Tundu Lissu: Vincent Mashinji alikosa uadilifu ndani ya CHADEMA. Hakuna pengo kuondoka kwake

Tundu Lissu: Vincent Mashinji alikosa uadilifu ndani ya CHADEMA. Hakuna pengo kuondoka kwake

Wewe ni shabiki wa nje tu hujuwi yanayotokea ndani ya chama, visiki vya yule anayejiita mwamba. Wengi wanalalamika chini chini, hata Lissu ana malalamiko yake, alikuja mpaka Kenya akataka kukiwasha wakaenda kumpoza. Uwongo ukweli ?
Kutunga uongo kunakusaidia nini ?
 
Kiujumla mbowe alichemka kumpa mashinji .katibu Mkuu alipaswa kuwa yule jamaa Wa Moro, Marcus albanie
 
Dr.Vicent Mashinji Ni akili kubwa iliyokuwa inapotea ndani ya tope Ni moja ya katibu wakuu waliokuwa wanajua majukumu yao,Tatizo la wengi wa upinzani wanadhani KM kazi yake Ni kumtukana Rais,waziri mkuu,makamu wa Rais,Tiss, Police,Jwtz, magereza,wakuu wa mikoa na wilaya ama kuvunjwa mkono.Sorry
Ukiwa hujui majukumu ya Katibu,nakushauri kubali kuitwa Nzige tu.Thank me later
 
Kinachonisikitisha kwenye nchi hii ni kwamba mambo ya HOVYO kabisa ya mtu kuhama chama kimoja kwenda chama kingine ndizo HOJA zinazopewa FRONTLINE wakati vitu vya msingi kabisa kama vile-;
1. Kuboresha elimu
2. Kuboresha kilimo
3. Kupambana na uhaba wa maji
4. Ugumu wa maisha mtaani
5. Kudorora kwa biashara nchini
6. Kudorora kwa huduma za jamii
Badala ya mijadala yetu ijikite kwenye suruhisho wa hizo changamoto lakini sisi kila siku ni kelele za vitu vya kijinga kabisa vya watu wajinga kuhamia kwenye vyama vya siasa,hii nchi tunaipeleka wapi jamani,kwanini tunajadili vitu vya hovyo kabisa. Hebu tubadilike jamani hii nchi tunaipeleka kusiko kabisa
 
Ni dhahiri huna akili timamu au labda umelogwa ili uwe kikaragosi cha mtu ili uwe ndondocha , huo upumbavu ulioandika hapo ndio ulioandikwa kwenye Katiba ya Nchi ? hivi mnadhani waliotunga Katiba hawakuwa na akili ?
Hii katiba mnasoma juu chini au? Badala ya kuja na matusi ungekuja na vipengele vinavyotoa uhuru wa mikutano ya siasa bila kuzingatia sheria zingine za nchi ningekuelewa.

Wengi wenu mnachanganua uhuru kujieleza, uhuru wa mawazo, uhuru wa kujumuika na uhuru wa kuwa na mikutano ya hadhara ya kisiasa. Fuatili sehemu ya tatu ya katiba, pitia ibara zote kuanzia ya 18 halafu uje utuonyeshe sehemu ya mikutano ta hadhara ya siasa inapewa uhuru isio ingiliana na sheria zingine za nchi.
 
Je wanaondoka wenyewe kwa sababu ya matatizo ya Chadema ama wanalipwa ? Ukweli ni kwamba wananunuliwa , sasa mtu kama Mashinji au Waitara unamnunua ili iweje ? ukiishangaa chadema basi unatakiwa uishangae na ccm inayokubali ushauri wa Polepole wa kununua watu wasio na ushawishi wowote na kuwapa vyeo huku wanachama halali wakitoswa .
CCM tunajua imeoza, ndiyo maana hata sitaki kuipa muda wa kuijadili hapa.
Kuna mtu kahoji kama CCM kweli inaiba kura, nikamwambia CCM sio tu inaiba kura leo, imeiba kura tangu enzi za Chama kimoja katika uchaguzi wa Zanzibar, Idris Abdul Wakili hakushinda uchaguzi, enzi za kura za NDIYO/ HAPANA.Kwa aibu Wakil alikataa kugombea tena urais.

Sasa usione naisema CHADEMA ukaanza kutaja CCM. Two wrongs do not make a right. Kama CCM imeoza, CHADEMA ikianza kuonesha kuoza nayo tusiiseme?

Mimi sina ushabiki na chama chochote cha siasa, navisema vyote tu.

CHADEMA ndicho chama kilichojinadi kuwa chama mbadala.Yani kwa mtu ambaye hataki kupigia kura CCM, anaangalia chama kingine, CHADEMA kilikuwa kinara.

Sasa mtu ambaye kashaitoa CCM, anatafuta chama mbadala, utataka azungumzie habari za CCM tena? Mtu kashakubali CCM si chama, kimekosa sifa ya kuongoza, unataka azungumzie CCM bado?

Ndiyo hapo mtu anapo focus kwenye vyama mbadala, nako anaona udhaifu mtupu.

CHADEMA ina udhaifu, hili tulikubali.

Waswahili walisema, la uvundo halina ubani.

Tundu Lissu anachofanya ni kupigia ubani hili la uvundo, ili kupunguza harufu mbaya.

Danage control.

Lakini, kwa kuwa uvundo huu una harufu kali kuliko ubani, tunaoweza kunusa tunajua tu kwamba hapa uvundo unafunikwa kwa ubani, lakini harufu ya uvundo imeuzidi ubani.
 
Mbowe amehojiwa jana na Clouds FM kipindi cha Jahazi. Amesema very clear Kuwa wahuni wote wanajulikana. Hata ambao wapo kwenye negotiations wanajulikana. Lakini kama chama hawatawafukuza. Watashughulika nao kwa akili na mwishowe watajitoa wenyewe. Wakianza kufukuzwa watapata public sympathy watakapoanza kulia lia wamefukuzwa na hivyo kuondoa ajenda muhimu ya chana kwa sasa. Kwaiyo wanaofika bei wanajulikana, waliofika bei wanajulikana. Mbowe akamalizia kwa kusema Chadema ipo imara kuliko nyakati zote zile!

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwa zitto kabwe hakuwa na akili hii?
 
Tatizo la vetting hata huko lipo tena limekuwa sugu ndiyo maana teua tumbua teua tumbua teua tumbua teua tumbua teua tumbua haziishi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama chama tawala kina tatizo la vetting, hiyo ni sababu kubwa kutufanya watu tuangalie kama chama mbadala kimeweza kuondokana na tatizo hilo.

Vinginevyo, watu watasema, CCM wana tatizo la vetting, CHADEMA wana tatizo la vetting.

Sasa kwa nini tuwatoe CCM wenye tatizo la vetting, halafu tuwaweke untested CHADEMA wenye tatizo la vetting nao?

CHADEMA ilitakiwa kujionesha ina uongozi imara, usio na tatizo la kufanya vetting, na kuifanya hiyo ni sehemu ya kampeni ya uongozi bora zaidi utakaoletwa na CHADEMA.

Sasa kama CHADEMA na CCM wote wana matatizo yaleyale, kwa nini watu wabadilishe uongozi?

Ndiyo nakumbuka maneno ya rafiki yangu mmoja, haipendi kweli CCM. Kila siku anaisema.

Lakini alisema kimsingi hawezi ku recommend upinzani uchukue nchi, kwa sababu upinzani haujawa tayari kuongoza nchi.

Na hizi defections zinaonesha kwamba kuna ukweli fulani katika hii hoja.
 
Mkuu Dr Slaa aliondoka kwa presha na chuki kubwa sana , aliuacha Ukatibu Mkuu , mbona Haikuleta athari yoyote kubwa , ndio awe Mashinji ?
Hahaha, atahri kubwa unaipimaje?

CHADEMA ingeshinda na kuchukua nchi, labda ungeweza kusema kuondoka kwa Slaa hakujaleta athari kubwa.

Sasa kila mwaka mnapigwa bao, halafu unasema hakuna athari kubwa?
 
View attachment 1363963

Makamu Mwenyekiti wa Chadema Mh Tundu Lissu amesema kwamba kuondoka kwa Mashinji na waliomtangulia ndani ya Chadema , wakati tayari wamevuliwa vyeo hakuwezi kuathiri chama chake kwa lolote .

Amedai kwamba wangeweza kuathirika iwapo kama wahusika wangehamia ccm wakiwa na vyeo vyao , lakini kwa style hii hawawezi kuathiri chochote .

Lissu pia amegusia uadilifu wa Mashinji , ambapo amedai kwamba hakuwa Muadilfu ( hakufafanua )
Tungeambiwa haya akiwa bado ndani ya Chadema tungeelewa. Haya ya sizitaki mbichi hizi baki nayo huko huko!
 
Cdm Ni chama cha kisiasa sio kikundi cha kigaidi kinachopanga kupindua nchi, sasa kuna mikakati gani ya kutisha ambayo Mashinji akiijua itakuwa na madhara? Sana alichokuwa anajua ni passwords ambazo watu watareset na kuendelea na mambo mengine.
Hahaha,

Jibu lako, kama ni kweli, linaweza kuelezea kwa nini CHADEMA si tu ni chama cha upinzani siku zote, bali pia, kwa nini ni chama cha upinzani kinachozidi kuporomoka katika ushawishi.

Chama chochote cha siasa ni lazima kiwe na Politburo inayokaa inner sanctum na kufanya high level strategy meetings.

Chama kitakachokosa hilo kimekosa sifa ya kuitwa chama.

Kitakuwa ni kijiwe tu.

Sasa CHADEMA ni chama au kijiwe?
 
Uongozi ukibadilika mikakati inabadilika na mfumo unabadilika. Kwahiyo taarifa alizokua nazo ni outdated sababu Mnyika na entire crew mpya wamekuja na informants,channels,strategies na watendaji wapya kabisa so Mashinji hana analojua kuhusu uelekeo wa chama uchaguzi mkuu.

Na hii ni dunia nzima mkuu ukibadilishwa hata leo password na kila kitu vinabadilishwa kabisa ili usije kuwa threat baadae otherwise kina Zitto wangeimaliza CHADEMA wakati wa uchaguzi mkuu. Same to magufuli kapangua watu wengi sana wa awamu iliyopita huko kwenye system ili kuepuka kuhujumiwa na ''loose ends''.

Cc Titicomb
Chama kinachoweza kubadili mikakati ya muhimu na mizito kabisa kwa haraka namna hii si chama.

Unaelewa kuwa hata ile high level strategy snapshot ya chama kwa wakati fulani tu ni sensitive information?

Kwamba, mtu akipata mikakati ya chama ya mwishoni mwa mwaka jana, mwaka mmoja kabla ya uchaguzi, mwaka huu wa uchaguzi, hapo hata ukianza kubadilisha strategy ushapigwa bao kubwa sana tu?

Hususan kwa utawala huu wa Gestapo.

Mtu akiambiwa tu "Wale Chadema anayewapa hela fulani, mikkati ya usafiri anafanya fulani, fulani hana ushawishi chamani, fulani ndiye kinara anayeanzisha chokochoko za maandamano, fulani tunaweza kumnunua akaja CCM, dau lake hili, fulani aliwahi kusema anagopa sana kesi yake ikienda hivi, fulani ana mazabe fulani, hela za ruzuku zinaliwa hivi, etc"

Mpaka hapo kwa sbnapshot kama hiyo tu, CCM washajua wanakaba wapi.

Na hata ukisema ubadilishe, utabadilisha mpaka mazungumzo uliyofanya mwaka jana?
 
Hii katiba mnasoma juu chini au? Badala ya kuja na matusi ungekuja na vipengele vinavyotoa uhuru wa mikutano ya siasa bila kuzingatia sheria zingine za nchi ningekuelewa.

Wengi wenu mnachanganua uhuru kujieleza, uhuru wa mawazo, uhuru wa kujumuika na uhuru wa kuwa na mikutano ya hadhara ya kisiasa. Fuatili sehemu ya tatu ya katiba, pitia ibara zote kuanzia ya 18 halafu uje utuonyeshe sehemu ya mikutano ta hadhara ya siasa inapewa uhuru isio ingiliana na sheria zingine za nchi.
Sheria zilizo kinyume na katiba zina uhalali gani? Kama kuna sheria zinazokinzana na uhuru uliotolewa na katiba, hizo ni sheria kandamizi. Na ni kinyume na katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
 
Hahaha,

Jibu lako, kama ni kweli, linaweza kuelezea kwa nini CHADEMA si tu ni chama cha upinzani siku zote, bali pia, kwa nini ni chama cha upinzani kinachozidi kuporomoka katika ushawishi.

Chama chochote cha siasa ni lazima kiwe na Politburo inayokaa inner sanctum na kufanya high level strategy meetings.

Chama kitakachokosa hilo kimekosa sifa ya kuitwa chama.

Kitakuwa ni kijiwe tu.

Sasa CHADEMA ni chama au kijiwe?

Unapimaje cdm kuporomoka ushawishi katika mazingira haya? Au ccm ikitumia nguvu yake ya dola kufanya ushawishi wa mabavu hiyo inamaanisha cdm inakosa ushawishi? Unajua maana ya kukosa ushawishi au unapagawa na hizo swagga za ccm kufanya siasa za wazi peke yao? Umeongea kama vile cdm kina siri za hatari ambazo huyo Mashinji akienda ccm basi itakuwa ni hatari ya maana. Ni kweli anaweza kupeleka mikakati ya hapa na pale, lakini sio lolote la maana ambalo ccm kupitia nguvu yake ya dola watashindwa kujua iwapo wanataka bila msaada wa huyo Mashinji.

Kimsingi ccm wanawachukua viongozi wa cdm wakiamini kabisa wakiwapata viongozi wa cdm watawavunja moyo wapinzani wao, na washabiki wa upinzani watahamia ccm na kuikubali. Lakini ukitaka kujua ccm wanatwanga maji kwenye kinu, pitia hapa mjini uone jinsi zoezi la kuandikisha wapiga kura lilivyododa na kukosa hamasa, wakati ilitarajiwa watu wawe wengi na hamasa iwe juu. Wangewatumia Lowassa, Sumaye, Mashinji nk kuhamasisha watu wajitokeze kujiandikisha kupiga kura ili tuone wamepata watu wenye ushawishi.
 
CHADEMA imeshindwa kazi ndogo tu ya ku mobilize Watanzania kupinga katazo dhalimu na lisiloheshimu katiba ya nchi la kukataza vyama vya siasa kufanya mikutano.

Hili katazo linavunja katiba wazi.

CHADEMA mpaka leo imefyata mkia na kukubali falsafa za "hewala bwana mkubwa".

Sasa chama kama hiki kimeshindwa kutetea haki za msingi za kikatiba utaniambiaje kinazidisha ushawishi?
 
Back
Top Bottom