Tundu Lissu: Uhusiano wangu na Mwenyekiti Mbowe siyo mzuri

Tundu Lissu: Uhusiano wangu na Mwenyekiti Mbowe siyo mzuri

Makamu mwenyekiti ambaye pia ni mgombea wa kiti cha mwenyekiti wa Chadema kwenye uchaguzi ujao tarehe 21, January Bwana Tundu Antipas Lisu amefichua siri kuwa uhusiano wake na mwenyekiti wa chama Freeman Mbowe kuwa ni mbaya sana kiasi kwamba hawezi kwenda nyumbani kwa Mbowe akala na kunywa kwa uhuru kama zamani.
Bwana Lisu amebainisha kuwa hayo mahusiano mabaya hayajaishia kwake tu kwani hata viongozi wengine kama Peter Msigwa, Godbless Lema, John Heche mahusiano yao na Mbowe ni mabaya sana kiasi kwamba wamekuwa wakishughulikiwa mmoja baada ya mwingine hali iliyopelekea mch Msigwa kukimbia chama.

View: https://youtu.be/ecX9MBEE8y4?si=5tpMLBCrMM5Llyb7

Umeitoa wapi hii? Maana ni kama amerekodiwa sehemu akiwa mwenyewe. Au ni huu ujinga wa AI mnaleta humu mitandaoni kuchafua watu?
 
Kung'ang'ania madaraka kwa mbowe ndio kumemletea yote hayo, angeachia mtu mwingine yeyote astaafu kwa heshima historia ingemkumbuka.
 
Uhusiano uliharibika mara tu Lisu alipostukia yale mabilioni ya rushwa toka Abdul kwenda kwa mbowe
 
Heri ya Christmas Wanajamvi.
Mjadala wa CHADEMA, kwa sasa ndio habari ya mjini, hata kwa wasiofuatilia Siasa.

Imefikia hatua hata uteuzi na uapisho uliofanyika Ikulu ndogo ya TUNGUU uliofanyika majuma kadhaa yaliopita ,kutopata coverage ya kutosha kwenye mitandao ya kijamii kama ilivyo Habari ya umwenyekiti wa CHADEMA.

Ushauri wangu, mteue KINGWENDU kuwa Mbunge, na BAMBO kuwa mjumbe wa bodi Mojawapo kama vile bodi ya utalii,kupitia waziri mwenye dhamana.

Baada ya uteuzi huo kwa muda Mjadala wa CHADEMA utaenda likizo na watu watajadili uteuzi wa BAMBO na KINGWENDU.

Ukilifanya hilo mheshimiwa Rais, utakuja kunishukuru.

Nimetumia BAMBO na KINGWENDU kama mfano, inawezekana pia ukawateua Ndugu wengine tofauti, kama ndugu yangu MADEBE LIDAI na na mtaani wangu Muhogo mchungu.

Ushauri sio shururuti, unaweza kukataa pia sio Lazima kuafiki.

Ni hayo tu mh Rais, Nikutakie Christmas njema.
 
Makamu mwenyekiti ambaye pia ni mgombea wa kiti cha mwenyekiti wa Chadema kwenye uchaguzi ujao tarehe 21, January Bwana Tundu Antipas Lisu amefichua siri kuwa uhusiano wake na mwenyekiti wa chama Freeman Mbowe kuwa ni mbaya sana kiasi kwamba hawezi kwenda nyumbani kwa Mbowe akala na kunywa kwa uhuru kama zamani.
Bwana Lisu amebainisha kuwa hayo mahusiano mabaya hayajaishia kwake tu kwani hata viongozi wengine kama Peter Msigwa, Godbless Lema, John Heche mahusiano yao na Mbowe ni mabaya sana kiasi kwamba wamekuwa wakishughulikiwa mmoja baada ya mwingine hali iliyopelekea mch Msigwa kukimbia chama.

View: https://youtu.be/ecX9MBEE8y4?si=5tpMLBCrMM5Llyb7

Endelea kuropoka Lissu. Sasa tunataka utwambie ukiwa kitandani na mkeo huwa mnafanyaje mambo yenu. Na yenyewe ni muhimu sana kwenye kupata kura za uwenyekiti wa Chadema. Ahahahahaha!!!
 
Sema Lissu nae anaongea sana tatizo mimi ndio maana nashindwa kumuamini 100% ., mbowe simkubali ila lissu ananipa mashaka pia
Fikra zangu, Lissu ameamua kutumia mbinu ya kujihami mapema kabla. Likimpata jambo mnakuwa na taarifa. 2017 alishasema pia anafuatiliwa na watu kabla hakapigwa risasi.
 
Back
Top Bottom