Tundu Lissu: Ni ufisadi na ufujaji wa fedha za umma kwa Bunge kuwalipa watu ambao hawana sifa za kuwa wabunge

Tundu Lissu: Ni ufisadi na ufujaji wa fedha za umma kwa Bunge kuwalipa watu ambao hawana sifa za kuwa wabunge

Hata wale Viti Maalum wa CCM nao wanakula tu kodi zetu. Wana kazi gani wale!! Wanamuwakilisha nani pale Bungeni?

Zaidi tu ya kupiga vigelegele na kushindana kwenye uvaaji wa mavazi ya gharama?

Katiba ya Wananchi ilifutilia mbali huu ujinga wote wa viti maalum na pia ule wa wale marafiki 10 wa Rais.

#Bring back our New Citezens Constitution#
 
Tangu nipuuze wanasiasa kuwa hawawezi kunifanyia lolote, naishi kwa amani sana.
 
Ukidai risiti ukienda nunua siku nyingine wanakupandishia bei
 
Nunua usidai risti afu ukutane na TRA utachokutana nacho wakukusaidia apo ayupo
 
Naam wana bodi!

Leo nimetafakari sana maneno na vitendo vya Speaker wa Bunge la JMT, ndugu Job Ndugai.Hivi huyu mtu anatuona sisi watanzania hatujitambui, tunamuogopa au anatuona wajinga? Haiwezekani mtu anachezea fedha zetu kuwalipa side chicks wake!! Hivi wale wabunge 19 wako Bungeni kupitia chama gani? Anachezea kodi zetu kuwalipa vidosho?..
Chief naunga mkono hoja kama ifuatavyoo.
 
Kama Taifa tuanzishe mgomo kwa kitu kimoja cha muhiku sana kwa uchumi wa nchi hata kwa siku saba tu kwa ajili ya huyu mtu!! Ninkweli kashawaona watanzania mazezeta kumbe tunajitambua sana!!

Mgomo si lazima kuandamana...huu ni wakati wa utandawazi!!
 
Wajuzi wa Sheria na Katiba wanisaidie.

Nijuavyo huwezi kuwa Mbunge, Rais, Diwani bila kuwa na chama labda uteuliwe na Rais au vinginevyo.

Swali langu hawa kina mama/dada 19 waliowahi kuwa wana-Chadema wakavuliwa uanachama leo wako Bungeni wanamwakilisha nani? Katiba yetu haijasiginwa?

Kwa nini wasizuiwe getini? Ni wapi panatoa uhalali wa kuingia Bungeni?
 
Back
Top Bottom