Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Niko tayari kugombea Urais mwaka 2020 nikipewa ridhaa na Upinzani

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Niko tayari kugombea Urais mwaka 2020 nikipewa ridhaa na Upinzani

Mwaka 2013 Zitto alitangaza nia ya kugombea urais 2015 chama kikampa onyo kali na baadaye kikamfukuza kwa kuonesha nia nje ya utaratibu wa chama!

Huyu naye sijui kama atasalimika! Na vile mmiliki halali wa chama bado ana nia. Ngoja tuone.
 
Nazani safari hii Chadema wanasahihisha makosa yao.

Tuliwashauri kuwa unapokutana na mchina usiongee kiswahili wakati yeye anatema kichina, hamtoelewana.

Kuingia kwenye uchaguzi wakati mpinzani wako ndiye mmiliki wa tume pamoja na vyombo vya ulinzi alafu unategemea kushinda na kutangwaza mshindi, da! Huko ni kuota ndoto za mchana tena ukiwa unaogelea ndani ya swimming pool

Ndio, unapokutana na mchina wote walima muongee lugha moja ndipo mtaoelewana.
Kama wao wanamiliki vikosi vya ulinzi na nyie milikini vya kwenu, ( Rejea maamuzi ya binge la Ulaya "TUTATOA MSAADA/ULINZI WOWOTE UTAKAO HITAJIKA KWA WAPIGANIA HAKI, WANAHARAKATI" )
Hiyo in fursa adimu wakati sahihi.

Kama wao wanamiliki tume ya uchaguzi basis na ninyi milikini ya kwenu, Rejea tamko la USA kupiti waziri wa mambo ya nje "2020 in lazima tusimamie/kuakikisha uchaguzi huru na wahaki unafanyika"
Hapo jecha atakimbia.

Toka vyama vingi vianzishwe hakuna kipindi kizuri kwa wapinzani kama 2020 na hii ni kwasababu:-
1: Serekali ya awamu ya tano imefeli kwenye mambo ya kidiplomasia
2:Watumishi wengi wa uma na sekta binafsi wanalia hali ngumu na hawaoni matumaini
3: Ccm imewazarau wakongwe wao na kuwapa nafasi watu wasiokijua chama.
4:Watu wamenyimwa juongea na vifuwa vyao vimejaa na watakapopata nafasi lazima waongee kwa ngumi,mateke nk.
5:..........
6:...........
7;...........

NB😀hahabu iliyosafi ni lazima ipite kwenye tanuru la mito ndipo itang'aa. Taifa lazima litikisike ili likitulia tuwe na historia sahihi itakayotuongoza mbele na kuwafanya viongozi kujua nini gharama halisi ya uonevu.

Kwenye ufahamu na aelewe....
kufeli kidiplomasia,kwani wapiga kura ni mabwana zenu wazungu?Lowassa,Sumaye ni wakongwe Chadema?
 
taahira ambaye tangu 1995 unaamini upinzani utashika nchi?

bado na hali ya sasa ya kisiasa na hali ya wapinzani utegemee Lissu kuwa rais? bora kuwa taahira basi ..ha ha

..gazeti limeandika ili kuuza habari.

..soma vizuri kwenye maandishi madogo chini ya kichwa cha habari ktk makals ya gazeti iliyokuwa-posted, Lissu amesema ikiwa vikao vitaamua atagombea.

..kauli hiyo ni tofauti na wale wanaotamka kuwa wanagombea, au wanaochukua fomu za maombi ya kugombea Uraisi.
 
Zitto ana mapungufu yake lakini namuona ni mzuri kias chake kwenye uongozi kuliko ata mpiga kelele Lissu! Lissu ni mpiga kelele tu lakini mweupe sana japo kwa wote simuoni wa kumshindanisha na Magufuli
Wewe mwenyewe ni admirer wa lissu. Taarifa tunazo.
 
..gazeti limeandika ili kuuza habari.

..soma vizuri kwenye maandishi madogo chini ya kichwa cha habari ktk makals ya gazeti iliyokuwa-posted, Lissu amesema ikiwa vikao vitaamua atagombea.

..kauli hiyo ni tofauti na wale wanaotamka kuwa wanagombea, au wanaochukua fomu za maombi ya kugombea Uraisi.

mwananchi wameishiwa kumbe

Lissu ni potential, ila sio muda wake huu

2025 can work better for him kama akiruhusiwa na kama wakianza siasa za mvuto na kuwa karibu na raia
 
Huyu jamaa domokaya kweli kweli. Haoni risk ya kugombana na Mwenyekiti wa chama chake aliyejiandaa tangu 2010? Asisahau kuwa kuna Lowasa, Sumaye na Membe pia wanasubiri kipenga. Tuwasubiri wamalizane.
 
kufeli kidiplomasia,kwani wapiga kura ni mabwana zenu wazungu?Lowassa,Sumaye ni wakongwe Chadema?
Mkuu heshima kwako.
Raid lazima apikwe na kuiva, awe ni mtu mwenye uwezo wa kuzicheza siasa za ndani na kimataifa, zaidi za kimataifa.

Kosa la ccm ni kutomwandaa Magu,waliangalia upepo unavyovuma na kufanya maamuzi bila kujua upepo utatulia na mambo yatatakiwa kusonga mbele.

Nchi ka USA inapompata Raid anayesuasua kwenye siasa za kimataifa wanamwondoa. Sasa kama taiga Kubwa linajua umuhimu wa saiasa za kimataifa sembuse sisi tunaochechemea!?

Sikukuu njema
 
Hawezi kushinda urais, wapiganie tume ya uchaguzi iwe huru kwanza
 
unanikumbusha mwanamke akizaa watoto wawili, wakati anazaa anajiapiza hazai tena!..ghafla mimba

hivi kwa TZ hii, tume hii, upinzani huu na record za JPM za barabara kila kona, Lissu anamtisha nani??

kama EL alifikia pale, record yake haiji kuvunjwa miaka ya karibuni
Heeee! Barabara peke yake ndiyo zinabeba maisha yote ya wananchi!!!! Ama kweli upande ule vichwa pombe!
 
Mkuu heshima kwako.
Raid lazima apikwe na kuiva, awe ni mtu mwenye uwezo wa kuzicheza siasa za ndani na kimataifa, zaidi za kimataifa.

Kosa la ccm ni kutomwandaa Magu,waliangalia upepo unavyovuma na kufanya maamuzi bila kujua upepo utatulia na mambo yatatakiwa kusonga mbele.

Nchi ka USA inapompata Raid anayesuasua kwenye siasa za kimataifa wanamwondoa. Sasa kama taiga Kubwa linajua umuhimu wa saiasa za kimataifa sembuse sisi tunaochechemea!?

Sikukuu njema
Hujui kuandika,rudi shule kwanza.
 
Bavicha hawaelew saiz waende na Membe au Lisu. Hahahah hawa wafuasi wana LAANA sio bure.
 
Back
Top Bottom