazi ipasavyo katika level ya chini y wananchi. Kujenga siasa bora na kuleta maendeleo. Vitu ambavyo mwananchi anataka ma kuthamini.
Chadema ingewatumia vizuri viongozi hawa hakuna hata katazo lolote la mikutank au vibali vy polisi vingefua dafu.
Madiwani wengi wa chadema hawaonekani kwenye kata zao, wabunge hawaonekani majimboni. Hawafanyi tena kazi na wananchi bega kwa bega.
Chadema imekuwa kama sikio la kufa. Hawabadiliki na mazingira...hawaundi mbinu mpya.
Wameshindwa hata kutumia weakness kubwa ya ccm wakati huu...hata hawaijui. Ni
Viongozi wake kupenda sifa na kutaka kukubalika na wananchi ghafla ghafla.
Afu utasikia mtu wa chadema anauliza hiyo ni advantage gani..ha ha ha hata hawajui kuwa hii weakness ndio sababu kuna viongozi wa ccm wanachukiwa saaana na wananchi. Wameshindwa kuitumia kujijrnga kiasiasa na kuwaletea wananchi wao maendeleo.
Chadema inatakiwa ijifunze siasa na ifanye siasa bora. Isisubiri matukio na mvumo wa upepo.
Sasa hivi wanashangilia umaarufu wa Lissu ambao hawapiganii kuujenga. Chadema ibadilike na ijiongeze.