Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Nikiibiwa kura nitawaingiza Wananchi barabarani

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Nikiibiwa kura nitawaingiza Wananchi barabarani

Wezi wa kura mwaka huu wataumbuka sana.
Viongozi wenu wa vyama pinzani wana waaminisha kuwa hakuna jema linalotenda na viongozi waliopo...

Uchu wa madaraka umewajaa tunaongea Ila mwishowe baada ya uchaguzi utasikia tumeibiwa kura[emoji1787][emoji1787]
 
Polisi walipiga ban mapokezi ya Lissu uliona kilichotokea?

Nyie endeleeni kupuuza lakini waTz wamechoka

Lissu hazuiliki mazee, hata risasi zaidi 38 zilishindwa kumnyamazisha sababu MWENYEZI MUNGU ALIE HAI yuko upande wake siku zote.
Teh teh teh!

Jaribu tena maana ile iliingiliana na maombolezo ya hayati mzee Mkapa,kwaiyo ukisema risasi 38 mnamdanganya ajione kama PREDATOR sio?

Nikurushie risasi 38 kama utapona wewe?
 
Lissu,Lissu _heart_️_heart_️_heart_️ ( 800 X 640 ).jpg
 
Viongozi wenu wa vyama pinzani wana waaminisha kuwa hakuna jema linalotenda na viongozi waliopo...

Uchu wa madaraka umewajaa tunaongea Ila mwishowe baada ya uchaguzi utasikia tumeibiwa kura[emoji1787][emoji1787]
Joined july 26 2020
 
Hiyo ndio Kauli ya Tundu Lissu iwapo ikitokea ameshindwa kwenye Uchaguzi Mkuu mwezi October 2020.

Tundu Lissu amepitishwa na CHADEMA kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho. Lissu amenukuliwa akisema ataingiza Watanzania barabarani ikiwa ataibiwa kura zake.

My Take: Ni mapema sana kwa Mgombea wa Urais kutoa kauli kama hii si kiashiria kizuri. Anataka kutuaminisha kuwa hata ikitokea ameshindwa kihalali tuamini kuwa kaibiwa kura ili atimize azima yake.

Uongozi wa CHADEMA umshauri huyu mgombea kauli hizi hazifai kwa usalama wa nchi yetu.
Naona siku hizi mataga mmeanza kuwa waungwana, sijasikia mkikemea Yule aliyesema" nikupe mshahara alafu umtangaze mpinzani mshindi"
 
Hapo mbona bado sana ngoja muda wa campaign aanze kuongelea mambo ya kuvunja muungano, kumwita Nyerere mtu wa ovyo na hadithi yake isiyoisha ya risasi kumi 16.

Jamaa ni narcissist he rates himself so highly wenzake wanaenda kwenye campaign kwa porojo za watawafanyia nini wananchi, yeye anakwenda na agenda ambayo anaifahamu mwenyewe.

Yaani kichwani kwake keshaanza kuchagua rangi ya pazia atazoweka Ikulu; ni swala la muda kabla ya watu kukubali huyu mtu anahitaji psychological intervention ajatulia bado kutokana na mkasa uliompata na wala hana sifa za high office.
Huyu ndo tunamtaka mzalendo wa kweli npigania haki za wanyonge historia inambeba tangu enzi hizo, wakati Yule uchwara akiwa analamba viatu vya watawala ili ashibe
 
Kwa siasa za Magufuli Lisu ndio saizi yake.
Mkuu trust me, kwa aina ya siasa za Lissu itakuwa more worse. Kidogo siasa zitachangamka lakini kama hawatampa timu nzuri inayomjua madhaifu yake wamshauri tena wasiomuogopa inaweza kuwa disaster achana watu kujipa moyo humu.

Kama umesikiliza hotuba zake toka afike utaona madhaifu makubwa kisiasa, naona wengi wanaleta tu ushabiki na ufuasi lakini uongozi wa Chadema wasicheze tune za wafuasi wao ambao walimpigia deki hadi Lowasa na kuzungurusha mikono na hawakusikia tuliyowaonya.

Wamstadi mgombea wao madhaifu yake na kumpa timu makini kumdhibiti aache mihemko apangilie maneno yake vizuri maana huko site sio uwanja wa mahakama.

JPM tayari ana rekodi kupitia awamu yake ya kwanza na huko site kazi yake imekubalika sana tofauti na mbwembwe za huku mitandaoni. Lissu ana kazi kubwa kuonesha kwanini awe mbadala na aweze kufuta dhana za kutafuta huruma kupitia shambulio lake.

Lakini tusisahau pia kama Membe hatoungana na Lissu litakuwa pigo kubwa zaidi kwa upinzani maana tegemea massive campaign kutoka kwake pia na itawagawa. Sioni dalili Zitto kukubali terms za Chadema bila 50/50 ratio kwenye mazingira ya sasa ambayo kuna kila dalili ACT kuwa main opposition.

Hii kufungua nyuzi kibao humu na kujifariji kuwa upepo umebadilika wataumia na kurudi kwa aibu kubwa baada ya October, kura zipo huko ground sio mitandaoni wanakojaza kelele utafikiri zitageuka kura.
 
Mkuu trust me, kwa aina ya siasa za Lissu itakuwa more worse. Kidogo siasa zitachangamka lakini kama hawatampa timu nzuri inayomjua madhaifu yake wamshauri tena wasiomuogopa inaweza kuwa disaster achana watu kujipa moyo humu.

Kama umesikiliza hotuba zake toka afike utaona madhaifu makubwa kisiasa, naona wengi wanaleta tu ushabiki na ufuasi lakini uongozi wa Chadema wasicheze tune za wafuasi wao ambao walimpigia deki hadi Lowasa na kuzungurusha mikono na hawakusikia tuliyowaonya.

Wamstadi mgombea wao madhaifu yake na kumpa timu makini kumdhibiti aache mihemko apangilie maneno yake vizuri maana huko site sio uwanja wa mahakama.

JPM tayari ana rekodi kupitia awamu yake ya kwanza na huko site kazi yake imekubalika sana tofauti na mbwembwe za huku mitandaoni. Lissu ana kazi kubwa kuonesha kwanini awe mbadala na aweze kufuta dhana za kutafuta huruma kupitia shambulio lake.

Lakini tusisahau pia kama Membe hatoungana na Lissu litakuwa pigo kubwa zaidi kwa upinzani.

Hii kufungua nyuzi kibao humu na kujifariji kuwa upepo umebadilika wataumia na kurudi kwa aibu kubwa baada ya October, kura zipo huko ground sio mitandaoni wanakojaza kelele utafikiri zitageuka kura.
Kuna wakati akili zinakurudia
 
Hiyo ndio Kauli ya Tundu Lissu iwapo ikitokea ameshindwa kwenye Uchaguzi Mkuu mwezi October 2020.

Tundu Lissu amepitishwa na CHADEMA kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho. Lissu amenukuliwa akisema ataingiza Watanzania barabarani ikiwa ataibiwa kura zake.

My Take: Ni mapema sana kwa Mgombea wa Urais kutoa kauli kama hii si kiashiria kizuri. Anataka kutuaminisha kuwa hata ikitokea ameshindwa kihalali tuamini kuwa kaibiwa kura ili atimize azima yake.

Uongozi wa CHADEMA umshauri huyu mgombea kauli hizi hazifai kwa usalama wa nchi yetu.
Kwa hiyo mkuu unataka hata kama ameibiwa kura akae kimya tu?
 
Kauli hatari kwa usalama wa nchi au kwa viongozi walio madarakani?
Busara ya fisiemu inakuaga juu sana wkt kama huu hasa wakiona upepo unaelekea kuwakataa,sijui mtapiga tena push up safari hii.Nakumbusha tu miongoni mwa ahadi hewa mlizotupa 2015 ni laptop kwa kila mwalimu nchi nzima,milioni hamsini kila kijiji bado tunasubiri wiki zilizobaki nafikiri zitatosha kutekeleza ahadi zenu.
Usalama ni kwa ajili ya watu wote,haijalishi ni kiongozi au yeyote kichaa.
Tatizo tunashindwa kutofautisha maslahi ya nchi na yale ya mtu au kakikundi ka watu /vyama vya siasa.
Siku zote waoga ndio wenye busara kuliko majasiri wapumbavu.
Na kama itatokea jasiri ni mwenye hekima basi ujue roho wa malaika wa mbingu yu karibu naye.
 
Aanze yeye na mke wake kuingia barabarani wamalizie kazi. Anajua kabisa hawezi kushinda
Wale walioenda kumpokea na kufunga road na kusimamisha Dar kwa muda ndo hao watakaoenda mtaaani
 
Tundu Lissu ni miongoni mwa nembo za taifa na tunu zinazopaswa kulindwa alichozungumza leo sitashangaa hata CCM wenyewe kumpigia kura 28 October 20 nimepata nguvu ya kwenda kupiga kura.

#NI YEYE
 
Tundu Lissu ni miongoni mwa nembo za taifa na tunu zinazopaswa kulindwa alichozungumza leo sitashangaa hata CCM wenyewe kumpigia kura 28 October 20 nimepata nguvu ya kwenda kupiga kura.

#NI YEYE
Hata mimi, nilisha give up kupiga kura tena. Lakini sasa nipo tayar kusimama kwenye foleni.
 
Back
Top Bottom