Tundu Lissu: Uhusiano wangu na Mwenyekiti Mbowe siyo mzuri

Tundu Lissu: Uhusiano wangu na Mwenyekiti Mbowe siyo mzuri

Makamu mwenyekiti ambaye pia ni mgombea wa kiti cha mwenyekiti wa Chadema kwenye uchaguzi ujao tarehe 21, January Bwana Tundu Antipas Lisu amefichua siri kuwa uhusiano wake na mwenyekiti wa chama Freeman Mbowe kuwa ni mbaya sana kiasi kwamba hawezi kwenda nyumbani kwa Mbowe akala na kunywa kwa uhuru kama zamani.
Bwana Lisu amebainisha kuwa hayo mahusiano mabaya hayajaishia kwake tu kwani hata viongozi wengine kama Peter Msigwa, Godbless Lema, John Heche mahusiano yao na Mbowe ni mabaya sana kiasi kwamba wamekuwa wakishughulikiwa mmoja baada ya mwingine hali iliyopelekea mch Msigwa kukimbia chama.

View: https://youtu.be/ecX9MBEE8y4?si=5tpMLBCrMM5Llyb7

Mbowe kagoma kustaafu kwa heshima, acha astaafishwe kwa fedheha.
 
Kwahiyo kumbe ni hotuba ile ile tu sio kingine?
Maana baada ya kutangaza nia, mara kesho yuko clouds mara ka tweet huko X, ndio kiongea sana huko nakosemea mimi
Alitangaza nia, baada ya hapo akawa kimya hadi walipomfuata baada ya Wenje kutoa Tuhuma, ndiyo akatoa ufafanuzi wa hilo na mengineyo, so Tangu juzi wamekuwa waki shara hayo mahojiano na vingi vitaendelea kuwa shared sababu anayoyaongea yanajadilika na yanawafungue wengi macho.
Kinyume cha hapo angeonekana ni wa hovyo na hafai.
 
Makamu mwenyekiti ambaye pia ni mgombea wa kiti cha mwenyekiti wa Chadema kwenye uchaguzi ujao tarehe 21, January Bwana Tundu Antipas Lisu amefichua siri kuwa uhusiano wake na mwenyekiti wa chama Freeman Mbowe kuwa ni mbaya sana kiasi kwamba hawezi kwenda nyumbani kwa Mbowe akala na kunywa kwa uhuru kama zamani.
Bwana Lisu amebainisha kuwa hayo mahusiano mabaya hayajaishia kwake tu kwani hata viongozi wengine kama Peter Msigwa, Godbless Lema, John Heche mahusiano yao na Mbowe ni mabaya sana kiasi kwamba wamekuwa wakishughulikiwa mmoja baada ya mwingine hali iliyopelekea mch Msigwa kukimbia chama.

View: https://youtu.be/ecX9MBEE8y4?si=5tpMLBCrMM5Llyb7

naona wengi sasa wameshajua kuwa, mbowe ndio mrudisha maendeleo ya nchi hii namba moja, kwa sababu huwa anawachezea wenzake akili, anavuta mpunga, anaacha wenzie waumizwe, vijana wapigwe, ila yeye huo uwenyekiti anafaidika nao sana na hataondoka. wananchi wa chadema nadhani angalieni wenyewe na mhukumu wenyewe. pia, Lisu anapata shida sana hata kuongea mengi kwa sababu tu ati mbowe ndiye alishika chupa wakati amepigwa risasi. risasi zenyewe alipigwa akipigania hicho chama, mbowe hakuwa na harakati zozote za kuweza kupigwa risasi. lakini kijana aliyekuwa mstari wa mbele ndio umekuwa utumwa sasa, lisu hatakiwi kumbeza saaana kwa sababu tu atasema mimi ndiye nilikuokoa siku ile usife.

napenda kuwaambia watu, mtu akikusaidie mshukuru Mungu, usimpe sifa mwanadamu, Mungu ndiye alimwokoa lisu, iwe kwa kutumia mbowe, msigwa au yeyote, na mbowe pia ajue kuna Mungu mbinguni ambaye hata yeye aweza kupatwa na janga hata leo akasaidiwa na wengine, yeye sio mwokozi wa kushikilia wenzake utumwa kwa sababu tu ati aliwasaidia. kwa hiyo mtu akikusaidia ndio afanye chochote usiseme? na kama lisu anasema hawezi kuwa na ujasiri kula kwa mbowe, ina maana mbowe ana mambo ya siri ya uuaji pia huwa anafanya, yale anayolaumiwa nayo kumbe inawezekana sio ya uongo.
 
Wanasiasa wapizani Tanzania ni pasua kichwa jambo la muhim mbowe kusoma alama za nyakati
 
Juzi tu alisema kuwa Hana tatizo lolote na Mbowe Leo tena anasemaje? Acha CDM ife ili wananchi tuidai nchi yetu kwa nguvu ya Umma
 
deed5ff644655f7b99ba1ff6559532f0.jpg
 
TL asema uhusiano wake na Mbowe ni Civil akiimanisha kwamba wote wana jakamoyo ingawa bado waweza kuwasiliana na kuongea haya na yale kama kawaida.

Kwa kiingereza amaanisha kwamba "polite and formal meaning civil to each other but they both still angry".
 
Lissu ni aina ya watu wasio na siri, watatoitoboa tu wakiguswa penyewe.

Aina hii ya watu ni wazuri na ni wabaya vilevile, inategemeana na upande uliopo.
 
Kuongea kwake ndio umekuwa ulinzi wake na tegemeo lake pekee.Bila hivyo tungesha msahau zamaani.
Ila ni kweli, kuna vitu nimemsikia kaongea unaona kabisa hii imeongelewa kiufundi zaidi.
Mfano kwenye power breakfast ya clouds aliongea sentesi moja akasema "Nimetonywa habari na mtu mkubwa serikalini kuwa Dola ina mpango wa kunidhuru halafu BANGUSILO (mbeba lawama) AWE MWENYEKITI MBOWE".

Hapa kwa wenye akili tukajua tu hii kauli nani kalengwa na kama vipi inabid arudishe majeshi nyuma.
 
Makamu mwenyekiti ambaye pia ni mgombea wa kiti cha mwenyekiti wa Chadema kwenye uchaguzi ujao tarehe 21, January Bwana Tundu Antipas Lisu amefichua siri kuwa uhusiano wake na mwenyekiti wa chama Freeman Mbowe kuwa ni mbaya sana kiasi kwamba hawezi kwenda nyumbani kwa Mbowe akala na kunywa kwa uhuru kama zamani.
Bwana Lisu amebainisha kuwa hayo mahusiano mabaya hayajaishia kwake tu kwani hata viongozi wengine kama Peter Msigwa, Godbless Lema, John Heche mahusiano yao na Mbowe ni mabaya sana kiasi kwamba wamekuwa wakishughulikiwa mmoja baada ya mwingine hali iliyopelekea mch Msigwa kukimbia chama.

View: https://youtu.be/ecX9MBEE8y4?si=5tpMLBCrMM5Llyb7

Huu uchaguzi umetufumbua macho
 
Sema Lissu nae anaongea sana tatizo mimi ndio maana nashindwa kumuamini 100% ., mbowe simkubali ila lissu ananipa mashaka pia
Ni kwasababu watanzania tumezoea sana maisha ya kinafki hata pale ambapo jibu la wazi lipo bayana

Hata jambo ambalo kila mtu mwenye akili timamu anaweza kujua kinachoendelea, bado tunataka kutegemea kupewa majibu tofauti wakati mazingira yanapinga.

Hivi kwa situation ya sasa hata kama Lissu asingeweka bayana uhusiano wake na Mbowe unataka kuniambia kwamba wewe ulikuwa ukiamini kuwa Lissu na Mbowe uhusiano wao hauja shake?

Au ulikuwa unalijua ila ulitaka tu kuona jamaa akifanya unafki kupinga kuonesha bado wanaukaribu wa siku zote??

Halafu jamaa hajajibu kwa kubeza upande wa Mbowe kuwa ndio una tatizo, ameweka uwezekano wa hata yeye huwenda ni sababu ya huo ukaribu kupungua.
 
Back
Top Bottom