Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Nikiibiwa kura nitawaingiza Wananchi barabarani

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Nikiibiwa kura nitawaingiza Wananchi barabarani

Hadi sasa Katiwa ulemavu na hakuna alichofanya ni sawa na kumuachia Mungu tu,sasa akiibiwa kura ndio atafanya nini na watanzania hawa wa Mange kimambi?
 
Halafu hao wananchi wafanye nini?! Wamtafute aliyeshinda au aliyetangaza mshindi?!
Judge Kaijage atakuwa kama Lubuva.
 
Kwa macho yangu nimeshuhudia mawakala wa upinzani wakati wa uchaguzi wa marudio wakipigwa na jeshi la polisi ili kusaini fomu fake za matukio. Kwa macho yangu niliona uchaguzi wa marudio hapo jimbo la Mtolea wakati wa uchaguzi wa marudio kupitia kituo cha ITV mabox ya kura yakitolewa kwenda kujazwa kura za ccm, na haya yalifanyika mbele ya polisi na afisa wa tume ya uchaguzi. Na hakuna hatua yoyote ilichukuliwa. Kwa macho yangu nilishudia msimamizi wa uchaguzi akifunga ofisi ili asipokee fomu ya mpinzani ili mgombea wa ccm apite bila kupingwa.

Hayo ni baadhi tu ya matendo yaliyofanyika mbele ya wapiga kura, na haya yalikuwa ni maagizo maalum. Baada ya ccm kunogewa na hali hiyo, uchaguzi wa SM ndio kukafanyika uhayawani wa wazi. Je kuendelea kukalia kimya ushenzi huo ni mpaka lini? Kwakuwa ccm mmeamua kuichezea amani, ngoja itumike njia itakayowafanya kuheshimu box la kura. Enough is enough, hakuna mwananchi asiyejua ushenzi unaoendelea kwenye box la kura, ndio maana watu hawajitokezi kwenye upigaji kura.
Kule Bungeni CCM hukosa umakini kwa kuwa wabunge wake wengi huwa siyo chaguo la wapiga kura nafsi zinawasuta sana kwa vitendo vya kuiba kura ambavyo huwafanya kujutia madhambi yao mda mwingi badala ya kujenga hoja kuwaletea maendeleo jamii zao
 
Huyu mdau mbona mbinafsi sana, badala aseme "ataingia na wanachi barabarani" yeye anasema "atawaingiza wananchi barabarani". Au hajasema yeye atakuwa wapi muda ambao wanachi atawaingiza barabarani ?
 
Hadi sasa Katiwa ulemavu na hakuna alichofanya ni sawa na kumuachia Mungu tu,sasa akiibiwa kura ndio atafanya nini na watanzania hawa wa Mange kimambi?
Kufanyiwa ubaya awali hukupa mbinu za kukabili ubaya unaokuja mbele, atafanya nini subiria wamuibie kura utaona atakachokifanya
 
Hiyo ndio Kauli ya Mh Tundu Lissu iwapo ikitokea ameshindwa kwenye uchaguzi mkuu mwezi October 2020. Ataingiza watanzania barabarani ikiwa ataibiwa kura zake.

View attachment 1526711

My take: Ni mapema Sana kwa mgombea urais kutoa kauli Kama hii si kiashiria kizuri. Anataka kutuaminisha kuwa hata ikitokea ameshindwa kihalali tuamini kuwa kaibiwa kura ili atimize azima yake.

Uongozi wa CHADEMA umshauri huyu mgombea kauli hizi hazifai kwa usalama wa nchi yetu.
Kwanini usiwashauri tume ya uchaguzi wasicheze na kura? Tatozo Ni wizi wa kura, Kama hakuna wizi wa kura automatically hakuna maandamano
 
So mkuu unataka akiibiwa kira aende akalale zake home?
Mkiambiwa umatanga wenu umesababishwa na elimu duni mnasema mmetukanwa.
Kuwa na elimu duni hamkumfazi mtu awe mbumbumbu wa mantiki.
Suala la kuibiwa kura halipo na kama litakuwepo litasababishwa na wao wenyewe kujiibia kura ili kujustify walichokipanga kufanya.
 
Huyu mdau mbona mbinafsi sana, badala aseme "ataingia na wanachi barabarani" yeye anasema "atawaingiza wananchi barabarani". Au hajasema yeye atakuwa wapi muda ambao wanachi atawaingiza barabarani ?

..na wanaopanga kumuibia kura na kumdhulumu wao siyo wabinafsi?

..tujielekeze ku-deal na watu waliounajisi mfumo wetu wa uchaguzi kiasi kwamba vyama vya upinzani havina imani nao.
 
..na wanaopanga kumuibia kura na kumdhulumu wao siyo wabinafsi?

..tujielekeze ku-deal na watu waliounajisi mfumo wetu wa uchaguzi kiasi kwamba vyama vya upinzani havina imani nao.
Unao ushahidi kuonyesha kuna watu wanapanga kumuibia kura ?
 
Kauli za mfa maji. Yeye ajiandae kuipatia ruzuku ya kutosha CDM. Nani aandamane kuhatarisha uhai wake kisa ulaji wa kikundi cha watu flani.
Nakufeel nikikuona kwenye baadhi ya threads, japo hatujuani. Ila haya mambo ya siasa, my dear one's unaniangusha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uongozi wa CHADEMA umshauri huyu mgombea kauli hizi hazifai kwa usalama wa nchi yetu.
Nilipoona jana wanabadili Tunu yetu ya taifa, utambulisho wetu wa Taifa yaani wanageuza maneno ya Wimbo wa Taifa kwa kuweka maneno ya chama chao, nikajua hapa hawa hawana nia njema na watanzania. Wana ushari. Na wanachokitafuta watakipata.

Hakuna mtanzania anaweza kukubali chama kumpitisha mgombea ambaye aliitakia mabaya Tanzania awe huyo huyo kuwaongoza kelekea barabarani. Lissu ni mwanaharakati si mtu wa kusimamia mfumo wa uongozi wa nchi. Hili nililisema muda mrefu sana. Hapa watu wataanza kunielewa.

Na kwa kosa la jana nadhani wanatafuta sababu ya kujitoa uchaguzi kukwepa aibu kushindwa vibaya sana hapo October, 2020.
 
Kufanyiwa ubaya awali hukupa mbinu za kukabili ubaya unaokuja mbele, atafanya nini subiria wamuibie kura utaona atakachokifanya
Kwa hivyo tu mkuu hata Tanzania tunaweza kumchimba mkwara US.

Hebu niambie tu ni lipi la kufikiria ambalo Lissu anaweza kufanya? Kushtaki kwa wazungu au kuingiza wananchi barabarani?

Mtu ambaye pale alipo hata usalama wa maisha yake tu kamuachia Mungu,sasa hapo ana lipi la kufanya endapo ccm wakiiba kura?

Tuacheni huu ulevi wa siasa,hata kwa Lowasa kuna watu waliamini kuwa ccm wasingeweza kuiba kura.
 
Back
Top Bottom