Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu alihojiwa na Dar 24 Media siku chache zilizopia. Akiwa katika mahojiano hayo Lissu amezungumza masuala mengi yanayohusu mwenendo wa kisiasa nchini.
Aidha alipoulizwa kuhusu kumchukulia Mkuu wa Wilaya wa zamani wa Hai, Lengai Ole Sabaya kama Mkosaji wa kisiasa, Tundu Lissu alipinga kwa kueleza kuwa kiongozi huyo hafai kuchukuliwa kama Mfungwa wa kisiasa, asema kiongozi huyo ni jambazi. Katika hilo Lissu amesema:
Mwandishi: Ukimtazama Sabaya anastahiki kuachiwa kama mkosaji wa kisiasa.
Lissu: Sabaya sio mkosaji wa kisiasa, Sabaya ni jambazi.
Mwandishi: Unahukumu Tundu
Lissu: Amehukumiwa! Ni mimi ndiyo nimemhukumu? Amehukumiwa kwa Ujambazi wa kutumia silaha. Na ambayo tunayafahamu sisi aliyoyafanya. Angeshtakiwa kwa yote ambayo tunayafahamu angekaa gerezani maisha yake yote.
Mwandishi: Lakini alikuwa anafanya kwa utashi wa kisiasa!
Lissu: Sio kwa utashi wa kisiasa, hakuna utashi wa kisiasa kwa kufanya makosa ya jinai. Wakwetu amesingiziwa, Sabaya hajasingiziwa. Shida yangu mimi na serikali ya Samia ni hii, kina Sabaya wapo wengi ajabu.
Mwandishi: Wapo uraiani?
LIssu: Ndiyo wapo Uraiani.
Mwandishi: Kama nani?
Lissu: Mfano: Paul Makonda anatakiwa ashughulikiwe. Makosa mengine ameyafanya waziwazi kabisa. Amenyang'anya watu magari, nyumba. Amevamia Clouds.
Mwandishi: Una Ushahidi?
Lissu: Upo! Umeonekana. Nakwambia kuna kina Sabaya wengi sana. Watu waliokuwa wanawanyang'anya watu mali na kuwafungulia makosa ya uongo haya. Kina DPP Mganga Biswalo leo jaji. Namsikia Mama juzi anasema wanawanyang'anya watu hela wanazipeleka China. Wote hawa walifanya makosa ya jinai wanapaswa kushughulikiwa kijinai. Lakini anachukuliwa Sabaya anakaangwa peke yake. That's my only regret. Na hiyo inaleta taswira kwamba pengine labda kuna sababu zingine zingine.
Mwandishi: Kwa nani?
Lissu: Kwa Sabaya, lakini the fact kwamba anang'ang'aniwa peke yake wakati waliotenda makosa kama haya wengi.