GRANDPUBA
JF-Expert Member
- Nov 10, 2012
- 751
- 790
Hao watu wa kuingia barabarani, Ni barabara hizi za kwetu hapa Tanzania, au Ubelgiji?Hiyo ndio Kauli ya Mh Tundu Lissu iwapo ikitokea ameshindwa kwenye uchaguzi mkuu mwezi October 2020. Ataingiza watanzania barabarani ikiwa ataibiwa kura zake.
View attachment 1526711
My take: Ni mapema Sana kwa mgombea urais kutoa kauli Kama hii si kiashiria kizuri. Anataka kutuaminisha kuwa hata ikitokea ameshindwa kihalali tuamini kuwa kaibiwa kura ili atimize azima yake.
Uongozi wa CHADEMA umshauri huyu mgombea kauli hizi hazifai kwa usalama wa nchi yetu.
Na atakayeongoza hao watu ni yeye na wale watoto wake na familia yake, au Wabelgiji na Wajerumani?
Huyu alikwisha fahamika kuwa Ni mtu asiye na vision yoyote wala hana agenda ya maendeleo katika Nchi hii.
Huyu anachohitaji ni jukwaa la kueneza uchochezi , chuki, fitina ili Nchi hii iingie kwenye machafuko na kila kitu kizuri kilichoanzishwa kiharibike tukose wote, kwa sababu yeye na hao waliomtuma wanafahamu fika kwamba anatumika tu, hawezi kuchaguliwa kuwa Rais kwa sababu hana chochote cha ku_deliver.
Kwa hiyo, hili halitowezekana kwa sababu tunataka kuendelea kuona watoto wetu wakiwa wanaongozana kila siku asubuhi wakielekea shule huku wakiwa katika hali ya utulivu Kama ilivyo sasa, tunataka kuendelea kuona watoto wetu wakisubiri mabasi ya shule vituoni na kwenye "junctions" wakiwa wanacheka kwa furaha kama ilivyo hivi sasa bila kuhofu milipuko.
Tunataka kuona rasilimali za Nchi hii zikiendelea kulindwa na kuinufaisha Nchi hii na Wananchi wake.
Haya yote, pamoja na masuala mengine muhimu kwa Nchi hii na raia wake, tayari yameshawekewa misingi thabiti, na misingi hii lazima ilindwe kwa gharama yoyote dhidi ya mtu/ kikundi chochote wenye lengo ovu la kuivunja na kuisababishia Nchi kuingia kwenye vurugu kwa sababu za kutumika tu.