Uchaguzi 2020 Tundu Lissu, Sheikh Ponda, Askofu Mwamakula, Mbowe na Maalim Seif jukwaa moja wilayani Hai leo

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu, Sheikh Ponda, Askofu Mwamakula, Mbowe na Maalim Seif jukwaa moja wilayani Hai leo

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Lala salama ya uchaguzi zikiwa zimebaki siku 8 ( one digit) inaanza leo ambapo Tundu Lissu atakuwa Hai mkoani Kilimanjaro akiwa na Sheikh Ponda, Askofu Mwamakula na mgombea urais wa Zanzibar maalim Seif.

Kipenzi cha Watanzania Dkt. Magufuli akiwa na komredi Polepole wao wanaanzia Bagamoyo mkoani Pwani wakielekea Korogwe Tanga.

Habari ndio hiyo, kumeshakucha!

Maendeleo hayana vyama.

=====

LISSU: MAGUFULI ALIINGIA KWA KURA, ATAONDOKA KWA KURA

Mgombea Urais wa JMT kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu Lissu amesema ifikapo siku ya kupiga kura Oktoba 28, wananchi wote wakapige kura kufuta kilio na machozi ya miaka mitano

Akizungumza na wananchi katika kampeni zilizofanyika Hai Mkoani Kilimanjaro Lissu amewataka wananchi kuchagua viongozi watakaoleta haki kwakuwa Tanzania inahitaji haki

Ameongeza kuwa, maandiko matakatifu yanasema Haki huinua taifa na sio pesa wala barabara. Amewataka wananchi kupiga ili kupata haki na kuondokana na miaka ya njaa
 
Kwani CCM bado ipo ? siwasikii wananchi hata kuitaja,yaani wau huwasikii kabisa kuizungumza,wanasema kwanza ukiitaja tu basi siku yako nzima inavurugika,jinsi haka kachama kalivyolaanika.

Bwana Mungu aliona haina haja ya kutuletea Corona, Gonjwa liitwalo CCM peke yake litatosha kupambana nalo hadi tarehe 28 tunaenda kuliangamiza.

Yaani Bwana Mungu ana busara zisizo na mfano wake kama corona ingekuwepo ,tusingeweza kuiondoa CCM ,leo Alhamdulillah kila dalili zinaonyesha CCM inatokomezwa.
 
Nasikia bwana Sabaya amejiandaaa kwa vulugu leo hai kitanuka. #Sasabasi2020 #Tundulissu #maendeleo ya watu na huru
 
mtalia nyie na waume zenu ...Lissu ndie Rais wa Tanzania

Hawezi kuwa Rais.. wananchi hatutaki wanaolalamika na kukimbilia mawakili wa ulaya badala ya kuwa mzalendo na kuwapa kazi wa hapa nchini.

Waambie wamalize salama utalii.. naona maneno mengi.. wanajipeleka kuvunja kanuni.. msilie waambueni wapunguze udaku

Nasambaza lavu kwako 💚💛💚💛💚😃
 
Back
Top Bottom