Mtondoli
Member
- Nov 9, 2021
- 70
- 174
Wadau mjumbe hauwawi,,tulikosea Sana kumwamini lissu kuwa anafaa kuwa rais wa nchi ,tulikosea Sana na hii kitu imekighalimu Sana chama chake,,tulidhani Kila mhubiri anafaa kuwa mchungaji,,la hasha wengine wanatakiwa tu kuwa wainjilisti na sio wachungaji,,au tulidhani kuwa mchungaji wa mifugo anaetembea na fimbo Kila mahali ndie Bora ,na kumbe si hivyo fimbo Ina mahali pake,lissu Hana karama ya uongozi labda awe mwanaharakati,lissu hawezi kutafuna kitu ndipo ameze yeye anameza bila kutafuna,Hana japo chembe ya hekima ya kujua kuishi na mtu mwema na mbaya pia,msikilize hotuba zake zote za kampeni ,anatukana Kila kitu hata wanaomlinda yeye mwenyewe ,awamu nyingine tusimpe mtu nafasi ya kutuongoza kwa kigezo Cha uongeaji wake abaki kuwa mwanasheria lakini siasa haziwezi tulikosea Sana ,pili yeye nimakamu mwenyekiti nilitegemea kipindi hiki ambacho mwenyekiti yupo gerezani yeye akitumie kutafuta suluhu ya kidipromasia lakini naona yupo mitandaoni anamenyana na akina zitto,zitto ametimiza wajibu wake na yeye atimize wajibu wake,tuone na yeye hekima yake kwa Jambo hili,kinyume chake yeye ndiye atachelewesha mbowe kuachiwa kwa kiburi Cha uanasheria mjumbe hauwawi Niko tayari kwa maoni yoyote maana nawajua kazi iendelee