Tundu Lissu: Ninampinga Magufuli hadharani. Sio mnafiki na sijahongwa

Tundu Lissu: Ninampinga Magufuli hadharani. Sio mnafiki na sijahongwa

Naona vijana wa Lumumba kama kawaida yenu mnajaa povu..... Acheni hisia nendeni kwa hoja. Mikataba mibovu ya madini ndo iliyotufikisha hapa, na ni mikataba hii hii iliyoingiwa na serikali hii hii ya CCM.

Kila nikikumbuka sakata la samaki na gharama tulizoamriwa kulipa, nakata tamaa kabisa. Mahakamani hatutakatiza. Hawa hawa tunaoshangilia leo, hukumu zikishatoka sijui tutajificha wapi! Katika hili, tuache ushabiki wa mazoea!!!
Ndo maana kuna tume ya pili ya sheria na uchumi, tusubiri tuone, hii style ya Tundu haitakaa isaidie taifa na yeye anajua. kusema ni kitu kingine na kutenda ni kitu kingine. mbona huko chadema wameshindwa kutenda wanayosema!
 
Lissu tangu lini ulikuwa mzalendo! Uzalendo wa kutetea fisadi lowasa, au uchumia tumbo upi anausema zaidi ya huu wa kupewa kitu kidogo kumsafisha mtu aliye mchafua kwa miaka 10. Lissuu wadanganye vipofu wa vabichaa
Tunaongelea madini unamleta Lowasa, mkuu umetuonyesha waz kabsa kwamba huna akili timamu na hyo ndyo sifa ya wana CCM
 
Jibu swali ukiteleza hutakiwi kuamka bila kujali umetelezeshwa na nini?
Naona umeanza kuja na Mifano mfu. Hisiyoendana na jambo husika. Kwahiyo kwenye hili ni nani alitelezeshwa na kwanini, na ni nani alimtelezesha?
 
Lissu tangu lini ulikuwa mzalendo! Uzalendo wa kutetea fisadi lowasa, au uchumia tumbo upi anausema zaidi ya huu wa kupewa kitu kidogo kumsafisha mtu aliye mchafua kwa miaka 10. Lissuu wadanganye vipofu wa vabichaa
Umemsikia Mtemi Chenge?
 
Acheni siasa katika mambo ya msingi kipind cha JK tulikua tunasema JK mpole hana maamuzi Leo kaja Mzee wa hapa kazi tu tena tunalaumu.sisi ni watu wa aina gani? ?
Sio ukali kama roboti tunataka ukali wa kufumua mikataba ya kinyonyaji sio timuatimua za kutafutia kick
 
Yeye anaweza kuwa chizi ila ujuaji wako utacost nchi yote kama ilivyo tanesco na mikataba nyingine. Siasa na mihemko yake isiwatoe kujua kuwa once you have penned down something ndo hivyo otherwise mipaka tuliyo nayo sasa iliyosigniwa 1884 tusingeiheshimu. Jiulize kwa nini??? Think, read, research then come back. Kwa nini hutumii maji ya Victoria kwa Irrigation wakati Misri inayatumia? Mbona hilo hupingi?
Kutotumia maji ya Ziwa Victoria, hii ni hoja nyingine mpya inayohitaji tafakuri jadidi . .
 
18622446_1126398777465538_2060351389369899505_n.jpg



Na mimi ni Mtanzania pia.

Tofauti kati yangu mimi na wewe na Magufuli ni hii: Mimi nimepigania nchi yangu katika masuala haya tangu mwaka '99.

Wakati huo tulikuwa na mgodi mmoja tu wa dhahabu, Resolute Golden Pride Nzega. Bulyanhulu ilikuwa haijajengwa. Geita ndio kwanza walikuwa wanafukuza wanakijiji wa Mtakuja.

Nadhani nilikuwa wa kwanza katika nchi hii kupiga yowe kwamba tutaibiwa sana kwenye sekta ya madini.

Wewe sijui ulikuwa wapi wakati huo. Najua Magufuli alikuwa wapi: upande wa MaCCM na wawekezaji hawa.

Nimepigana na wawekezaji hawa mahakamani, kwenye medani ya kisiasa ndani na nje ya nchi hii kwa zaidi ya miaka 15. Nimetetea wananchi completely free of charge Bulyanhulu, Tarime, Nzega, Geita, n.k.

Sijui wewe ulikuwa wapi lakini najua Magufuli alikuwa upande wa nani: wa MaCCM na wanyonyaji hawa.

Soma Rai ya tarehe 17 Julai, 2001, uone tulimwambia nini Mkapa siku anaenda kuzindua Mgodi wa Bulyanhulu.

Sijui ulikuwa wapi lakini najua Magufuli alikuwa wapi: alikuwa anatetea tumbo lake na matumbo ya wanyonyaji hawa.

Nilikamatwa na kushtakiwa kwa uchochezi kwa sababu ya Bulyanhulu. Hiyo ilikuwa December 2002. Nilikaa na kesi hiyo mahakamani Kisutu kwa miaka sita.

Sijui ulikuwa wapi ila najua Magufuli alikuwa wapi: upande wa watesi wa wananchi na wanyonyaji wa rasilmali zetu.

Leo Magufuli anajifanya mzalendo na anahoji uzalendo we yeyote anayepingana nae.

Ni muongo. Anatafuta umaarufu wa kisiasa kwa wasiojua na wasiokumbuka. Ataupata. Kwa siku chache tu. Mark my words: ataumbuka na mtaumbuka.

Mimi ninampinga hadharani. Sio mnafiki, na sijahongwa. Ninampinga kwa sababu atatusababishia matatizo makubwa zaidi kuliko tuliyonayo sasa.

Huo mchanga atauachia upelekwe ambako umepelekwa kwa miaka 16 iliyopita. Kama sheria ndiyo hiyo na mikataba ndiyo hiyo hana pakwenda.

Tatizo ninaloliona ni kwamba by the time anawarudishia mchanga wao, Tanzania itakuwa imekuwa a basket case kama Zimbabwe.

Na tutakuwa tumelipishwa mapesa mengi kama fidia na arbitral tribunals za kimataifa kwa kuvunja mikataba na wawekezaji hawa.

Kama kuna anayefikiri uzalendo ni kufumbia macho masuala haya basi huyo na amuunge mkono Magufuli kwenye upofu wake wa kujitakia.

Ripoti ya Prof. Mruma haitamaliza hata nusu saa under serious scrutiny. Zaidi ya majina ya maprofesa walioiandaa, ripoti hii haina credibility yoyote. Ni kazi ya kisiasa iliyopakwa rangi ya usomi.

Kama umefuatilia taarifa za kitaalamu za Bulyanhulu hata kabla ya Barrick Gold kuingia mwaka '99 utajua ninasema nini.

Sutton Resources, Outukumpu Oy na hata STAMICO walishafanya utafiti mkubwa juu ya utajiri wa Bulyanhulu. Taarifa zipo na zimekuwepo kwa hata mbumbumbu wa jiolojia ya madini kama mimi.

Hiki alichoambiwa Magufuli ni rubbish, hata kama ni ya kiprofesa. Rubbish. Hatuibiwi kwenye mchanga, that's the rubbish fed on the unlettered.

Tunaibiwa kwenye sheria. Kama hamuoni hilo then God have mercy on us.
Keep it up!
 
Huyu ndiye mpiganaji wa ukweli sio yule mwingine anayetafuta kick kwa kufukuza mawaziri huku akijua tatizo lipo kwenye mikataba
Mimi sijaelewa Kwani hoja ni sheria au hoja ni wizi kwenye taarifa wanazotoa,Lissu,Chenge na Werema wamejuaje kwamba tume wamedanganya kiasi kilichomo?hizi siasa zetu ni za hovyo sana
 
Tatizo la watanzania elimu ni ndogo sana ukisoma magazeti ukondiyo hovyo kabisa kila kinachosemwa na mkuu watu wanapiga makofi bila hata kufanya utafiti kidogo kuangalia ilo jambo linaukweli gani na athari zake ni zipi sitashangaa siku za usoni Tanzania kuwa kama zimbabwe
 
Tafiti hupingwa kwa tafiti siyo maneno ya kijiweni! Unafahamu maana ya neno rubbish? Hizi ni taaluma tijaribu kuziheshimu
naona umepanic,nimenukuu maneno ya lisu na brad...wanachotka acacia ni full report ili waone kama n sawa kwa wao kulipa hayo mabilioni kama yalivyopendekezwa na mruma na kamati yake..is that too much to ask for?
 
Kuyazuia makontena si ni adhabu hiyo?
Ikitokea kamati ikashauri ifuatwe njia ya kisheria huioni stepu tuliyobugi?
Kamati imeundwa imshauri. Ikimshauri aombe msamaha sawa. Hakuna kubugi kokote bali taifa litakuwa limeufunga mjadala wamakinikia na kuendelea na mengine kama taifa.
Kihelehele chenu cha kumuingilia ni upuuzi wa kupuuzwa kwa nguvu zote.
 
Back
Top Bottom