naona wengi sasa wameshajua kuwa, mbowe ndio mrudisha maendeleo ya nchi hii namba moja, kwa sababu huwa anawachezea wenzake akili, anavuta mpunga, anaacha wenzie waumizwe, vijana wapigwe, ila yeye huo uwenyekiti anafaidika nao sana na hataondoka. wananchi wa chadema nadhani angalieni wenyewe na mhukumu wenyewe. pia, Lisu anapata shida sana hata kuongea mengi kwa sababu tu ati mbowe ndiye alishika chupa wakati amepigwa risasi. risasi zenyewe alipigwa akipigania hicho chama, mbowe hakuwa na harakati zozote za kuweza kupigwa risasi. lakini kijana aliyekuwa mstari wa mbele ndio umekuwa utumwa sasa, lisu hatakiwi kumbeza saaana kwa sababu tu atasema mimi ndiye nilikuokoa siku ile usife.
napenda kuwaambia watu, mtu akikusaidie mshukuru Mungu, usimpe sifa mwanadamu, Mungu ndiye alimwokoa lisu, iwe kwa kutumia mbowe, msigwa au yeyote, na mbowe pia ajue kuna Mungu mbinguni ambaye hata yeye aweza kupatwa na janga hata leo akasaidiwa na wengine, yeye sio mwokozi wa kushikilia wenzake utumwa kwa sababu tu ati aliwasaidia. kwa hiyo mtu akikusaidia ndio afanye chochote usiseme? na kama lisu anasema hawezi kuwa na ujasiri kula kwa mbowe, ina maana mbowe ana mambo ya siri ya uuaji pia huwa anafanya, yale anayolaumiwa nayo kumbe inawezekana sio ya uongo.