GE2025 Tundu Lissu: Ni ajabu Mshtakiwa ndiye anayedai apelekwe Mahakama Kuu ashitakiwe, kama ana hatia anyongwe!

GE2025 Tundu Lissu: Ni ajabu Mshtakiwa ndiye anayedai apelekwe Mahakama Kuu ashitakiwe, kama ana hatia anyongwe!

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Tundu Lissu "Ni ajabu Mhe kwamba Mshitakiwa ndiye anayedai apelekwa mahakama kuu ashitakiwe kama mahakama itaona ana hatia anyongwe, mshitakiwa ndiye anayesema twendeni huko."

Fuatilia hapa: Mwenendo wa Kesi ya Lissu (Uhaini) kuendelea leo Julai 30, 2025, afikisha siku 112 akiwa Gerezani

Makahama ingekua huru leo Lisu angeachiwa. Hakimu kawaokoa sana mawakili wa serikali. Ule msisitizo alioutoa unaonyesha wazi angefanya maamuzi ingekula kwao. Kusema atafanya maamuzi baaday ya kuwasikiliza tena tarehe ijayo ni kuonyesha wazi leo wameshindwa kuishawishi mahakama.
 
Kama ukoo wa heche,lissu na lema unavonyonya michango ya chadema
20250417_093236.jpg

Kuna tozo hazifiki kunakohusika. Ccm na magenge yao huzichota na kuzitafuna.
20250327_181820.jpg
 
Haki imeshindwa, Mahakama ni toothless bulldog….basi, hata ubinadamu hakuna kweli?
 
Rostam Alishamaliza kila kitu kuhusu Mahakama zetu. Na ukitaka kujua Kwa undani Mahakama za tz zinavyofanya KAZI tafadhali sana rejea kauli ya Rostam aliyoitoa.
 
Ukweli hapo hakuna kesi ya uhaini bali ni woga wa Samia tu wa kukutana na Lissu kwenye uchaguzi ndiyo maana katumia Polisi na Mahakama kuendelea kumuweka kizuizini hadi uchaguzi uishe. Kwenye uchaguzi huru na wa haki Samia hamuwezi Lissu, anapigwa asubuhi tu tena kwa ushindi wa kishindo.
 
Tuna serikali ya hovyo na ya kishetani haswa nadhani mfumo umejaa laana na dhulma tupu
Yaani serikali ya ccm hata liwe jiwe litatenda haya mambo ya hivyo ....hawana hata SONI majirani zangu muda kipindi hiki nikijua ni maccm nayapotezea sitaki ushirika nao maana hata ukiyaangalia humu mitaani mambo yaao ni HOVYO
 
Back
Top Bottom