Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Niko tayari kugombea Urais mwaka 2020 nikipewa ridhaa na Upinzani

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Niko tayari kugombea Urais mwaka 2020 nikipewa ridhaa na Upinzani

Zitto hawezi kukubali atatumia 2020 kujitangaza kwa 2025
naona upinzani unaweza kuchukua Nchi kama watafanya mambo kadhaa.
haya nitayasema siku nikionana na Mbowe.
lakini ki uhalisia kwa hali ya sasa Upinzani kuchukua Nchi ni bado Sanaa na mapema mnoo..
Binafsi sipendi lakini na UHAKIKA 2020-2025 Ni Magufuli tena
swala la Nani atagombea upinzani
hilo bado ni confidential lakini kwa Lowassa hapana yule kashapoteza tenaa
namuona Mbowe&Lissu
lakini wote naona bado wana pwaya
 
Ndio maana kuna wapiga kampeni ambao wanawasaidia hao wapiga kura kuchagua kilicho bora
Mkuu, hizo facts ulizoandika hazielezei ubora wa mtu kama kiongozi wa kitaifa ama la. Hizo facts ziko very shallow kulingana na context nzima ya cheo kama cha Uraisi. Raisi bora anapaswa afanye nini, then hayo anayopaswa kuyafanya yalitakiwa yalinganishwe na uwezo wa TAL akipimwa kwa vigezo vya uongozi wake katika siasa na TLS. Mambo uliyoandika ni vijembe vya kwenye taarabu na kwa wasomaji makini tunaona una expose your ignorance
 
Naona kama huu uzi unahujumiwa ahahahaha. Huyu mtu amechafua hali ya hewa. Kiukweli napenda kusema Lissu ni very smart person. Ana akili ya ziada. Sizungumzii mambo ya kukariri hapa nimefuatilia mijadala yake mingi na hoja zake hakika sina shaka na akili yake.
 
Namshaaga sana lisu anamuogopa mbowe kuliko raisi wa jamhuri, bila shaka mbowe ni mtu hatari sana. Sasa kama anamuogopa na kumyenyekea mbowe kiasi hiko, ataweza uraisi kweli, jibu ni no, aanzie kwanza umwenyekiti chadema then akitoboa ndo tuone

Magufuli alikuwa kwanza mwenyekiti wa ccm ndio akawa rais?
 
Kwasababu NI mwanasheria mbobezi wa haki za binadamu plus fatma karume ushoga.
 
Mbona wewe unamshauri Rais wa CCM na CCM?

Sio mbaya ndio uhuru wa maoni kwenye post yako namba moja. Ila kwa taarifa yako kuwa rais wa Tanzania kunahitaji tu kuwa na akili timamu. Hiyo ndio sifa pekee yenye kubeba asilimia 90. Hizo asilimia 10 ndio sifa nyinginezo. Kwenye nchi ambayo rais hashitakiwi kwa kosa lolote afanyalo akiwa madarakani ni sifa gani kubwa ya muhimu zaidi ya akili timamu?
 
Yaani Lissu ndo asitoshe na Magufuli unaona anatosha,,??. Hii nchi kama mafufuli amekua Rais na watu wanaona sawa Hata ukimpa Hamisa Mobeto atamudu tu ,,,
 
KUMEKUCHAAAA TUNDU LISSU ATANGAZA KUANZA HARAKATI ZA KUGOMBEA URAIS 2020

BY Mwanakijiji Lugusi

Ifikapo Mwaka 2020, Chama hiki cha Mababu zetu, kitakuwa kimekata pumzi Kabisa, kiasi kwamba Mgombea yeyote wa upinzani akiandaliwa vizuri na mapema, njia ni nyeupe State House. Huyu Tundu Lisu anao uelewa mkubwa, Siyo mla Rushwa, ni Very Strong leader, hafanani na Dr Slaa, Lipumba,Zito na wengine wa Namna hiyo. Nina Imani huyu Lisu angekuwa mla Rushwa CCM wangeshampa kiasi chochote anachotaka. Na wanajua ktk Chama hiki kikuu cha Upinzani, ukimtoa Lisu Na mbowe, chama kimekwenda na Maji.

KWANINI UMAARUFU WA CHADEMA ULISHUKA GHAFLA BAADA YA 2015?

Mwaka 2015 Chama cha Demokorasia na Maendeleo( CDM) kilikuwa ktk kilele chake cha mafanikio. Kama si technical error's walizofanya mwishoni kabisa, kushindwa kumuelewa mwenye ngoma waliyokuwa wakiicheza kwa mda mrefu ,uzoefu wa CCM, CCM kuwa chama Dola na mambo kadhaa ya kikatiba kuhusu uchaguzi ambayo hayajakaa sawa, basi CDM chini ya mwamvuli wa UKAWA walikuwa wanatinga magogoni!

Moja ya dalili ya kushuka kwa chama chetu ni UKUTA. Ililetwa bila kifikiria madhara yake kwa watu wengi. Wengi wameona CDM yetu kama kakikundi cha waasi ndani ya nchi.

Kibaya zaidi ni kule kuahirisha kumefanya watu wengi kuwa hawajiamini. Siku nyingine watu wataona; ni walewale wa kila siku. Hivyo mambo yao hayatapata mwitikio wa kutosha

KUHUSU LOWASA KUGOMBEA 2020

1) UMRI.
Lowassa hana mvuto sijui ni afya au umri wapigakura wengi hawamwoni mkakamavu wa kuyafanya yale MAAMUZI MAGUMU ambayo amekuwa akihimiza yafanyike.

Ikumbukwe katika uchaguzi wa 2020, karibu 70% watakuwa vijana kwa maana ya umri wa kuanzia 18-55

Magufuli naye anaonekana ni habari ya jana. Anajaribu aonekane ni kijana lakini kitaswira na matendo hana mvuto. Teuzi zake nyingi zinabagua na kuwanyanyapaa vijana na kama kateua vijana ni kuzijenga familia za wanasiasa awaonao ni jembe kwake kisiasa.
FB_IMG_1545888308117.jpeg
 
Namshaaga sana lisu anamuogopa mbowe kuliko raisi wa jamhuri, bila shaka mbowe ni mtu hatari sana. Sasa kama anamuogopa na kumyenyekea mbowe kiasi hiko, ataweza uraisi kweli, jibu ni no, aanzie kwanza umwenyekiti chadema then akitoboa ndo tuone
Kwani Jiwe alianzia uenyekiti CCM?
 
Lissu anawapa taabu eeeh!!
Hata Daudi alimpa taabu sana mfalme Saul hata akatamani kuumtoa roho na akashindwa.
Sasa mmemtandika risasi Lissu na hajafa 😁😁
Mungu sio JPM endeleeni na mchakato wenu but Lissu is the next chosen president of URT
 
TANGAZO:
Kesho tarehe 24/10/2020 kutakuwa na mdahalo wa kitaifa wa kufunga kampeni katika ukumbi wa Nkurumah;
Wagombea wanaotarajiwa kuhudhuria;
J.P. Magufuli - CCM
T.A. Lissu - CHADEMA
H.R. Sipunda - CHAUMA
Z.R. Kabwe - ACT Wazalendo
NYOTE MNAKARIBISHWA.
Hawa wawili wa chini waondoe wawe Tim ya lissu ili kuunganisha nguvu ya kuvunja jiwe.
 
Miongoni wa sababu, eti hawezi kukaa kwenye kikao dakika 20 bila kutoka nje..Jamani?
 
Ukitupa jiwe gizani mara ukasikia Yalaa, ujue kunamtu kapigwa. Sasa nimeamini Membe na Lissu wanawakosesha usingizi maccm.
 
Kwamujibu wa katiba yetu Lisu amekidhi vigezo.wanao amua nani awe Raisi ni wspiga kura.sio wwewe mwendawazimu
 
Wewe tulishakufukuza cdm kwa sababu ya wizi alafu unaifuatafuata cdm sababu gani?
Nimesoma habari ya gazeti la Mwananchi kuhusu swala la Lissu kujiandaa na Urais 2020 hivyo kufanya idadi ya wagombea waliokwisha kutangaza nia ya kugombea Urais kwa tiketi ya Chadema kinyume kabisa na miongozo ya chama hicho kwa watia nia wake kuwa wawili mpaka sasa yaani Lissu na Lowassa.

Miongozo ya CHADEMA inawataka watia nia wa Urais kutangaza nia hiyo mwaka mmoja kabla ya Uchaguzi mkuu ili kuepusha mpasuko ndani ya Chama. Aidha yuko Mbowe nae anataka kugombea Urais ila hatangazi ili apate nafasi ya kuwaengua wanaotangaza mapema wakati ukifika.

Kwa tunaomjua Lissu tunaamini kabisa kuwa hawezi kuwa kwenye nafasi kubwa kama Urais kwa sababu kubwa kuwa hayuko settled. Lissu anapaswa kuwa na chombo au mtu wa juu yake kumdhibiti. Lissu ni kama Lema, Wenje na sampuli hizo. Ni waongeaji, wakosoaji na wakitumwa kusemea jambo wana uwezo mkubwa wa kufanya.

Udhaifu wao mkubwa ni kwamba hawawezi kukaa kwenye kikao dakika 20 bila kutoka nje. Wako mbio mbio muda wote. Hawana ubunifu wao ni watekelezaji tu, ni watu wa visasi na makundi, wamekubuhu kwenye fitina hawa wote ndio walimpoteza Lytonga Mrema kwa kumgombanisha na wenzake akina Marando sasa wameshamgombanisha Mbowe na waliokuwa wapenzi wake akina Zitto, Dr. Slaa sasa wanataka Urais.

Dhambi kubwa ya Zitto na Dr Slaa CHADEMA ilikuwa ni kutangaza kugombea Urais. Waliosimamia mkakati wa kuvunja ndoto zao ni hawa vijana wa Lytonga Mrema waliotoka nae NCCR kwenda TLP halafu wakamtelekeza kule na kukimbilia CHADEMA. Kwasababu ni wabaguzi dhambi ile hawajawahi kuiacha ni sawa na kula nyama ya mtu.

Mimi binafsi namuunga mkono Lissu kuwa mwenyekiti wa CHADEMA kwa sababu ndio pekee ninayemuona ana ujasiri wa kupambana na Mbowe japo hana mkakati. Simuungi mkono kwa sababu yeye atakuwa mwenyekiti mzuri kuliko Mbowe la hasha ila atavunja mwiko na kufungua mlango uliofungwa miaka mingi wa kupokezana vijiti ndani ya CHADEMA.

Aidha Lissu atatoa changamoto kwa siasa za upinzani nchini na kuzinogesha. Nampa tahadhari Lissu kuwa kama amesharubuniwa na Mbowe kuwa ataachiwa Urais na yeye aachie uenyekiti ameshashindwa kabla ya kuanza.

Kwa sasa Lissu focus kwenye Uenyekiti wa CHADEMA kwanza Urais unakuja tu wenyewe.

Nakutakia uponaji wa haraka Kamanda
 
Back
Top Bottom