Lissu kurudi URaiani, ni haki; yake, ya wanachama wenzake na ya waTanzania wote wenye mapenzi mema na nchi hii; siyo zawadi kutoka kwa yeyote.Lissu akiachiwa huru hata tarehe 29 Julai, macho na masikio yataelekezwa kwake na hivyo kupumua na kuamua kutapata utulivu. Lissu anapokelewa; ataongea; ataendelea na chama chake na siasa zitarudi kwenye barabara yake. Lissu atarejesha siasa siasani na maneno majukwaani.
Imebaki hii ya Lissu tu kurudi uraiani na siasani ili kufanyike siasa!
Unfortunately,ni sualalamudatu, something like "bness as usual...." Ndo basi TenaNajua hamtaniamini. Najua mpo mtakaobisha vya kutosha na kutisha. Mtapaniki kuliko pikipiki ya kutumia kiki. Lakini, nawaambia jambo hili. Ni jambo geni na kubwa lakini muhimu na linalowezekana kwenye siasa za sasa. Siasa za sasa zinahitaji amshaamsha.
Haifichiki tena kuwa mambo ndani ya CCM yetu si shwari. Hali si hali. Wanaohoji hadharani kuhusu uhalali wa uteuzi wa rais Samia kuwa mgombea wa Urais wa CCM wamefika wawili: Mch. Malisa wa Kilimanjaro na Polepole wa palepale.
Sirini, maelfu ya wana-CCM wanawaunga mkono hao. Ni uoga-wa-kawaida tu wa kitanzania unaowazuia kusema hadharani. Wanaogopa 'kushughulikiwa' kichama na kadhalika. Wanaogopa kujikuta wakiishi mafichoni kuliko porini na kusikojulikana kama maficho ya Havana.
Nami ni muoga wa hadharani kutokana na 'viapo' vyangu. Lakini, nami niko kwenye msimamo kuwa mchakato wa kumteua Mwenyekiti huku yeye akiongoza uteuzi huo haukuwa halali na ulikiuka Katiba ya CCM na ya Tanzania. Uteuzi wa wagombea vyamani huanza baada ya kuvunjwa kwa Bunge. Ni msimamo wa kikatiba yenye tiba.
Rais na Mwenyekiti wangu ametingwa. Hata mkutano mkuu kuhamishiwa kwa mtandao usio na mtandio hakutasaidia kitu. Mkutano utakosa hamshahamsha na ufanisi. Wajumbe wataambiwa tu bila ya wao kusema. Wataagizwa bila kuumizwa lakini watalizwa. Misimamo itabaki ile ile.
Rais na Mwenyekiti wangu amebaki na Tundu Lissu kama turufu mujarabu yenye jawabu kwa yanayoendelea. Lissu anaungwa mkono ndani na nje ya CCM. Anaungwa mkono na ndani na nje ya nchi. Wengine wanatema nyongo zao kwakuwa tu Lissu yuko mahabusu na 'kuonekana' anateseka kule.
Lissu akiachiwa huru hata tarehe 29 Julai, macho na masikio yataelekezwa kwake na hivyo kupumua na kuamua kutapata utulivu. Lissu anapokelewa; ataongea; ataendelea na chama chake na siasa zitarudi kwenye barabara yake. Lissu atarejesha siasa siasani na maneno majukwaani.
Imebaki hii ya Lissu tu kurudi uraiani na siasani ili kufanyike siasa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Gauteng, Afrika ya Kusini)
Najua mnapenda sana kujiaminisha hivyo, nyinyi mliopo upande huo wa GENGE.Wacha kujipa umaarufu usiokuwa nao. Ma threads yako yote unajifanya wewe ni "insider" wa Lumumba wakati ni kapuku tu.
Hii sintofahamu ya CCM kwa kipindi hiki ni ya kawaida tu tukikaribia uchaguzi. Makundi masilahi lazima yawepo, lazima yavutane lakini mwisho wa siku inabakia CCM moja.
Litakwisha, Oktoba tunatiki na Samia tunaye hadi 2030. Wenye akili wanajipanga 2030. Hii ya 2025 imekwisha
Naam,ndivyo ilivyo.Unanikumbusha utabiri wa Mwalimu Nyerere kuwa tukimaliza kubaguana Bara dhidi ya visiwani,tutaanza kubaguana makabila na makabila na baadaye tukimaliza huko,tutabaguana ndani ya kabila moja; wataanza Mchaga wa Rombo dhidi ya wa Machame nk.
Kwa hiyo,CCM tumemalizana na Chadema,tumeanza wenyewe kwa wenyewe.
Wewe mkulima wa miwa huwezi kuwa na akili ndiyo maana unalima miwaTangu lini mambo magumu kama haya vijana wa ccm mkaelewa?
Mambo haya anayajua na yanamuumiza mno M/kiti wako, ila wewe endelea kufanya zamu ya kuondolewa ubongo kichwani ili uendelee na ukapuku wako
Hakuna kundi litazidi la Lowassa. Lilikuwa na nguvu kisiasa, kifedha na lilikuwa na mshikamano. Na lilisambaratika. Sasa hivi kuna waganga njaa tu Sukumagang wamemtanguliza PolepoleNajua mnapenda sana kujiaminisha hivyo, nyinyi mliopo upande huo wa GENGE.
CCM, siyo CCM ile ya kawaida tena; na hili sasa ni jambo lililo wazi, na wana-CCM wenyewe sasa wamelitambua.
Hayo makundi unayoyazungumzia wewe ndani ya CCM, hayajawahi kuwa kama haya yaliyopo sasa, ambapo kuna kundi la GENGE lililoamua kukishika chama na kukifanya kiwe ndiyo nyenzo yake yaa kufanyia uchafu.
Hapajawahi kuwepo na kundi la aina hiyo, tokea CCM ianzishwe; hii ni mara ya kwanza kabisa.
Kwa hiyo usitegemee kuona ile kawaida ya miaka mingine, ndiyo iwe kawaida
Bongo za watanzania zimeharibiwa sana na maccmWewe mkulima wa miwa huwezi kuwa na akili ndiyo maana unalima miwa
Ila msiwaogopeshe kuhusu Lissu akitoka hatazuilika. Wakisikia haya maneno ndio kwanza wanafunga mbinu za kumshikilia gerezani asitoke.Ccm wanadai solution ni NRNE 💪 🔥
Akitoka Lissu hatozuilika.
Ukikaa moto, tukisimama 🔥
GENGE lenu; la Samia na Kikwete; siyo Kundi; nimekwisha kueleza lakini hutaki kuelewa tu kwa sababu zako mwenyewe.Hakuna kundi litazidi la Lowassa. Lilikuwa na nguvu kisiasa, kifedha na lilikuwa na mshikamano. Na lilisambaratika. Sasa hivi kuna waganga njaa tu Sukumagang wamemtanguliza Polepole
Naona mnajitekenya na kujichekesha wenyewe kama mazuzuNyie vidampa wa mama Lucas Mwashambwa ChoiceVariable The Sunk Cost Fallacy The Sunk Cost Fallacy 2
Mmemsikia hapa huyu kada mkongwe wa Lumumba ?
Nyie bado mnajidanganya na kuendeshwa na nguvu ya buku 7 kwamba huko chamani ni shwari kumbe nyie mnatupiwa makombo tu nje hamjui ndani wamekula nini.
Hapo unaona kuna mtu anatekenywa?Naona mnajitekenya na kujichekesha wenyewe kama mazuzu
Vipi sintofahamu imekwisha??Wacha kujipa umaarufu usiokuwa nao. Ma threads yako yote unajifanya wewe ni "insider" wa Lumumba wakati ni kapuku tu.
Hii sintofahamu ya CCM kwa kipindi hiki ni ya kawaida tu tukikaribia uchaguzi. Makundi masilahi lazima yawepo, lazima yavutane lakini mwisho wa siku inabakia CCM moja.
Litakwisha, Oktoba tunatiki na Samia tunaye hadi 2030. Wenye akili wanajipanga 2030. Hii ya 2025 imekwisha
Ulipoteleaga wapi Mzee VUTA-NKUVUTE?Najua hamtaniamini. Najua mpo mtakaobisha vya kutosha na kutisha. Mtapaniki kuliko pikipiki ya kutumia kiki. Lakini, nawaambia jambo hili. Ni jambo geni na kubwa lakini muhimu na linalowezekana kwenye siasa za sasa. Siasa za sasa zinahitaji amshaamsha.
Haifichiki tena kuwa mambo ndani ya CCM yetu si shwari. Hali si hali. Wanaohoji hadharani kuhusu uhalali wa uteuzi wa rais Samia kuwa mgombea wa Urais wa CCM wamefika wawili: Mch. Malisa wa Kilimanjaro na Polepole wa palepale.
Sirini, maelfu ya wana-CCM wanawaunga mkono hao. Ni uoga-wa-kawaida tu wa kitanzania unaowazuia kusema hadharani. Wanaogopa 'kushughulikiwa' kichama na kadhalika. Wanaogopa kujikuta wakiishi mafichoni kuliko porini na kusikojulikana kama maficho ya Havana.
Nami ni muoga wa hadharani kutokana na 'viapo' vyangu. Lakini, nami niko kwenye msimamo kuwa mchakato wa kumteua Mwenyekiti huku yeye akiongoza uteuzi huo haukuwa halali na ulikiuka Katiba ya CCM na ya Tanzania. Uteuzi wa wagombea vyamani huanza baada ya kuvunjwa kwa Bunge. Ni msimamo wa kikatiba yenye tiba.
Rais na Mwenyekiti wangu ametingwa. Hata mkutano mkuu kuhamishiwa kwa mtandao usio na mtandio hakutasaidia kitu. Mkutano utakosa hamshahamsha na ufanisi. Wajumbe wataambiwa tu bila ya wao kusema. Wataagizwa bila kuumizwa lakini watalizwa. Misimamo itabaki ile ile.
Rais na Mwenyekiti wangu amebaki na Tundu Lissu kama turufu mujarabu yenye jawabu kwa yanayoendelea. Lissu anaungwa mkono ndani na nje ya CCM. Anaungwa mkono na ndani na nje ya nchi. Wengine wanatema nyongo zao kwakuwa tu Lissu yuko mahabusu na 'kuonekana' anateseka kule.
Lissu akiachiwa huru hata tarehe 29 Julai, macho na masikio yataelekezwa kwake na hivyo kupumua na kuamua kutapata utulivu. Lissu anapokelewa; ataongea; ataendelea na chama chake na siasa zitarudi kwenye barabara yake. Lissu atarejesha siasa siasani na maneno majukwaani.
Imebaki hii ya Lissu tu kurudi uraiani na siasani ili kufanyike siasa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Gauteng, Afrika ya Kusini)
Huyu mzee tupatupa kapotea kabisaWewe Mzee mbona umepotea hivi hadi mambo yanaharibika kwa kiwango hiki kulikoni?