MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,113
- 65,124
aseme akishindwa, na watapigwa kweli
Wananchi gani?
Hawa hawa wadanganyika wanaokupa moyo mitandaoni ikifika siku yenyewe kila mtu amejifungia kwake?
Sisi ambao tumefuatilia siasa za Tanzania tokea awamu ya kwanza tumewahi shuhudia watanzania wakiasi nchi na kutaka hadi kumuua Baba wa Taifa zaidi ya mara moja. Kaa ukikumbuka kwamba huyu Baba wa Taifa ndiye Raisi ambaye aliwahi kupendwa kuliko maraisi wote Tanzania na alilindwa sana na vyombo vya usalama. Lakini miaka yake ya mwisho ilikuwa imejaa vimbwanga vingi kutoka kwa watanzania hadi ikampelekea ang'atuke kwa amani.
Sasa sembuse utawala wa awamu ya tano kweli ??? Hivi nyie wandungu mmepeleka akili zenu likizo hadi kuzisahau siasa za Tanzania kipindi cha funga mkanda. Nadhani wewe ni shabiki na una utoto mwingi sana, lakini kama ungekuwa ni mtu mzima nadhani ungefahamu kwamba Tanzania inapita katika kipindi kigumu kuliko wakati wowote ule. Kama hatutakuwa makini basi tutakuja kuikumbuka hii miaka kwa masikitiko sana huko mbeleni.