Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Kesi ya uhaini inayomkabili mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu inaendelea Jumatatu Agosti 24 ambapo mshtakiwa anajitetea mbele ya mahakama.
Lissu: Ukiangalia miaka kabla ya 2020 tume imekuwa ikifanya hivyo. Lakini 2020 kuna matokeo ya urais hayakuchapishwa. Sina uhakika kama ya mwaka jana yalichapishwa maana nilikuwa gerezani.
Ni kweli kwamba kuna vitu vya ajabu sana. Sasa Mheshimiwa, majaji ukisoma taarifa za watazamaji wa uchaguzi wa kimataifa na wa Umoja Africa walisema kabisa hakukuwa na uchaguzi. Uchaguzi ulikuwa bandia.
Fuatilia mwenendo wa Kesi > Lissu: Tume ya Uchaguzi ni ya CCM na haifai katika mfumo wa Demokrasia wa Vyama Vingi
Ripoti ya tume ya uchaguzi mkuu 2020 alikabidhiwa rais Samia August 2021 na katika sherehe hizo rais alisema, wagombea wa upinzani tumewapiga vibaya, waangalizi wa kimataifa walisema bila mabadiliko ya kikatiba 2025 itakuwa maafa.
Magufuli kafa kaja Samia. Akasema hakuna haja ya mabadiliko ya katiba. Katiba haileti chakula mezani.
CHADEMA ikasema tunaanzisha kampeni ya kudai katiba mpya Mwenyekiti wetu akakamatwa na kufunguliwa kesi ya ugaidi kwa miezi nane.
Jana nimesikia jamaa (Mbowe) yupo kwenye uzinduzi wa bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere huko wakati mwenyekiti wake yupo Ukonga yeye yupo huko na mama.
"Nimesikia Mbowe yuko kwenye uzinduzi wa bwawa, wakati Mwenyekiti wake yuko Ukonga"
Soma: