PreGE2025 Tundu Lissu: Tumepokea barua za wabunge wawili kati ya 19 tuliowafukuza uanachama CHADEMA, wanataka kurudi

PreGE2025 Tundu Lissu: Tumepokea barua za wabunge wawili kati ya 19 tuliowafukuza uanachama CHADEMA, wanataka kurudi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu amesema wale wabunge 19 wapo 2 wameandika barua za kuomba msamaha warudi,
Mnanichanganya!! Warudi kutoka wapi? Si walitajwa kuwa ni wanachama halali hawana kadi za kijani!!
 
Viti maalum mhimili wa bunge Slaa alijiunga na mhimili wa serikali ya CCM na CCM
mbona kuna mama kule serengeti chadema walimpokea kutoka ccm na alikuwa mkuu wa wilaya mi nafkiri ni muda wa kuunganisha nguvu hata huko CCM kumegawanyika haswa ila kwa hawa covid 19 hapana
 
Ni Njaa tu pamoja na kutishwa na JPM, tuwasamehe tu hawa mama zetu.
 
Haya ya kutaka kuwarejesha Covid 19 ndani ya Chadema anafanya Lissu sasa, angeyafanya Mbowe angetukanwa kila tusi na kuitwa msaliti kutoka kwa wanachadema na maCCM.
Katiba inasema wenye mamlaka yakuwarudisha ni kikao kilichowafukuza sasa vijana wa Mbwamba mbona mnaumia sana uchaguzi umeisha jengeni chama kubalini matokeo mnaona TAL anasonga na chama kwa michango ya wananchi mnaanza kuumia tena mnataka afeli nyie mtanufaika na nini? Kama mwamba alipitiliza Jumba jeupe moja kwa moja bila kuwaarifu wenzie kwanini hawa wanawake wakiomba msamaha wasisamehe? Acheni ubaguzi muacheni TAL anyooshe chama na ayanyooshe ma vegetables chama kipo salama kuliko wakati wowote ule
 
Ila hili la kumpokea slaa chadema naona wamebugi mzee katumwa huyu wakafanya na igizo la kuwekana ndani ionekane ana ugomvi nao ili chadema wamsogezee jikon ajue nn kinaendeleea awapelekee
Uzuri wa ccm mambo yao huenda kwa akili sana.........tena hukuacha mwenyewe useme, wao utawaona wanashughulika na vitu vingine tu
 
Mimi nadhani ni jambo zuri kuwasamehe hawa hawakwenda kwa kupenda ila kwa mazingira ndiyo yaliyo wa force kwa wakati ule hata hawa wasienda wangeweza hata kuokoteza ambao siyo wanachama na kuwabambika kuwa ni wabunge wa CDM. Mimi nishauri waandike barua na kwakuwa watakuwa wamesamehewa watamalizia ubunge wao kisha waende wakapambane majimboni. Siasa zinakwenda na mda,, ana wakati. Huu ni mda wa hamsha amsha kila kinachowezekana kifanyike. Zimebaki siku chache sana kila kitu kiende kwa speed ya umeme. Hawakuibagaza CDM wakiwa bungeni imgawa waliitia doa na maumimuvu ila ndiyo siasa si hasa.
Ni kweli CHADEMA kilipitia kipindi kigumu sana wakati wa Awamu ya Magufuli, na kulikuwa na mashinikizo magumu sana na wenzetu wengine ikawa ni too much, lakini kama wanaomba msamaha kwa makosa yao basi warudi tupambane kwa pamoja dhini ya hili jinamizi la CCM.
 
Hili ni jambo la Kamati kuu na Baraza kuu
Ndiyo.
Lijadiliwe huko na liamriwe huko kwa mijadala huru na haki.
Pamjoja na yote, itashangaza sana wakirudi kirahisi tu kana kwamba hakuna lolote baya lililofanyika kwa chama.
Kurudi kwao kuwe kwa masharti maalum; moja likiwa kutogombea nafasi yoyote ya uongozi katika muda maalum, ikiwemo ubunge.
Atakaye kubaliana na sharti hilo, huyo atakuwa na mapenzi na chama na siyo msukumo wa maslahi binafsi.
 
Mpeni Gwanda Dr.Slaa aingie Vitani ni mpambanaji mwenye experience ya miongo mingi, amekwepa mishale mingi ya ccm.
 
Back
Top Bottom