Pre GE2025 Tundu Lissu: Ninakiri juu ya Dhambi ya kumleta Lowassa CHADEMA. Watanzania tumekusamehe, ubarikiwe

Pre GE2025 Tundu Lissu: Ninakiri juu ya Dhambi ya kumleta Lowassa CHADEMA. Watanzania tumekusamehe, ubarikiwe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Momentum of Lowasa ndio iliwapa ubunge hata wasiostahili kuwa wabunge na madiwani kibao, ni ndoto kwa Chadema sasa hivi kupata kura millioni 8 za Urais hasa kwa huu utoto walioleta hata mimi siwapigii tena kura.
Mashabiki na wafuasi wengi wa Chadema hawapendi sana kukiri hili kuwa 'upepo wa Lowassa uliwafaidisha mno mwaka 2015'

Ila kutwa ni kulalama tu kuhusu ujio wake.

Rabbon Tindo JokaKuu zitto junior
 
Hellow Tanganyika!!

Akihojiwa kuhusu ushirika wake kumleta chamani Lowwassa, amedai ,Yeye na Mnyika walipewa taarifa juu ya ujio wa Lowassa mwishoni kabisa, hivyo wasingekataa,

Alipoulizwa kwanini binafsi hakujiondoa kama Dr Slaa, amedai kuwa Dr Slaa alishiriki mchakato mzima wa kumleta Lowwassa mwanzo mwisho kama katibu mkuu,

Alipoulizwa kwanini hakuondoka CHADEMA, amedai kuwa Hiyo ni dhambi na kukiri dhambi ni jambo la kheri.

Nachukua fursa hii kumsamehe TUNDU Lissu, na rasmi nampa nafasi ya kuongoza chama na Nchi ikimpendeza Mungu maana ni mkweli.

Abarikiwe TUNDU Antipas Lissu.

Mungu ibariki CHADEMA.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA.

Karibuni 🙏

Source: Mdahalo wa wagombea nafasi ya Mwenyekiti Taifa CHADEMA, star Tv.
Tundu Lissu ni Muungwana sana.
 
Kitendo cha Mbowe kushindwa kuhudhuria mdahalo kinamfanya siwe right person kuongoza chama, amekuwa na tabia za Maccm, ameshachoka na hafai tena. Simkubali Lissu kwa sababu kadhaa, na sioni kama anafaa kuongoza chama, ila I give him benefit of the doubt.

Huwezi kukimbia mdahalo kama kina Samia, Magufuli, Kikwete nk halafu unataka kupewa nafasi, tutajuaje kama bado unafaa?
 
Momentum of Lowasa ndio iliwapa ubunge hata wasiostahili kuwa wabunge na madiwani kibao, ni ndoto kwa Chadema sasa hivi kupata kura millioni 8 za Urais hasa kwa huu utoto walioleta hata mimi siwapigii tena kura.
Lumumba fc na wewe uliwapa kura?😀😀
 
Momentum of Lowasa ndio iliwapa ubunge hata wasiostahili kuwa wabunge na madiwani kibao, ni ndoto kwa Chadema sasa hivi kupata kura millioni 8 za Urais hasa kwa huu utoto walioleta hata mimi siwapigii tena kura.
Cdm hawahitaji kura yako. Lowassa kura alizikuta cdm acheni kutaka kumpa sifa asiyostahili. Kama aliweza kuwapa kura hizo 6m+ akiwa na miezi miwili, aliwapa viti ngapi akiwa na miaka miwili? Yeye Lowassa alitakiwa aje cdm na hao wabunge 50+ wa ccm, kitu ambacho alishindwa. Kwa sasa hivi hakuna uchaguzi tena, wanaweza vipi kupata kura 8m? Na kwa taarifa yako wala hakuna watu milioni 8 kwa sasa wanaojitokeza kupiga kura.
 
Cdm hawahitaji kura yako. Lowassa kura alizikuta cdm acheni kutaka kumpa sifa asiyostahili. Kama aliweza kuwapa kura hizo 6m+ akiwa na miezi miwili, aliwapa viti ngapi akiwa na miaka miwili? Yeye Lowassa alitakiwa aje cdm hao wabunge 50+ ccm, kitu ambacho alishindwa. Kwa sasa hivi hakuna uchaguzi tena, wanaweza vipi kupata kura 8m? Na kwa taarifa yako wala hakuna watu milioni 8 kwa sasa wanaojitokeza kupiga kura.
Baada ya ujambazi wa ccm na washirika wake. Kura zote zinazopigwa hazifiki Milioni 8.

😀😀😀
 
Mashabiki na wafuasi wengi wa Chadema hawapendi sana kukiri hili kuwa 'upepo wa Lowassa uliwafaidisha mno mwaka 2015'

Ila kutwa ni kulalama tu kuhusu ujio wake.

Rabbon Tindo JokaKuu zitto junior
Hii Si Kweli,

Lowassa angeenda basi Chauma kama alikuwa na upepo huo.

Ni lazima tukubali pia kuwa CHADEMA enzi zile ilikubalika sana na wananchi, Lowassa akaja kuongeza pia chachu ya kukubalika huko.
 
Dr Slaa angekuwa amemleta Lowassa CHADEMA angeweza vipi kukikimbia chama tena mbele ya waandishi wa habari?.
Ni lissu aliyetuhabarisha kwamba kabla ya kumpokea lowasa walifanya utafiti kuona nani anachagulika kati ya Slaa na lowasa, wakapata majibu kuwa lowasa ndiye anachagulika.

Kusema Slaa alimleta lowasa, lissu kadanganya.
 
Mnafiiki Lissu, kipindi Lowassa akiwa amehamia upinzani alikuwa asubuhi anaonekana akielekea ofisi kwake mara nyingi tu, leo anadhani watu hawana rekodi zake, keshamgeuka Lowassa na Dr Slaa.
 
Unapingana na Lissu kwamba haikuwa dhambi kumleta Lowwassa CHADEMA?

Lowassa alikuwa msafi?

Utajiri alitoa wapi?

Unaweza kutajirika Kwa mishahara wa waziri mkuu?
You don’t get the point. Unataja mishahara kama kipimo cha utajiri? Unafahamu “utajiri” wa Rais au Waziri wa Fedha au Waziri Mkuu hivi leo? Unafahamu utajiri wa JK?

Kama Unafahamu linganisha na mishahara, posho na privilege zao zote halafu uje utuambie nani kati yao sio fisadi; nani msafi kwa mtazamo huo.

Certainly, Lowassa hakuwa msafi. Lakini hakuwa “shetani” kwenye nchi inayoongozwa na mfumo wa kifisadi!

Dhambi? CHADEMA sio dhehebu la dini. Uliza kama ulikuwa MKAKATI MBOVU au SAHIHI wa kisiasa kumleta Lowassa agombee uRais wakati ule.

Leo hii Republicans wamemkumbatia Trump pamoja na kwamba ana mizigo ya kukosa maadili, hana ustaarabu, janja za kukwepa kodi, kudanganya na kutozingatia tunu za kihafidhina (conservative values). Lakini Ana mvuto mkubwa sana kwa wapiga kura wengi. Halafu uwaambie habari ya DHAMBI kuhusu mtu wao!
 
Conclusion ni kuwa,

. CHADEMA ilikuwa na nguvu kubwa tu kabla ya ujio wa Lowwassa.

.Lowassa aliingiza pesa zisojulikana vyanzo vyake ndani ya chama, pesa zikasaidia kuongeza watu na chachu ya ushindi.

. Wananchi hawakufurahishwa na ndimi mbili za viongozi wa CHADEMA kuhusu tuhuma za ufisadi wa Lowassa, hivyo baada ya kushindwa uchaguzi, wakapuuza na kususia harakati za kisiasa nchini.

.Jambo hili ndilo Lissu anajaribu kulitatua Kwa kukiri dhambi hiyo hadharani Ili kurudisha tena Imani ya wananchi Kwa CHADEMA.
 
Back
Top Bottom