Pre GE2025 Tundu Lissu: Ninakiri juu ya Dhambi ya kumleta Lowassa CHADEMA. Watanzania tumekusamehe, ubarikiwe

Pre GE2025 Tundu Lissu: Ninakiri juu ya Dhambi ya kumleta Lowassa CHADEMA. Watanzania tumekusamehe, ubarikiwe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Lissu ni Muungwana na mkweli uliopitiliza. Tazama kwa sasa Dr.Slaa anamuunga mkono Lissu na hivi sasa yuko ndani kwa ajili ya Lissu. Lakini bado ilipokuja swala la Dr. Slaa kukana kuhusika kwake kumleta Lowassa,Lissu amesema kweupe kuwa Slaa katika hilo si mkweli kwakuwa alihusika.

Wangelikua wanasiasa wengine kwakuwa kwa sasa Dr. Slaa yuko upande wake angempaka mafuta.
 
Dr Slaa kama katibu mkuu ni LAZIMA angeshiriki.

Kwa kuwa Lissu amekiri dhambi hiyo, Dr Slaa Hana kosa pia.

Arejeshwe CHADEMA haraka.
 
Hellow Tanganyika!!

Akihojiwa kuhusu ushirika wake kumleta chamani Lowwassa, amedai ,Yeye na Mnyika walipewa taarifa juu ya ujio wa Lowassa mwishoni kabisa, hivyo wasingekataa,

Alipoulizwa kwanini binafsi hakujiondoa kama Dr Slaa, amedai kuwa Dr Slaa alishiriki mchakato mzima wa kumleta Lowwassa mwanzo mwisho kama katibu mkuu,

Alipoulizwa kwanini hakuondoka CDM, amedai kuwa Hiyo ni dhambi na kukiri dhambi ni jambo la kheri.

Nachukua fursa hii kumsamehe TUNDU Lissu, na rasmi nampa nafasi ya kuongoza chama na Nchi ikimpendeza Mungu maana ni mkweli.

Abarikiwe TUNDU Antipas Lissu.

Mungu ibariki CHADEMA.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA.

Karibuni 🙏

Source: Mdahalo wa wagombea nafasi ya Mwenyekiti Taifa CHADEMA, star Tv.
Lisu hafai kuwa kiongozi kadanganya mengi sana
 
Back
Top Bottom