Pre GE2025 Tundu Lissu: Ninakiri juu ya Dhambi ya kumleta Lowassa CHADEMA. Watanzania tumekusamehe, ubarikiwe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
operanews1692097375458-360x330.jpg

FREE DR.SLAA
 
Hellow Tanganyika!!

Akihojiwa kuhusu ushirika wake kumleta chamani Lowwassa, amedai ,Yeye na Mnyika walipewa taarifa juu ya ujio wa Lowassa mwishoni kabisa, hivyo wasingekataa,

Alipoulizwa kwanini binafsi hakujiondoa kama Dr Slaa, amedai kuwa Dr Slaa alishiriki mchakato mzima wa kumleta Lowwassa mwanzo mwisho kama katibu mkuu,

Alipoulizwa kwanini hakuondoka CHADEMA, amedai kuwa Hiyo ni dhambi na kukiri dhambi ni jambo la kheri.

Nachukua fursa hii kumsamehe TUNDU Lissu, na rasmi nampa nafasi ya kuongoza chama na Nchi ikimpendeza Mungu maana ni mkweli.

Abarikiwe TUNDU Antipas Lissu.

Mungu ibariki CHADEMA.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA.

Karibuni 🙏

Source: Mdahalo wa wagombea nafasi ya Mwenyekiti Taifa CHADEMA, star Tv.
Mtu mkweli hukiri kosa na kusamehewa
 
Ina maana mpaka aulizwe ndio akiri? Toka 2015 hakukiri tapeli mkubwa Lisu

Asingeulizwa angeendelea kujifanya mtakatifu
Mtu akishakiri kosa, hahesabiwi dhambi.

Tumemsamehe na tunamuunga mkono.
 
Mtu akishakiri kosa, hahesabiwi dhambi.

Tumemsamehe na tunamuunga mkono.
Pumbavu zake vyama vya siasa ,serikali na mahakama havina dini

Yaani miaka 10 toka amefanya huo ujinga hakuomba msamaha leo sababu anagombea ndio anajitia kuomba msamaha tena baada ya kuulizwa huyo tapeli mkubwa wa kisiasa

Awatapeli huko huko Chadema wasiojielewa

Chadema sio kanisa wala msikiti wa kuungama dhambi tapeli huyo

Asante mwandishi wa habari kumbana barabara
 
Kama katibu mkuu ilikuwa BUSARA kumaliza mchakato ndipo ajiuzulu kama alivyofanya Dr Slaa.

Kama ambavyo Lissu amekiri kukosea kumleta Lowwassa na wao yaani yeye na Mnyika hawakuafiki.

Hadi hapo,

Lissu na Slaa Wana makosa. Hivyo Kwa kuwa ametubu,

Tumemsamehe Lissu na kuomba Slaa arejeshwe CDM sababu Hana kosa.
 
Lissu: Mimi Nina kabba, na friji LANGU linagandisha, Kuna mambo nikiyasema hapa, watu watakimbia Nchi.
Tundu Lissu hatanii eti...

Bila shaka kuna mambo makubwa, ya ajabu na mabaya sana yanamwandama Mwenyekiti Freeman Mbowe...

Hii kauli ya "Kuna mambo nikisema hapa, watu watakimbiana mchana kweupe. Lakini kwa kuwa mimi Nina Koo na friji langu linagandisha siwezi kuyasema hapa" Inatoa ujumbe mkubwa sana...

Na pengine ndiyo maana watu wamejitokeza ghafla na kuamua kuwa "Sasa huyu Mwenyekiti ni lazima iwe basi, lazima atoke na kukiacha chama...!!"
 
Mimi siku Ile Mbowe alipopanda furahisha akiwa amelewa na kusema CCM hoyeee!!

Nilinotice jambo kubwa behind the scenes!

Lissu ameweza kurudisha tena Imani ya watz Kwa CDM!
 
Hellow Tanganyika!!

Akihojiwa kuhusu ushirika wake kumleta chamani Lowwassa, amedai ,Yeye na Mnyika walipewa taarifa juu ya ujio wa Lowassa mwishoni kabisa, hivyo wasingekataa,

Alipoulizwa kwanini binafsi hakujiondoa kama Dr Slaa, amedai kuwa Dr Slaa alishiriki mchakato mzima wa kumleta Lowwassa mwanzo mwisho kama katibu mkuu,

Alipoulizwa kwanini hakuondoka CHADEMA, amedai kuwa Hiyo ni dhambi na kukiri dhambi ni jambo la kheri.

Nachukua fursa hii kumsamehe TUNDU Lissu, na rasmi nampa nafasi ya kuongoza chama na Nchi ikimpendeza Mungu maana ni mkweli.

Abarikiwe TUNDU Antipas Lissu.

Mungu ibariki CHADEMA.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA.

Karibuni 🙏

Source: Mdahalo wa wagombea nafasi ya Mwenyekiti Taifa CHADEMA, star Tv.

Kama kuna Mwanachadema anakataa faida ya Lowassa kuja CDM 2015 huyo atakuwa Punguani.

Ujio wa ENL umekiongezee ruzukua CDM maradufu.

Umekiongezea wanachama na wabunge.

Kwahiyo ENL kuja CDM siyo dhambi , ni kama Lema na Msigwa walivyotoka TLP na kuja CDM au Lissu Kutoka NCCR kuja CDM an Dr Slaa kutoka CCM kuja CDM na kutoka CDM kwenda CCM.
 
Ikiwa Lowwassa alikuja na pesa chafu, zikasaidia kupata ruzuku kubwa na wabunge wengi na kununua wapiga kura,

Basi yote hayo ni ubatili.

Tugange yajayo.
 
Mimi siku Ile Mbowe alipopanda furahisha akiwa amelewa na kusema CCM hoyeee!!
Hii video clip akisema "CCM OYEEE" huko Mwanza hebu itafutwe popote ilipo tuwakumbushe Chawa wake ili waanze kumtetea na kujitetea haraka...
 
Ikiwa Lowwassa alikuja na pesa chafu, zikasaidia kupata ruzuku kubwa na wabunge wengi na kununua wapiga kura,

Basi yote hayo ni ubatili.

Tugange yajayo.
Unajua bajeti ya Kugombea Urais au Ubunge ambayo msajili amepitisha?(Gharama za kampeni).
 
Back
Top Bottom