Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 143,138
- 288,731
- Thread starter
-
- #101
Kutunga uongo kunakusaidia nini ?Wewe ni shabiki wa nje tu hujuwi yanayotokea ndani ya chama, visiki vya yule anayejiita mwamba. Wengi wanalalamika chini chini, hata Lissu ana malalamiko yake, alikuja mpaka Kenya akataka kukiwasha wakaenda kumpoza. Uwongo ukweli ?
Hii katiba mnasoma juu chini au? Badala ya kuja na matusi ungekuja na vipengele vinavyotoa uhuru wa mikutano ya siasa bila kuzingatia sheria zingine za nchi ningekuelewa.Ni dhahiri huna akili timamu au labda umelogwa ili uwe kikaragosi cha mtu ili uwe ndondocha , huo upumbavu ulioandika hapo ndio ulioandikwa kwenye Katiba ya Nchi ? hivi mnadhani waliotunga Katiba hawakuwa na akili ?
Na wewe nimegundua sio mshirika wa ndani.Kutunga uongo kunakusaidia nini ?
CCM tunajua imeoza, ndiyo maana hata sitaki kuipa muda wa kuijadili hapa.Je wanaondoka wenyewe kwa sababu ya matatizo ya Chadema ama wanalipwa ? Ukweli ni kwamba wananunuliwa , sasa mtu kama Mashinji au Waitara unamnunua ili iweje ? ukiishangaa chadema basi unatakiwa uishangae na ccm inayokubali ushauri wa Polepole wa kununua watu wasio na ushawishi wowote na kuwapa vyeo huku wanachama halali wakitoswa .
Mbowe amehojiwa jana na Clouds FM kipindi cha Jahazi. Amesema very clear Kuwa wahuni wote wanajulikana. Hata ambao wapo kwenye negotiations wanajulikana. Lakini kama chama hawatawafukuza. Watashughulika nao kwa akili na mwishowe watajitoa wenyewe. Wakianza kufukuzwa watapata public sympathy watakapoanza kulia lia wamefukuzwa na hivyo kuondoa ajenda muhimu ya chana kwa sasa. Kwaiyo wanaofika bei wanajulikana, waliofika bei wanajulikana. Mbowe akamalizia kwa kusema Chadema ipo imara kuliko nyakati zote zile!
Sent using Jamii Forums mobile app
Kama chama tawala kina tatizo la vetting, hiyo ni sababu kubwa kutufanya watu tuangalie kama chama mbadala kimeweza kuondokana na tatizo hilo.Tatizo la vetting hata huko lipo tena limekuwa sugu ndiyo maana teua tumbua teua tumbua teua tumbua teua tumbua teua tumbua haziishi.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuongea uongo kunawasaidia nini bavicha?Kutunga uongo kunakusaidia nini ?
Hahaha, atahri kubwa unaipimaje?Mkuu Dr Slaa aliondoka kwa presha na chuki kubwa sana , aliuacha Ukatibu Mkuu , mbona Haikuleta athari yoyote kubwa , ndio awe Mashinji ?
Tungeambiwa haya akiwa bado ndani ya Chadema tungeelewa. Haya ya sizitaki mbichi hizi baki nayo huko huko!View attachment 1363963
Makamu Mwenyekiti wa Chadema Mh Tundu Lissu amesema kwamba kuondoka kwa Mashinji na waliomtangulia ndani ya Chadema , wakati tayari wamevuliwa vyeo hakuwezi kuathiri chama chake kwa lolote .
Amedai kwamba wangeweza kuathirika iwapo kama wahusika wangehamia ccm wakiwa na vyeo vyao , lakini kwa style hii hawawezi kuathiri chochote .
Lissu pia amegusia uadilifu wa Mashinji , ambapo amedai kwamba hakuwa Muadilfu ( hakufafanua )
Hahaha,Cdm Ni chama cha kisiasa sio kikundi cha kigaidi kinachopanga kupindua nchi, sasa kuna mikakati gani ya kutisha ambayo Mashinji akiijua itakuwa na madhara? Sana alichokuwa anajua ni passwords ambazo watu watareset na kuendelea na mambo mengine.
Chama kinachoweza kubadili mikakati ya muhimu na mizito kabisa kwa haraka namna hii si chama.Uongozi ukibadilika mikakati inabadilika na mfumo unabadilika. Kwahiyo taarifa alizokua nazo ni outdated sababu Mnyika na entire crew mpya wamekuja na informants,channels,strategies na watendaji wapya kabisa so Mashinji hana analojua kuhusu uelekeo wa chama uchaguzi mkuu.
Na hii ni dunia nzima mkuu ukibadilishwa hata leo password na kila kitu vinabadilishwa kabisa ili usije kuwa threat baadae otherwise kina Zitto wangeimaliza CHADEMA wakati wa uchaguzi mkuu. Same to magufuli kapangua watu wengi sana wa awamu iliyopita huko kwenye system ili kuepuka kuhujumiwa na ''loose ends''.
Cc Titicomb
Sheria zilizo kinyume na katiba zina uhalali gani? Kama kuna sheria zinazokinzana na uhuru uliotolewa na katiba, hizo ni sheria kandamizi. Na ni kinyume na katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania.Hii katiba mnasoma juu chini au? Badala ya kuja na matusi ungekuja na vipengele vinavyotoa uhuru wa mikutano ya siasa bila kuzingatia sheria zingine za nchi ningekuelewa.
Wengi wenu mnachanganua uhuru kujieleza, uhuru wa mawazo, uhuru wa kujumuika na uhuru wa kuwa na mikutano ya hadhara ya kisiasa. Fuatili sehemu ya tatu ya katiba, pitia ibara zote kuanzia ya 18 halafu uje utuonyeshe sehemu ya mikutano ta hadhara ya siasa inapewa uhuru isio ingiliana na sheria zingine za nchi.
No. huyu watampa ka cheo, even uwaziri mdogo etc. Definitely ni kuwakomoa CDM, but it does not help!
Alikuwa mzigo tu cdm huyuNo. huyu watampa ka cheo, even uwaziri mdogo etc. Definitely ni kuwakomoa CDM, but it does not help!
Hahaha,
Jibu lako, kama ni kweli, linaweza kuelezea kwa nini CHADEMA si tu ni chama cha upinzani siku zote, bali pia, kwa nini ni chama cha upinzani kinachozidi kuporomoka katika ushawishi.
Chama chochote cha siasa ni lazima kiwe na Politburo inayokaa inner sanctum na kufanya high level strategy meetings.
Chama kitakachokosa hilo kimekosa sifa ya kuitwa chama.
Kitakuwa ni kijiwe tu.
Sasa CHADEMA ni chama au kijiwe?
CHADEMA imeshindwa kazi ndogo tu ya ku mobilize Watanzania kupinga katazo dhalimu na lisiloheshimu katiba ya nchi la kukataza vyama vya siasa kufanya mikutano.Unapimaje cdm kuporomoka ushawishi katika mazingira haya? Au ccm ikitumia nguvu yake ya dola kufanya ushawishi wa mabavu hiyo inamaanisha cdm inakosa ushawishi? Unajua maana ya kukosa ushawishi au unapagawa na hizo swagga za ccm kufanya siasa za wazi peke yao? Umeongea kama vile cdm kina siri za hatari ambazo huyo Mashinji akienda ccm basi itakuwa ni hatari ya maana. Ni kweli anaweza kupeleka mikakati ya hapa na pale, lakini sio lolote la maana ambalo ccm kupitia nguvu yake ya dola watashindwa kujua iwapo wanataka bila msaada wa huyo Mashinji.
Kimsingi ccm wanawachukua viongozi wa cdm wakiamini kabisa wakiwapata viongozi wa cdm watawavunja moyo wapinzani wao, na washabiki wa upinzani watahamia ccm na kuikubali. Lakini ukitaka kujua ccm wanatwanga maji kwenye kinu, pitia hapa mjini uone jinsi zoezi la kuandikisha wapiga kura lilivyododa na kukosa hamasa, wakati ilitarajiwa watu wawe wengi na hamasa iwe juu. Wangewatumia Lowassa, Sumaye, Mashinji nk kuhamasisha watu wajitokeze kujiandikisha kupiga kura ili tuone wamepata watu wenye ushawishi.