Tundu Lissu: Tumekuwa na Marais Wezi

Hata Chadema mmekuwa na viongozi wezi,tena wasiotaka kuhojiwa kuhusu mapato na matumizi ya Chama.

Ni juzi mmetoka kumfukuza mtunga sera mahiri Dk Marcus Albanie.

Kisa amehoji ubadhirifu unaofanyika kwenye matumizi ya fedha za chama,nje ya mfumo rasmi.

Lissu anapata wapi ujasiri huo,wakati siku hizi Chadema ndio mtetezi wa mafisadi nchini.
 
Haya ndio yanayo waharibia leo hii ukimwambia mwananchi wa kawaida hakuelewi, watu wanataka maendeleo na maisha bora hicho ndio kitu wanacho kihitaji , ama sijui uzungumzie katiba hakuelewi maana katiba haimbadilishii maisha yake
 
Hivi hizi ndinga ziliendaga wapi?
 
Kwani kwa sasa tajiri akitaka ardhi anaikosa sababu ya maskini?
 
Hiyo ni kazi ya polisi na pccb, kama hivyo vyombo ni vya wavivu usiwalaumu chadema, mhalifu ni mhalifu tu, hakuna nani wala nani.
 
Haya mambo mbona mwenyekiti wako hana ujasiri wa kuyasema hadharani siku hizi?. Toeni majizi kwenye hilo genge lenu ndio muwe na legitimacy ya kukemea majizi waliopo kwenye vyama vingine.
 
Hiki chama hopeless kabisa.
 
Hapana. Nadhani hujaelewa au hujaunganisha vizuri yanayosemwa.

Kama rais ni mwizi, tena anayo mdaraka yote anayopewa na katiba, usalama wa ardhi hiyo upo wapi hapo?

Siyo lazima kufuata mfano mbovu wa Kenya kuhusu ardhi, lakini katiba inatakiwa kuwa wazi kuhusu ardhi kuwa mali ya nchi na kuweka utaratibu unaoeleweka katika matumizi yake bila ya kuigawa holela.
 
Hii sauti ya Lissu, sijui kama ndiyo sauti ya Mwenyekiti wake.

Hebu vuta subira kidogo mkuu 'Erythro', tuone mambo yanakoelekea.

Sasa hivi bado kuna ukungu mwingi unaozuia kuiona sura halisi ya chama ilipo. Nina hakika haitachukua muda kujua sura yenyewe halisi ni ipi, na jinsi Lissu alivyo.....Aaaah, sijui tena!
 
Kwa jinsi Lissu alivyo 'independent minded', naweza kumuondoa katika hitimisho unalofanya hapa, kwa sasa hivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…