Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Nikiibiwa kura nitawaingiza Wananchi barabarani

Acha kumuongezea maneno yako..
Yeye kasema akiibiwa kura..ina maana atakuwa na uthibitisho wote kwamba ameibiwa kura zake..ataingiza watu barabarani..
CCM mmezoea sana wizi.
 
Amuulize Mange kwanza 😁 😁 😁 😁, i cant wait ................................
Mange haikuwezekana tu kwa sababu ya timing. During Election time it's much easy kuorganize ... watu wanakuwa na Euphoria. Unahitaji watu kama 50,000 tu kulianzisha .... Kama wameweza Egypt, Syria hivi kweli unafikiria Tz haiwezekani kwa ajili tu ya POPLICCM ...!!
 
Kwahiyo kwenu ninyi kuiba kura ni sawa lakini kutembea barabarani ni kosa la jinai?
 
WEZI WAKOMESHWE TU
 
LISU HAKUBALI KUIBIWA KAMA ILIVYO KWANGU
 
Yaani kichwani kwake keshaanza kuchagua rangi ya pazia atazoweka Ikulu; ni swala la muda kabla ya watu kukubali huyu mtu anahitaji psychological intervention ajatulia bado kutokana na mkasa uliompata na wala hana sifa za high office.

Hayo maneno, kwamba amekuwa hivyo kwa sababu ya risasi, unampamba tu. Kwa wale tunaomjua Lissu hajabadilika. Maisha yake yote haheshimu mamlaka. Kwake yeye ndiye mamlaka ya mwisho. Ushahidi ni maneno aliyoyatamka wakati wa kuomba kura kwenye Mkutano wa Baraza Kuu la CHADEMA. Hayo maneno yanawakilisha kwa 100% tabia yake.

Lissu, anajua fika kuwa kesi zinazomkabili zinamweka katika mazingira magumu. Kwenye huo mkutano, akijibu swali kuhusu hizo kesi alijigamba kuwa hatishiki. Kwa hivyo anatafuta njia ya kutokea, ambayo ni ya yeye kuchaguliwa na chama chake kuwa mgombea wa Urais. Kichwani mwake, kwa jeuri aliyo nayo, anamini kuwa, kama mgombea Urais, kutampa kinga dhidi ya hukumu na kitendo chake cha kufutiwa dhamana, baada ya wadhamini kujitoa.

Na isitoshe ana "kiporo" cha kueleza kuhusu tukio la kushambuliwa, wakati dereva, shahidi wake muhimu, kafichwa.
 
Ameanza!!!
Mdomo umempatia risasi za kutosha,bado hakomi!
 
DAM55, Tafadhari, wewe ni mtu wa heshima sana humu, acha kupost kila kinachopostiwa na wengine bila kulijidhisha... Tundu alisem hivi jana

"Mimi sio yule wa kusema namwachia Mungu..."
 
Tukiibiwa kura hata mimi sitamsubiri Tundu Lissu kuniingiza barabarani. Akija kutamka atanikuta nikichanja mbuga kumkabili mwizi!
 
AJE ATANGULIE YEYE AKUMBANE NA VIRUNGU VYA MAMBOSASA ARUDI TENA UBERJIJI KUJIUZA
 
Sidhani kama wananchi watakuwa tayari kuingia barabarani kwa faida za wanasiasa.
Kauli hizi si tu ni hatari kwa usalama wa nchi bali ni hatari hata kwa yeye mwenyewe.
Hekima ya Mwenyezi Mungu inahitajika kumuongoza Mh. Lissu katika mbio za Urais, mtu mmoja hawezi kuwaingiza watu barabarani labda kama kuna mpango waliokwisha kuuandaa muda mrefu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…