Lissu kurudi URaiani, ni haki; yake, ya wanachama wenzake na ya waTanzania wote wenye mapenzi mema na nchi hii; siyo zawadi kutoka kwa yeyote.Lissu akiachiwa huru hata tarehe 29 Julai, macho na masikio yataelekezwa kwake na hivyo kupumua na kuamua kutapata utulivu. Lissu anapokelewa; ataongea; ataendelea na chama chake na siasa zitarudi kwenye barabara yake. Lissu atarejesha siasa siasani na maneno majukwaani.
Imebaki hii ya Lissu tu kurudi uraiani na siasani ili kufanyike siasa!
Samia hatoi zawadi ya kumwachia Tundu Lissu, na wala hana lolote atakalotegemea kunufaika nalo, hata kisiasa.
Juhudi za kuikomboa Tanzania zitabaki pale pale, kamwe hazipoi.