Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

Ha ha ha ha.. Lissu ni mzuri sana, ana akili sana, ni mpambanaji sana, na anaijua sheria sana.. Kwa kifupi yuko vizuri sana..
Ila kwa uraisi kwa maoni yangu hapana..
Mkuu Sosoliso, kwanini unasema Lissu kwa urais hapana?.
Kwa hiyo Chadema wame bugi step kumpitisha?
P
 
Wanabodi,

Hii ni update ya hizi trends nilizozizungumza humu za kuelekea 2020,
  1. Humu nilisema uchaguzi wa 2020, wapinzani wengi watapoteza majimbo na kata zao na kuchukuliwa na CCM, hivyo wanasiasa wenye kuona mbali watajiunga na CCM, hili limeendelea kufanyika na kutokea.
  2. Chadema wameishajua watapoteza kata karibu zote na majimbo karibu yote kwa madiwani na wabunge wake kuhamia CCM, ndio maana inaweza kuwafuta uanachama wabunge wake, kinyume cha katiba yake, kanuni na bila kufuata taratibu walizojiwekea.
  3. Tangazo la Mhe. Spika jana Bungeni kuwa Mhe. Mbowe hatarudi Bungeni ni uthibitisho wa hoja za bandiko hili, kuwa kama hata Mwenyekiti wa Taifa Chadema, Mhe. Freeman Mbowe hata rejea Bungeni!, then who will?!.
  4. Mbowe ni Mbunge wa Machame, amechaguliwa na wananchi wa Machame kuwa Mbunge wao na mwakilishi wao Bungeni, wenye uamuzi wa kama Mhe. Mbowe atarejea Bungeni au la, ni wapiga kura wa Machame na sio Spika wa Bunge. Kwa vile Spika wa Bunge ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, kauli ya Spika kuwa Mbowe hatarejea Bungeni ni kauli nzito inayithibitisha nilicho kisema humu kuwa Bunge la 2020 ni Bunge la CCM and CCM only!.
  5. Cheo cha Spika ni miongoni mwa vyeo vya derivatives au secondary, cheo cha msingi ni ubunge, yaani mtu huwezi kuwa spika hadi kwanza uwe Mbunge, the same kwa mawaziri na manaibu mawaziri, hivyo cheo chs msingi cha Spika wa Bunge ni Mbunge wa Kongwa, uspika ni cheo cha sekondari tuu kinaweza kuondolewa. Kitendo alichofanya Spika kumtangaza Mbowe hatarejea Bungeni ni Spika kukivaa kichwani cheo cha Spika, hivyo uspika umempanda kichwani na kuvuka mipaka ya jurisdiction yake, kwa Mbunge wa Kongwa, kuwaamulia wana Machame nani ndiye atakuwa Mbunge wao 2020 na sio Mbowe hata kama wao Mbowe wanampenda vipi!. Hili la vyeo kuwapanda kichwani baadhi ya viongozi ni tatizo kubwa!. Kwa mfumo wetu wa vyama vingi, hata rais wa JMT hawezi kutangaza hadharani kitu ambacho Spika amekitangaza!, if anything happens to Mbowe, Spika will be in hot soup to justifies alipotangaza kuwa Mbowe hatarejea Bungeni, how did he know?, kwani CCM wamepanga kumfanya nini Mbowe hadi asirejee Bungeni?, au by now tayari Spika wa Bunge ameisha letewa orodha ya wabunge wa 2020 ambayo inaonyesha Mbowe hatakuwepo?.
  6. Wakati napandisha bandiko hili, kitu kinachoitwa The NCCR Mageuzi Factor was not there hivyo nikaeleza humu kuwa wabunge wote wanaojitambua, wahamia CCM, lakini kufuatia a recent assumed secret alliance between CCM and NCCR Mageuzi to be secret allies, ili kuepuka aibu ya kurejea CCM, baadhi ya watakao hama Chadema hawahamia CCM bali watahamia NCCR-Mageuzi kwa ahadi kuwa CCM haitasimamisha wagombea wenye nguvu katika majimbo ya NCCR-Mageuzi.
  7. Kitakacho tokea ni ili kuubomoa upinzani kwenye maeneo ambayo ni ngome ya Chadema, na CCM kamwe haiwezi kushinda, hatua ya kwanza ni kuzigawanya jura za upinzani. Uchaguzi wa 2020 NCCR-Mageuzi haitajiunga na upinzani kusimamisha mgombea mmoja dhidi ya CCM.
  8. Hivyo sasa wote watakao enguliwa Chadema ama watajiunga CCM ama NCCR-Mageuzi, hivyo kila jimbo la Chadema kwa 2020 litakuwa na wagombea 3, mgombea wa Chadema wenye jimbo, mgombea wa NCCR-Mageuzi na mgombea wa CCM.
  9. Kwavile jimbo lilikuwa Chadema mfano Rombo, then kuna watu ni loyalists wa Chadema, wao wakamchagua mgombea yeyote atakayepitishwa na Chadema.
  10. Joseph Selasini atagombea kupitia NCCR-Mageuzi hivyo kuna wana Rombo wanamkubali hivyo watampigia jura zao
  11. Mchuano mkali utakuwa ni kati ya Chadema na NCCR-Mageuzi ndio wata zi split kura za upinzani kwa kugawana kura huku mgombea wa CCM amesimama pembeni akishuhudia vita vya panzi.
  12. Matokeo ya mwisho ni atakashinda ni mgombea wa CCM kwa slim margin kwasababu Chadema na NCCR-Mageuzi watagawana. Hata Mwenyekiti mwenyewe wa NCCR-Mageuzi hatakuwa salama jimbon kwake kwasababu Chadema watamsimamishia mtu, CCM itajiokotea, hivyo hoja ya 2020 ni CCM pekee kwa huku bara still stands.
  13. Sehemu pekee trick hii itagonga mwamba ni Zanzibar, kule CCM itafanya alliance na CUF ili wapinzani wagawane kura kati ya CUF na ACT-Wazalendo ili CCM washinde. Kwa kule ACT-Wazalendo haswa kwa upande wa Pemba, I doubt kama CUF or CCM wataambulia kitu. Hivyo wabunge pekee wa upinzani wenye uhakika wa kuingia Bungeni ni kutoka ACT-Wazalendo.
  14. Kwa upande wa bara, kama Zitto asipoteuliwa kuwa mgombea urais wa JMT kwa tiketi ya upinzani, (if Tundu Lissu atarudi), then kwa maoni yangu, Zitto ndiye Mbunge pekee wa upinzani atakayesema kuli retain jimbo lake kwa kirahisi, hivyo Zitto ndio likely atakuwa KUB kwa Bunge la 2020, hivyo kwa jinsi ninavyomfahamu na kwa uwezo wake, huo Muziki wake as KUB, licha ya Bunge lijalo kuwa CCM dominated, lakini mchakamchaka wa Zitto utakuwa usipime!.
P
Ulikuwa unajitekenya na kucheka mwenyewe Mnampala
 
Hana jipya, alafu ukisoma huu uzi vyema utawagundua wanafiki wengi sana ambao walikuwa wakimponda TL na sasa eti ni wanaharakati wanaomkubali.
Kila Goti Litapigwa kwa Lissu.

Jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la Pembeni(kona)
 
Labda , mimi nionavyo. Uonavyo wewe sema, haya ni maoni ya sisi wapiga kura kufuatana na hali ya kisiasa tunavyo iona.
Upo sahihi kbs.

Kaka Paschal aliona mbali kwa hii article yake na mara nyingi huwa prophecy zake zinatimiaga. Nataman kama kutakuwa na mdahalo ngazi ya Urais, yeye ndiye awe muongazaji mkuu wa mdahalo huo maana ana maswali fikirishi na yenye faida kwa Taifa.
 
Wewe ni mnafiki.
Only imbeciles ndo huwa hawanadiliki. Hata kama anaona anakwenda kwenye moto yeye anakwenda tu. Yes by then Lissu nilimwona hafai mbele ya Magufuli. Ila sasa Magufuli kuna vitu kaharibu naona bora Lissu. Tatizo lipo wapi ?Wapumbavu peke yao ndo huwa hawabadili misimamo yao hata kama msimamo wa mwanzo unawapeleka kwenye hatari. Iam not stupid.
 
Only imbeciles ndo huwa hawanadiliki. Hata kama anaona anakwenda kwenye moto yeye anakwenda tu. Yes by then Lissu nilimwona hafai mbele ya Magufuli. Ila sasa Magufuli kuna vitu kaharibu naona bora Lissu. Tatizo lipo wapi ?Wapumbavu peke yao ndo huwa hawabadili misimamo yao hata kama msimamo wa mwanzo unawapeleka kwenye hatari. Iam not stupid.
Nimekunyooshea mikono Victoire uko vizuri sana kwenye sector ya unafiki.
 
This was 2017.Tupo 2020 by now. VITU VINGI SANA VIMEBADILIKA. NI IMBÉCILES PEKE YAO NDO HAWABADILIKI KATIKA SITUATION AMBAZO WANATAKIWA KUBADILIKA.
Narudia Tena Ni mpumbavu pekee anaweza akabaki na msimamo wake wa awali hata Kama unaenda kumpelekea umauti. Welevu hubadilika kulingana na nyakati na mifumo
 
Mkuu Waberoya, maadam sasa ni Lissu kapitishwa Chadema, jee akipitishwa na NEC, ndie atakuwa rais?.
P

Kapitishwa na CHADEMA yote? Kutokoa mioyoni mwao? Wanaamini anaweza kabisa kuwa rais?

Yaani wanaamini kabisa au wako under influence? Au sympathy? Au hakuna alternative?

Naomba tu niyatoe maneno yangu au niifute post,

Hawezi kuwa rais, sitamani awe rais,nitaomba asiwe rais
 
Kapitishwa na chadema yote? Kutokoa mioyoni mwao? Wanaamini anaweza kabisa kuwa rais?

Yaani wanaamini kabisa au wako under influence? Au sympathy? Au hakuna alternative?

Naomba tu niyatoe maneno yangu au niifute post,

Hawezi kuwa rais, sitamani awe rais,nitaomba asiwe rais
utashangaa na roho yako
 
Wanabodi,
Tundu Lissu ndie mwanasiasa pekee wa upinzani ambaye so far, ameonyesha ana uwezo wa kumkabili Magufuli kwa vile uwezo wake ni zaidi ya Magufuli?

NB. Sijasema Lissu ni zaidi ya Magufuli kwenye nini, na nawaomba sana msiniulize!.

Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali
Mh. Pasco, kuna jambo moja tu, Magu na Lisu wanafanana
Naunga mkono hoja, ndio maana nilipandisha bandiko hili.
P
 
Kapitishwa na chadema yote? Kutokoa mioyoni mwao? Wanaamini anaweza kabisa kuwa rais?

Yaani wanaamini kabisa au wako under influence? Au sympathy? Au hakuna alternative?

Naomba tu niyatoe maneno yangu au niifute post,

Hawezi kuwa rais, sitamani awe rais,nitaomba asiwe rais
Siyo matamanio yote anayo kuwa nayo Mtu, yanatimiaga! Ugua pole!!
 
Upo sahihi kbs.

Kaka Paschal aliona mbali kwa hii article yake na mara nyingi huwa prophecy zake zinatimiaga. Nataman kama kutakuwa na mdahalo ngazi ya Urais, yeye ndiye awe muongazaji mkuu wa mdahalo huo maana ana maswali fikirishi na yenye faida kwa Taifa.
Tutajua
 
Back
Top Bottom