Tundu Lissu: Ninampinga Magufuli hadharani. Sio mnafiki na sijahongwa

Jibu swali usitoe vitisho, je Lissu kapima huo mchanga?
Ripoti yenyewe ishakosa uhalali haiaminiki tena
maneno matatu tuu ya accasia yametosha kuishushia hadhi iyo ripoti.
kwa nn tusingeunda kamati huru ichunguze ili kuondoa utata huu wa serkal kubishana na accasia?
 
Hiyo maana inayotokana na muktadha wanaoujua wazazi wako tu na kukufundisha wewe haunihusu.
Muktadha nilioutumia,neno hilo linawasilisha nilichokikusudia.
Umejisahau kuwa upo nje, umelizoea kwa muktadha wa vikao vya ccyemu vikao vya ndani.
 

Mkuu;
Kama nilimuelewa Tundu Lisu, nadhani hata yeye hakuwa na maana kuwa anataka tuu kuilaumu serekali ya ccm ila alitaka kutukumbusha aliyeileta hii kadhia na sasa aliyeileta anataka kutuongezea mzigo bila kutuandaa kuupokea.
Hata iweje, tusianze kuzozana. Hebu tupunguze munkari, tukae pamoja kama nchi/taifa. Tuseme, kwa kuwa sasa tumeamua kulitikisa dude, tusiliache tena litulie ila tulitikise kweli kweli hadi tufikie mahali pa kuondoa ujinga tuliofanya tulitikise hadi tung'oe hiyo mirija ya unyonyaji waliyo tufungia. Lisu, akalishwe na wenzake wote wa TLS, waje na kitu cha kutukwamua hapa. Asiende kichama wala hao wengine wote wasije hapo kichama cha siasa bali waje Kitaifa
 
Sawa unachosema mh. Lissu kinaweza kuwa ni sawa! Swali langu tena kwa mh. Lissu je tukubali kuendelea kuutupa kwa wazungu huu mchanga wenye madini lukuki;
Kwa sababu ya mikataba mibovu? Au alitakiwa mtu jasiri wa kusema imetosha? Ili iwe chanzo cha kubatilisha hizi sheria mbovu? Kipindi hicho alichokuwa tundu
Naamini kipindi mh. Lisu alichokuwa anapigania rasilimali uelewa wa watanzania ulikuwa mdogo na wasomi walikuwa wachache.
Hapa swala sio kuanza kumtafuta mchawi nani hapana, kinachotakiwa tuungane pamoja tupiganie rasilimali zetu.
Mh. Lissu atumie usomi wa kusaidi kutetea Mali zetu, aache kuwaogopa wazungu.
 
Hii nimeielewa mno
 
.., Kwenye masuala ya kukurupuka mimi sio mwenzenu (ninyi washangiliaji) ..., kama ujasiri ni sambamba na kukurupuka, mimi sio mwenzenu asilani.., na sasa mniite msaliti..., huu mchanga mtakuja kulipishwa Mapesa ya kutosha na fidia juu na arbitral tribunals za kimataifa.., rejea kesi ya IPTL.., rejea kesi ya kukamata samaki za wachina kwa kukurupuka.., wale wachina waliachiwa huru wao na meli yao ya TAWALIQ 1.., wakarejeshewa hati zao za kusafiria, pamoja na gharama yote ya samaki waliokuwemo ndani ya meli ile, samaki aina ya Jodari..., tukawalipa na fidia ya Bilioni 9.., endeleeni na hizi kelele zenu sasa, baadae msigeuze shingo pembeni wakati wa kuwalipa ACACIA fidia (Kiporo kikiwachachia).., tatizo sio ACACIA, tatizo ni CCM.., sheria mbovu zimetungwa na CCM, sera za madini na uwekezaji mbovu, mikataba haramu imeingiwa kwa siri.., mchawi sio ACACIA.., ni CCM!
 
Hivi hujui uchunguzi ulofanyika ni wa kisayansi. Hivyo ushahidi uliopo utabase ktk matokeo ya kisayansi. Tumwache mkuu afanye kazi kwa manufaa yetu. Nampongeza kwa kuunda tume
 
Fallacial statement. Tujadili hoja sio mtu!
 
HASWAAA
 
Hivi hujui uchunguzi ulofanyika ni wa kisayansi. Hivyo ushahidi uliopo utabase ktk matokeo ya kisayansi. Tumwache mkuu afanye kazi kwa manufaa yetu. Nampongeza kwa kuunda tume
Ndani ya CCM tu akina Chenge wamemwambi amedanganya sasa wewe unasema uchunguzi ni wa kisayansi kwani hao wana sayansi wao siyo wanadamu kwamba wanaweza kukosea!!?
 
Wakati miswada ya kipuuzi ya madini ikipitishwa bungeni Mhe. Raisi Magufuli alikua mbunge if m keeping my records well hakuwahi kusimama kupinga..
huyu ni chizi tuu aseme kama mikataba iliyo sainiwa ina halalisha kudanganya kiasi cha madini kilichomo ndani ya mchanga....
Tahira huyu
Lissu tangu lini ulikuwa mzalendo! Uzalendo wa kutetea fisadi lowasa, au uchumia tumbo upi anausema zaidi ya huu wa kupewa kitu kidogo kumsafisha mtu aliye mchafua kwa miaka 10. Lissuu wadanganye vipofu wa vabichaa
 
Mkuu elewa bandiko lake,kasema tunaibiwa kwenye sheria na mikataba.maana yake kakubali kwamba tunaibiwa na tunaibiwa isivyo sahihi ila sheria na mikataba ndio unatoruhusu kuibiwa huko
 
KWA NINI TUSIELEWE?
MFANYABIASHARA ANAPAKIA BANGI KUPELEKA INCHI JIRANI KWA KUCHANGANYA NA PUMBA YA MAHINDI.
BANGI INASAFIRISWA KWA JINA LA PUMBA.
TUJIRIDHISHE KWANZA, JE DHAHABU ILYOKO KWENYE MCHANGA NI NYINGI KULIKO TULIVYOKUBALIANA KWENYE MKATABA?
HAKUNA WIZI MDOGO, WIZI NI WIZI TU.
TUANZE NA WIZI MDOGO THEN TWENDE KWENYE ULE MKUBWA.
LISSU SHIRIKIANA NA RAIS KATIKA HILI KWA SABABU UMULIPIGANIA MUDA MREFU NA SASA AMEKUJA MTU AMBAYE ANATAKA KUFANYA ULIYOKUWA UNATAKA.
UKIMTUHUMU HATAKUBALI KUSHIRIKIANA NA WEWE HATA KAMA UNA UWEZO KIASI GANI.
ACHA RAIS ASHUNG'ULIKIE HILI SWALA KISIASA, KIUCHUMI, KISHERIA, KISAYANSI, KIDINI NA HATA KWA KUTUMIA NGUVU INGINE YEYOTE INAOKUBALIKA NA MUNGU AU ISIYOKUBALIKA ILI MRADI SISI TUSHINDE.
TUSIGOMBANIE SILAHA WAKATI TUNAPIGANA VITA MOJA.
CHADEMA WAJUE KAMA SI WAO KUMCHAFUA LOWASSA, LOWASA ANGEKUA RAIS WA INCHI HII KUPITIA CCM.
KWA MAANA HIYO NA KWA WATU WACHAMBUZI WA MAMBO, RAIS WA SASA YUKO MADARAKANI KWA MSAADA MKUBWA TOKA CHADEMA.
LEO LOWASA ANGEKUWA RAIS WA INCHI HII KUPITIA CCM MNGEMPIGIA KELELE ZAIDI NA ANGEWATANDIKA NAKUWAWEKA NDANI BILA HURUMA.
 
kama kweli watanzania wana uchungu na nchi hii waseme ukweli haya yote yanayotendeka yanafanyika katika utawala wa chama gani? na je?hakunawatu walikuwa wanalalamikia haya?tukibaki kujipendekeza kwa watu walioko madarakani tutazidi kuibiwa. ukwaeli ni kwamba yote haya yamefanyika chini ya utawala wa ccm hivyo bila kuwa wakweli wa kuwaondoa ccm madarakani tukubali kila mtu aishi kwa ujaja wake
 
Tundu lissu nimekosoma nimekuelewa Mkuu....Ila ni Wewe na wenzio mlipiga kelele sana Kuwa tutaingia hasara na kuwalipa wawekezaji kama tutaendelea kuyashikilia Yale makontena RAIS akaweka Pamba masikioni na kukomaa Leo baada ya Ripoti mnadai Kuwa ni nyinyi mlianza zamani kutetea huo unyonyaji...Kiufupi Wewe na wenzio ni WAPINZANI na kwa Africa hasa Tanzania UPINZANI tafsiri yake nyepesi ni KUPINGA....Kiufupi HAMUELEWEKI bora JPM na mapungufu yake yote aliyonayo ila angalau tunamuelewa....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…