Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Nitalipa malimbikizo ya wafanyakazi yote kuanzia 2015 - 2020

Ameshindwa kubadili mfumo wa Chadema ataweza mfumo wa Tanzania?
Chadema ina mfumo wa kupiga pesa ndiyo maana wamepiga hata pesa za wabunge wao walizochanga kwa ajili ya uchaguzi sasa wamebaki kuomba pesa kwa watz wanaohudhuria mkutanoni. Mimi leo niligoma kuchanga eti Faru John anatufundisha jinsi ya kutuma pesa toka Mpesa kwenda kwenye akaunti yao ya CDM2020 anataka azipige tena kama alivyozipiga za wabunge wao. Lissu rekebisha mfumo wa kipigaji kwa Saccos ya Chadema kama kweli uko serious!
 
Inavutia Lissu aendelee hivi hivi sera nzuri na mwelekeo mpya kwa Tanzania mpya tutafika, maendeleo ya watu sio vitu.
 
Huyu anataka turudi kwenye uchumi tegemezi.

Atatoa wapi hela endapo anaivunja TRA?

Haelezei atainuaje uchumi wa nchi bali anaelezea atakavyoharibu mifumo mizuri iliyojengwa
Reforms sio kuvunja! Matatizo ya elimu vila malipo haya(bora elimu)!!!!!
 

Kamanda hebu twambie huo mfumo mpya wa kodi ndio ukoje? Hahahahaha haya ndio matatizo ya kutokuwa na uzoefu na kuwa mwana harakati sana hahaha
 
Kamanda hebu twambie huo mfumo mpya wa kodi ndio ukoje? Hahahahaha haya ndio matatizo ya kutokuwa na uzoefu na kuwa mwana harakati sana hahaha
Wewe usifikiri Lissu ni jiwe anayehodhi kila kitu.....

Lissu hana huo ujinga yeye anaacha wataalamu na mifumo ifanye kazi
 
Sikiliza vizuri ..kwani tangu enzi za Nyerere TRA ilikuwepo?
Lissu kasema kuivunja na kuitengeneza upya yaani kuifumua basi...TULIENI JAMANI
Nyerere alikuwa anakusanya kodi kiasi gan bila Tra?
 
Kampeni wameanza au bado maana walisema hawataanza kampeni hadi walioenguliwa wateuliwe na tume?
Cha ajabu nchi hii kuna wanao shabikia awamu hii kutokana na wao kuifaidi keki ya taifa, na kuwatia ujinga ambao hata wale ambao hajui kesho atakula nini na wao wanafuatisha mkumbo tu!! Pili kuna wale ambao wanashabikia tu wakati ni wazee wa kwangu pakavu, ila ni ujinga tu!! Hata mpinzani aongee vipi jinsi ya kuwatoa kwenye hali hiyo, wao wanamuona ni adui!! SASA SIJUI WEWE UPO KUNDI GANI HAPO. kwani mwana ccm, lazima tu uwe kati ya makundi hayo.
 
Na.

Mwandishi wetu kigoma.


MGOMBEA UDIWANI CHADEMA KATA YA RUBUGA *OMARY GINDI* AKAMATWA NA POLISI KWA KOSA LA UTAPELI


Mgombea udiwani kata ya Rubuga kupitia chama cha demokrasia na maendeleo akamatwa na polisi na kufungwa kwa kosa la utapeli kama kawaida yake kuwa anauza pembe za ndovu.

Mgombea uyo alikamatwa jana akiwa hoteli na kuanza kuwalaghai na kufanya utapeli huo na baadae kukamatwa na polisi na mpaka sasa yupo ndani

Kigoma inahitaji madiwani safi na sio matapeli kama OMARY GINDI WA CHADEMA KATA YA RUBUGA.

Kigoma yetu safi hatuitaji matapeli kama OMARY GINDI WA RUBUGA TOKA CHADEMA.


KIGOMA YETU
KIGOMA MPYA
 
Inasukwa upya ili iache kubambikia watu kodi
Huyu anataka turudi kwenye uchumi tegemezi.

Atatoa wapi hela endapo anaivunja TRA?

Haelezei atainuaje uchumi wa nchi bali anaelezea atakavyoharibu mifumo mizuri iliyojengwa
 
Ndio sisi na kura tunampa, hatuwezi tapeliwa miaka 5 hakuna chochote cha kueleweka.
Anaongea upupu tu!! Malimbikizo ya wafanyakazi kwa miaka mitano. Asifikiri wafanyakazi hawajitambui kiasi hicho ajue wako serikalini wanajua pesa zinapatikana vipi.
 
Unakwama wapi ndugu,sema hapa wazi wamefanya vp ili Serikali ya wanyonge ikusaidie!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…