Uchaguzi 2020 Tundu Lissu usijidanganye; Watanzania siyo wajinga kama wananchi wa Belarus wanaoshinikizwa na mabeberu wamtoe Rais wao madarakani

Hivi Mabeberu ndio hawa waliowauzia "skrepa"anayozunguka nayo Chakubanga Moshi, na Arusha, kufanya kampeni haramu dhidi ya Mbowe..?!
 
Gaddafi aliondolewa na wasaliti na vibaraka wa mabeberu.

Mara nyingi mabeberu huwa nyuma yako ufanye kila kitu ikiwemo kumuua Gaddafi walimuua haowaho walibya wenzake.

Kiko wapi leo Libya wanapata tabu walizojitakia wenyewe?

Unafahamu mafuta ya Libya yanaenda wapi sasa?

Bila shaka majibu yote unayo ila unajitoa ufahamu.
Raslimali za Tanzania chini ya ccm kwa miaka 60 zinaenda wapi? Mbona maisha yetu ni afadhari ya jana
 
Mimi binafsi wala sisubiri Lissu au mwana siasa yeyote anambie, Miaka mitano ya Magufuli ilikua ni mateso, dhuruma na mauaji. Mkivuruga Uchaguzi huu tutapasuana matumbo tulane maini, wenyewe kwa wenyewe. Mwaka huu ni kufa na kupona. Magufuli alishashindwa ampishe Lissu.
 
Mabeberu ni kina nani hao embu kuwa specific wataje?
 
Poor post,labda nikuulize swali ambalo lissu ameuliza na hajapewa majbu mpka sasa,mabeberu ni kina Nani??ndio hao mnaowategemea kwa kila jambo au wap ebu wataje hao mabeberu
 
The thing is, jiwe anakubalika na wengi. Tembea na uliza tu kishkaji, watu wa mtaani watakuambia. Pamoja na makosa mengi ya "kiufundi" bado jiwe anashinda bila tatizo, ni kweli kuwa Lissu ataleta ushindani, lakini aandaliwe kwa 2025, not this time.
Umetembea wapi ukauliza kishkaji? Nani akupe jibu kinyume na lile unalotaka kulisikia? Unadhani hawajipendi? Pengine mkao wako wewe wakakudanganya, ama umeuliza huko kwenye viunga vyenu.
 
Raslimali za Tanzania chini ya ccm kwa miaka 60 zinaenda wapi? Mbona maisha yetu ni afadhari ya jana

Inategemea maisha yako uliyapanga vipi ni wewe ndie unaefahamu.

Kuhusu rasilimali ni kwamba zilikuwepo na hadi sasa zipo ila ulaghai wa nchi za kibeberu katika kutusainisha mikataba mibovu kwa kushirikiana na viongozi wasaliti.

Hata Tundu Lissu ni mmojawapo wa wasaliti hao kwani yeye alikuwa akisaidia makampuni ya kibeberu kuiba rasilimali zetu kwa kuwaelekeza kisheria namna ya kukwepa kodi na ulipaji mirahaba.

Kitendo cha kubadilisha sheria ya madini ili itunufaishe kama nchi na kuwabana wenye makampuni ambayo mengine ni ya kitapeli kama ACACIA, kimemchukiza sana Tundu Lissu, yeye kama yeye.

Ndo maana jambo hilo pia limemfanya awe na chuki tena binafsi dhidi ya raisi JPM na serikali yake.

Hivyo amekaa miaka mitatu mizima nchini Ubelgiji akipanga na nchi hizo za kibeberu namna ya kufanya ili awe raisi kibaraka wao halafu akiwa raisi arudishe tena mikataba ileile ilowasaidia wao kuiba rasilimali zetu.

Na hivyo ndivyo wanavyofanya nchi za kibeberu huko Iraq na Libya.

Wanashindwa kufanya hivyo huko Mali kwasababu Mali ni daraja la kwenda hukohuko kwao hivyo usalama wa Mali ndo usalama wa nchi za Italy na Greece na hatimae nchi zote za kibabaru maana hawatutaki sisi waafrika tuendelee kwenda kwao.

Ila wanataka waendelee kutuibia na kututumia.
 
.... ndiyo maana tunawashauri wenye dola yao wasilete figisu kwenye uchaguzi October dhidi ya Lissu ili tusiwe kama ilivyo Libya leo!
Mkuu wala hakuna figisu lisu kwa magu ni sisimizi kwa tembo wala usilinganishe atapata anacho style
 
Inategemea maisha yako uliyapanga vipi ni wewe ndie unaefahamu.

Kuhusu rasilimali ni kwamba zilikuwepo na hadi sasa zipo ila ulaghai wa nchi za kibeberu katika kutusainisha mikataba mibovu kwa kushirikiana na viongozi wasaliti.

Hata Tundu Lissu ni mmojawapo wa wasaliti hao kwani yeye alikuwa akisaidia makampuni ya kibeberu kuiba rasilimali zetu kwa kuwaelekeza kisheria namna ya kukwepa kodi na ulipaji mirahaba.

Ndo maana jambo hilo limemfanya awe na chuki tena binafsi dhidi ya raisi JPM na serikali yake.

Kitendo cha kubadilisha sheria ya madini ili itunufaishe kama nchi na kuwabana wenye makampuni ambayo mengine ni ya kitapeli kama ACACIA, kimemchukiza sana Tundu Lissu, yeye kama yeye.

Hivyo amekaa miaka mitatu mizima nchini Ubelgiji akipanga na nchi hizo za kibeberu namna ya kufanya ili awe raisi kibaraka wao halafu akiwa raisi arudishe tena mikataba ileile ilowasaidia wao kuiba rasilimali zetu.

Na hivyo ndivyo wanavyofanya nchi za kibeberu huko Iraq na Libya.

Wanashindwa kufanya hivyo huko Mali kwasababu Mali ni daraja la kwenda hukohuko kwao hivyo usalama wa Mali ndo usalama wa nchi za Italy na Greece na hatimae nchi zote za kibabaru maana hawatutaki sisi waafrika tuendelee kwenda kwao.

Ila wanataka waendelee kutuibia na kututumia.
Mkuu average ya kipato Cha mtanzania kwa mwaka ni USD 1080.00 yaani milioni mbili na laki moja na sitini? Hilo wewe unalielewaje? Pili kamati ya makinikia ilipendekeza baadhi ya watu wachukuliwe hatua kwa kuisababishia harasa serikali kwa kuingia mikataba mibovu,je Lissu alikuwa miongoni mwa hao watu? Na je Magufuli amefanya nini?mtadanganywa sana
 
Na pia salamu zimfikie Lissu na wale waliomtuma kuwa hapa ni MOTO WA KUOTEA MBALI kwani Watanzania wana uwezo na akili za kuchambua mambo ya kisiasa na kujua mahitaji na matakwa yao na kuwa wako tayari kuilinda nchi hii kwa hali na mali. HATUDANGANYIKI na kelele zake kwa maelekezo ya wanaomlipa.

Tuna akili za kuchambua mbivu na mbichi. Belarus siyo Tanzania na hata yeye Lissu hana uwezo wa kufanya uchambuzi wa kisiasa, kitu anachoweza ni KUKARIRI vifungu vya sheria mbalimbali. Huo ndio uwezo wake otherwise ni mere noise maker!
 
Mkuu average ya kipato Cha mtanzania kwa mwaka ni USD 1080.00 yaani milioni mbili na laki moja na sitini? Hilo wewe unalielewaje? Pili kamati ya makinikia ilipendekeza baadhi ya watu wachukuliwe hatua kwa kuisababishia harasa serikali kwa kuingia mikataba mibovu,je Lissu alikuwa miongoni mwa hao watu? Na je Magufuli amefanya nini?mtadanganywa sana

Kwa jinsi nchi yetu livyovurugwa kwa miaka mingi ni vigumu kurekebisha hilo la kipato kwa kutegemea majibu ya papohapo, itachukua muda hivyo tunapaswa kujipa muda wa kutosha.

lakini kama dira ya maendeleo ya taifa inavyoelekeza Inshaalah tutafika na hata kama si raisi huyu ipo siku raisi ajae atatufikisha kwenye dola 3000 kwa mwaka.

Pili, ni kweli kamati ilitoa mapendekezo lakin hakuna anaewafahamu hao watu na kama wamechukuliwa hatua au la.

Isipokuwa ipo mahakama ya mafisadi na hadi sasa kuna watu wengi tu wamefikishwa hapo kujibu mashtaka.

Pia Tundu Lissu angekuwa ni mwanasheria wa serikali bila shaka angewajibishwa.

Raisi Magufuli amefanikisha kurekebisha sheria ya madini ndo jambo la msingi hapa kwamba, serikali na hayo makampuni tunagawana faida inavyotakiwa na pia kuna kampuni moja sasa iitwayo Twiga.

Isitoshe kule Mererani kwa mfano sasa hivi kuna udhibiti wa madini yatokayo nchini hivyo kuzuia wezi kutoka India, Kenya, Thailand na kwingine kutuibia kwenye kuwauzia madini kwa bei ndogo na pia kutorosha mipakani ndo maana sasa kuna ukuta na jeshi latulindia ule ukuta.

Sasa hizi ni juhudi ambazo mtu mwenye uelewa anapaswa angalau kupiga walau kofi moja tu latosha badala ya kupinga kila kitu kutwa kucha.

Kama alivyosema raisi kwamba hii ni vita hivyo anahitaji msaada wa kuungwa mkono badala ya anayoyafanya huyo mwanaharakati wenu Tundu Lissu.
 
Ukitujibu BEBERU ni nani tutakuelewa zaidi. Je, ni wazungu wa World Bank?, ni Wazungu hawa wa mabenki makubwa ya binafsi? Ni hawa wazungu wanaokuja kuchimba madini yetu? Je, ni Waingeleza ama Wamarekani? BEBERU ni yupi hasa?
Beberu ni Mbuzi Dume.
Yeyote anaemuita binadamu mwenzake hilo jina, hana tofauti na yule anaemuita mwenzake Nyani.
 
Wanajamvi Salaam,

Bw. Lissu katika muda wake wakufanya kampeni ya kutafuta wadhamini alisikika mara kwa mara akisema hatokubaliana na matokeo ya uchaguzi yakitangazwa iwapo kama hatotangazwa mshindi, akaenda mbele zaidi akawahamasisha wananchi waingie barabarani kupinga matokeo hayo yatakayotangazwa kinyume na matarajio yao yeye na mabeberu. Sasa hii inaonyesha ni mkakati maalum ambao tayari umeshapangwa kwa ajili ya kuivuruga amani iliyopo Tanzania.

Wananchi wa Belarus, wanaandamana kwa kupinga ushindi wa Rais wao Bw. Alexander Lukashenko, aliyechaguliwa na wananchi na kushinda kwa asilimia 80 ya kura zote. Sasa maandamano hayo yanaungwa mkono na nchi zao majirani ikiwa ni mkakati wa kibeberu kwa ajili kuifanya nchi yao isitawalike.

Angalizo kwa Lissu: Sisi Watanzania siyo wajinga kiasi hicho cha kuwafanya wananchi waandamane eti kisa hautatangazwa kama mshindi. Waeleze mabeberu maandamano wanaofanya katika nchi ya Belarus wasitarajie yatafanyika katika nchi yetu, kama walikuhaidi kukusaidia katika maandamano hayo ya kuhatarisha amani, waeleze huku Tanzania wameingia mlango ambao hawataweza kutokea.

Salaam hizi ziwafikie nyumbu wote wa ufipa. Amani haina chama.
Kwakweli mtu wa aina yako ni hatari sana kwa amani ya nchi yetu. Hivi unathubutu kweli kutunga uwongo kwenye jambo kubwa kama hili? Hivi lengo hasa la wewe kutunga uwongo kama huu ni nini hasa kama sio kuhatarisha amani ya nchi. Sisi watanzania wote tunafuatilia vyombo vya habari na hatukuwahi kabisa kumsikia Lissu akitoa kauli eti asipotangazwa mshindi sijui wataandamana bali tumemsikia akisema wakiibiwa kura wataingia barabarani.
Pengine nimekuhukumu kwa kukuonea. Pengine mwenyewe hata huna nia mbaya ya kuhatarisha amani ya nhi ikiwa utatueleza kuwa kwa uelewa wako umeona wizi wa kura na kutangazwa mshindi zina maana moja
 
Sasa kuingia barabarani si ni sawa na kuandamana au?

Na kuingia barabarani bila kibali kwa minajili ya kuhamasisha vurugu si ni kuhatarisha amani na utulivu?
 
Nilikuwa nazungumzia sababu ya kufanya hivyo. Sijui hata kama umenielewa. Soma kabla ya hiyo kuingia barabarani
 
Wanajamvi Salaam,

Bw. Lissu katika muda wake wakufanya kampeni ya kutafuta wadhamini alisikika mara kwa mara akisema hatokubaliana na matokeo ya uchaguzi yakitangazwa iwapo kama hatotangazwa mshindi, akaenda mbele zaidi akawahamasisha wananchi waingie barabarani kupinga matokeo hayo yatakayotangazwa kinyume na matarajio yao yeye na mabeberu. Sasa hii inaonyesha ni mkakati maalum ambao tayari umeshapangwa kwa ajili ya kuivuruga amani iliyopo Tanzania.

Wananchi wa Belarus, wanaandamana kwa kupinga ushindi wa Rais wao Bw. Alexander Lukashenko, aliyechaguliwa na wananchi na kushinda kwa asilimia 80 ya kura zote. Sasa maandamano hayo yanaungwa mkono na nchi zao majirani ikiwa ni mkakati wa kibeberu kwa ajili kuifanya nchi yao isitawalike.

Angalizo kwa Lissu: Sisi Watanzania siyo wajinga kiasi hicho cha kuwafanya wananchi waandamane eti kisa hautatangazwa kama mshindi. Waeleze mabeberu maandamano wanaofanya katika nchi ya Belarus wasitarajie yatafanyika katika nchi yetu, kama walikuhaidi kukusaidia katika maandamano hayo ya kuhatarisha amani, waeleze huku Tanzania wameingia mlango ambao hawataweza kutokea.

Salaam hizi ziwafikie nyumbu wote wa ufipa. Amani haina chama.
Delete ccm Oct 28
 
Back
Top Bottom